Baadhi ya shehena ya zawadi za pikipiki watakazojishindia wateja. Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers, Chris Loiruk a...
Baadhi ya shehena ya zawadi za pikipiki watakazojishindia wateja.
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers, Chris Loiruk akiongea na wafanyakazi wakati wa uzinduzi wa promosheni.
Wafanyakazi wa Bonite wakisherekea kuzinduliwa kwa promosheni.
Baadhi ya wafanyakazi wa Bonite wakiandamana katika mitaa ya mji wa Moshi wakati wa uzinduzi
*Kuangalia mashindano ya kombe la Dunia wakiwa majumbani kwao
Wakati mashindano makubwa na maarufu ya soka ya Kombe la Dunia 2018 yanakaribia kuanza, kampuni ya Coca-Cola kupitia kampuni kiwanda cha Bonite Bottlers, imezindua promosheni kubwa itakayowawezesha watumiaji wa vinywaji yake kujishindia luninga bafa za kisasa (flat screen TV sets) zinakazowawezesha kufurahia mashindano ya soka ya Kombe la Dunia wakiwa wakiwa na familia zao majumbani kwao.
Promosheni hii mpya inajulikana kama “Mzuka wa Soka na Coka” na itanufaisha watumiaji wa vinywaji vinavyotengenezwa na kampuni ya Coca-Cola ambavyo ni Coca-Cola, Sprite, Fanta, Sparletta, Schweppes Stoney Tangawizi katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Singida.
Mbali na kujishindia luninga bapa za kisasa watumiaji wa vinywaji vya Coca-Cola kupitia promosheni hii wanayo fursa ya kujishindia zawadi kubwa ya pikipiki, fedha taslimu kuanzia shilingi 5,000/- hadi shilingi 100,000/- ikiwemo pia kujishindia soda za bure.
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya Bonite Bottlers, Chris Loiruk, amesema kampuni ya Coca-Cola ikiwa ni mdhamini mkuu wa mashindano yajayo ya Kombe la Dunia ,imewaandalia promosheni hii wakazi wa kanda ya Kaskazini ili kuhakikisha wanafurahia “Mzuka wa Soka na Coka” wakiwa majumbani kwao kupitia luninga za kisasa wakati huohuo wakiburudika na vinywaji vya Coca-Cola.
“Tukiwa wadhamini wakuu wa mashindano ya Kombe la Dunia yatakayoanza mwezi June mwaka huu tumeona kuna umuhimu wa kuwaletea wateja promosheni itakayowaunganisha na kufurahia mashindano haya makubwa duniani kupitia kunywa zetu.Zawadi za ushindi zitakuwa zinapatikana katika ganda lililopo chini ya kizibo”
Kwa upande wa zawadi kubwa za pikipiki,alisema anachotakiwa kufanya mywaji wa soda ni kukusanya maganda matatu ya chini ya vizibo yanayoonyesha sehemu 3 za pikipiki, yapo yanayoonyesha sehemu ya mbele, sehemu ya kati na sehemu ya nyuma ambayo yakiungaishwa yanaonyesha picha halisi ya pikipiki “Katika promosheni hii zawadi ya soda za bure zitatolewa madukani na zawadi za fedha taslimu, luninga na pikipiki zitakabidhiwa kwa washindi kutoka ofisi za kampuni ya Bonite,” Alisema, Chris Loiruk.
Meneja wa chapa ya Coca-Cola nchini Tanzania, Sialouise Shayo, alisema promosheni hii imelenga kuwaandaa washabiki wa soka nchini kujiandaa kufurahia mzuka wa kombe la Dunia na kufurahia mashindano haya pindi yatakapoanza.
COMMENTS