MAKAMU WA RAIS KUONGOZA HARAMBEE UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA MACHI 16 DAR ES SALAAM

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii MKUU wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Mhandisi Mwanasha Tumbo amewaomba wananchi wa wilaya hiyo na W...




Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
MKUU wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Mhandisi Mwanasha Tumbo amewaomba wananchi wa wilaya hiyo na Watanzania kwa ujumla kuchangia ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya hiyo ambapo kesho Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye harembee ya uchagiaji fedha kufanikisha ujenzi huo.

Kwa sasa Wilaya hiyo haina Hospitali ya Wilaya na wananchi wanaohitaji huduma za afya wamekuwa wakitumia hospitali teule ya Kanisa la Anglikana ambayo imeingia mkataba na Serikali na kutokana na idadi ya wananchi wa wilayani hapo hospitali hiyo imezidiwa.
Mkuu wa Wilaya ya muheza, Hajjat Mhandisi Mwahasa Tumbo akiwaelezea jambo waandishi wa habari kuhusu harambee ya ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Muheza, inayotarijiwa kuhudhuriwa na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye hoteli ya Golden Tulip Dar es Salaam Machi 16 2018. Kushoto ni Mwenyekitiwa kamati ya Maandalizi ya Harambee, Hamisi Ngoda, Katibu Tawala wa Wilaya ya uheza Desderia Haule na Mjumbe wa kamati hiyo, Juma Mngazija (kulia). (Picha na Robert Okanda Blogs)
Hayo yamesemwa leo na Mhandisi Tumbo wakati akizungumzia harambee ya kuchangisha fedha inayotarajia kufanyika kesho jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufanikisha ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya hiyo.

Mhandisi Tumbo amesema kutokana na Wilaya ya Muheza kutokuwa na Hospitali ya Wilaya tangu kuanzishwa kwake mwaka 1974, wananchi wamekuwa wakiteseka pindi wanapohitaji huduma za afya na hivyo wakaamua kuchanishana fedha ili kuanza ujenzi wa hospitali hiyo.

Amefafanua tayari wananchi na wadau wa maendeleo wilayani Muheza mkoani Tanga na Watanzania kwa ujumla wameanza kuchingiaa ujenzi huo na hadi kukamilika kwake zinahitajika fedha Sh.bilioni 11.1, hivyo wakati wakisubiri fedha za Serikali Kuu na zile za kwenye bajeti wameamua kuanza kwa kuchangisha fedha hizo.

"Kesho tutakuwa na harambee itakayofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia saa 12 jioni ambapo wananchi wa Wilaya ya Muheza wanaoishi Dar es Salaam pamoja na watanzania wengine tunaomba wajitokeze kuchanga fedha kwa ajili ya ujenzi wa hospitali mpya ya wilaya.

"Mgeni rasmi kwenye tukio hilo la harembee ya kuchangisha fedha atakuwa Makamu wa Rais ,Mama Samia Suluhu Hassan. Kwa wachangiaji ambao tumewapa kadi ya kuja kwenye harembee hiyo kila mchangiaji atachangia kuanzia Sh.milioni moja kwa walio na kadi.Na wote ambao tumewaalika kesho wana kadi za mualiko,"amsema.

Amefafanua kwa wale ambao wanahitaji kadi ni vema wakawasiliana naye kwa kutumia namba yake ya simu ya mkononi ya 0713 341937 ili wapatiwe kadi huku akifafanua pia mbali ya wale ambao watafika kesho kwenye harambee hiyo pia wameandaaa utaratibu mwingine wa kuchangia ujenzi huo.

Mhandisi Tumbo amesema ili kufanikisha ujenzi huo wanapokea mchango wa kiasi chochote cha fedha na hao wachangie kupitia Tigopesa au M-pesa kwa kutumia namba 395533 ambayo kumbukumbu namba ya kampuni ni 123.

"Tunatambua jitihada za Serikali katika kutatua changamoto kwenye sekta ya afya, na hasa Muheza lakini kwa upande wetu tumeamua kuanza kwa kuchangishana, wapo wanaotoa fedha, wapo wanaochangia kokote, mchanga , saruji na vifaa vingine vya ujenzi.Tumeanza vizuri kwani tayari msingi wa wadi ya akina mama na watoto umejengwa na lengo letu hadi Oktoba mwaka huu tuwe tumekamilisha ili wananchi wapate huduma za afya.

"Tukifanikiwa kuwa na Hospitali ya Wilaya Muheza mwananchi anayehitaji huduma za matibabu ya afya atakuwa na nafasi ya kuchagua aende kwenye Hospitali ya Anglikana au ya Wilaya.Niishukuru Hospitali ya Anglikana kutokana na kutoa huduma za tiba kwa wananchi wa Muheza,"amesema Mhandisi Tumbo.

Pia amesema wakati wanaendelea kutafuta fedha kujenga Hospitali ya Wilaya ya Muheza, wanaendelea na jitihada za kujenga zahanati na ujenzi huo unaendelea kwa kasi kutokana na wananchi kuhamasika kuchangia ili kuondoa changamoto ya uhaba wa zahanati za vituo vya afya.

Wana habari wakihudhuria mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya muheza, Hajjat Mhandisi Mwahasa Tumbo jijini Dar es Salaam leo. 

Mkuu wa Wilaya ya muheza, Hajjat Mhandisi Mwahasa Tumbo akizungumza na  wandishi wa habari waliohudhuria mkutano wa  jijini Dar es Salaam leo. 


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS KUONGOZA HARAMBEE UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA MACHI 16 DAR ES SALAAM
MAKAMU WA RAIS KUONGOZA HARAMBEE UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA YA MUHEZA MACHI 16 DAR ES SALAAM
https://i.ytimg.com/vi/5fBTbKHEvJc/hqdefault.jpg
https://i.ytimg.com/vi/5fBTbKHEvJc/default.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/makamu-wa-rais-kuongoza-harambee-ujenzi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/makamu-wa-rais-kuongoza-harambee-ujenzi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy