MWALIMU MPONDA WA TaSUBA HATUNAYE TENA, KIFO CHAKE CHAIGUSA SERIKALI
Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akisaini kitabu cha maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Mkufunzi wa Sanaa katika Chuo cha Sanaa na Utamaduni Bagamoyo (TaSUBa) marehemu Mwl. John Mponda leo  kabla ya ibada ya kumuaga kwa ajili ya safari ya mazishi yanayotarajiwa kufanyika Mbalizi mjini Mbeya.
HomeJamii

MWALIMU MPONDA WA TaSUBA HATUNAYE TENA, KIFO CHAKE CHAIGUSA SERIKALI

Kifo cha Mwalimu Mponda wa TaSUBa cha igusa Serikali Na Anitha Jonas – WHUSM 22/03/2018 Dar es Salaam. Serikali imetoa  pole kwa ...

TCAA YAAGIZWA KUSIMAMIA USAFIRI WA ANGAWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Kapteni mstaafu George Mkuchika akisisitiza kuhusu sheria inayotumika kutoa likizo kwa watumishi katika sekta ya umma na binafsi pale wanapojifungua. PIX2. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akisisitiza kuhusu mikakati ya Serikali kuboresha makazi ya Askari Polisi hapa nchini wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma. PIX3. Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Paramagamba Kabudi akisisitiza jambo kwa Waziri wa Madini Mhe. Anjella Kairuki wakati wa kipindi cha maswali na majibu leo Bungeni mjini Dodoma. PIX4. Sehemu ya wageni waliofika Bungeni wakifuatilia kipindi cha maswali na majibu Bungeni mjini Dodoma mapema leo. PIX5. Waziri wa Madini Mhe. Anjella Kairuki (katikati) akifurahia jambo na baadhi ya wabunge katika viwanja vya Bunge leo mjini Dodoma wakati wakielekea katika ukumbi wa Bunge mapema leo. (Picha zote na Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma)
WIZARA YAHAMSHA ARI YA WANANCHI KUSHIRIKI KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO
MAKAMU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AHUDHURIA UFUNGUZI WA MKUTANO WA CHOGM 2018


Kifo cha Mwalimu Mponda wa TaSUBa cha igusa Serikali
Na Anitha Jonas – WHUSM
22/03/2018
Dar es Salaam.
Serikali imetoa  pole kwa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo kwa kumpoteza Mwalimu mahiri John Mponda aliyekuwa balozi  wa tasnia ya Sanaa nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza katika ibada ya kumuaga marehemu huyo iliyofanyika katika Chuo cha TaSUBa Wilayani Bagamoyo kwa ajili ya kumuaga kwani anatarajiwa kuzikwa kijiji cha Mbalizi Mkoani Mbeya.
“Tunatambua mchango wa Mwalimu John Mponda katika tansia ya sanaa nchini na kupitia wanafunzi waliyopita katika mikono yake pamoja na vikundi vya vijana alivyovianzisha ambavyo amekuwa akivifundisha kazi za sanaa, hakika tumempoteza mtu makini,”alisema Mhe.Shonza.
Akiendelea kuzungumza  katika msiba huo Mheshimiwa Shonza  aliwasihi wasanii waliyopata mafunzo kutoka kwa mwalimu huyo kuwa mabalozi  kwa wasanii wenzao na kuwashauri misingi iliyobora katika katika kukuza na kuendeleza kazi za sanaa.

Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha TaSUBa Dkt.Herbert Makoye alisema kuwa marehemu mwalimu Mponda ameondoka katika kipindi walichokuwa wanamuhitaji sana kwani kwasasa taasisi hiyo ipo katika maandalizi ya Tamasha la Utamaduni la Bagamoyo ambalo nilakimataifa na hufanyika kila mwaka na yeye  alikuwa mratibu na mpaka mauti yanamfika alikuwa akiwa shughulikia maandalizi hayo.

“Kwa hakika msiba huu ni pigo kwa taasisi yetu na mwalimu huyu alikuwa kiungo miongoni mwetu na alifanya kazi yake kwa weledi na kujituma alikuwa ni mtu aliyeipenda kazi yake ,’’alisema Dkt.Makoye.

Pamoja na hayo nae Mwenyekiti wa Umoja wa Wanafunzi waliyosoma TaSUBa Deosonga Njelekela alisema kuwa mwalimu huyo kwao hakuwa tu kama mwalimu  bali alikuwa baba na mlezi kwani na alikuwa mstari wa mbele kutoa nasaha zake kwa lengo la kutaka wanafunzi wake waweze kufanikiwa zaidi.

Hata hivyo nae mtoto wa Marehemu Bi. Mary Mponda aliwashukuru watu wote waliyojitokeza kuungana nao katika msiba huo kwa imekuwa ni faraja kubwa kuona watu wakiomboleza pamoja nao baada ya kumpoteza baba yao mzazi ambaye alikuwa mlezi na nguzo ya familia.



                                  



Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MWALIMU MPONDA WA TaSUBA HATUNAYE TENA, KIFO CHAKE CHAIGUSA SERIKALI
MWALIMU MPONDA WA TaSUBA HATUNAYE TENA, KIFO CHAKE CHAIGUSA SERIKALI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhjBOBxaOHda5Y3oDqe4bV7dwxI1J3eY3stEHkD3BuC4WmCzfhx3YxU_wUoMYAuk4s1yMwG2A84dGEyFKlV4xppFz5pU9TzkFx2ntDf2NFrNFWuNnacFeVpuPmWWsjq2c9SELQuVhgmsOg/s640/PIX+1+%25285%2529.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhjBOBxaOHda5Y3oDqe4bV7dwxI1J3eY3stEHkD3BuC4WmCzfhx3YxU_wUoMYAuk4s1yMwG2A84dGEyFKlV4xppFz5pU9TzkFx2ntDf2NFrNFWuNnacFeVpuPmWWsjq2c9SELQuVhgmsOg/s72-c/PIX+1+%25285%2529.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/mwalimu-mponda-wa-tasuba-hatunaye-tena.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/mwalimu-mponda-wa-tasuba-hatunaye-tena.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy