CHUO CHA VTC MDABULO KIMEKUWA MKOMBOZI KWA WANAFUNZI YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MKOANI IRINGA.
HomeJamii

CHUO CHA VTC MDABULO KIMEKUWA MKOMBOZI KWA WANAFUNZI YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MKOANI IRINGA.

K atibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akiwa kwenye moja ya ma...

WIZARA YA AFYA ZANZIBAR NA BOHARI YA DAWA (MSD) WASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO
ESRF IKISHIRIKIANA NA PROFESA SANG LEE (KOREA KUSINI) IMEANDAA MHADHARA WA KUBADILISHANA UZOEFU
DKT MWANJELWA KUZURU CHINA KWA LENGO LA KUBORESHA MASHIRIKIANO KATI YA SERIKALI YA CHINA NA TANZANIA

Katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akipata maelezo kutoka chumba cha kompyuta ambacho nacho kipo chuoni hapo
 Katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akiwa kwenye chumba cha mapishi ambako wanafunzi wa fani ya upishi huwa wanajifunza kwa vitendo.
  Katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye maonyesho hayo akiwa kwenye karakana ya umeme
 Hii ni karakana ya useremala ambayo pia inawaongezea ujuzi wanafunzi wa fani hiyo ikiwa na vifaa vya kisasa kabisa
 
Na Fredy Mgunda,Iringa.

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania kupitia
chuo cha ufundi VTC Mdabulo kilichopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa linawasaidia
watoto yatima na walio kwenye mazingira magunu kwa kuwapatia elimu ya ufundi bure.





Akizungumza
na blog Mkurugenzi mtendaji wa R.D.O Fidelis Filipatali alisema kuwa shirika
hilo linawasomesha wanafunzi bure wanatoka katika mazingira magumu na watoto
yatima ili kuwapa elimu itakayowakomba katika maisha.





“Lengo
letu ni kuhakikisha wanafunzi walioshindwa kuendelea na masomo mengine kwenye
vyuo vingine wanapata nafasi katika chuo chetu hiki ambacho kinagharama nafuu
na kinatoa elimu bora ya ufundi ambayo inatamsaidia huko mbele kwenye maisha
yake” alisema Filipatali





Filipatali
alisema kuwa shirika hilo limebeba dhima ya Rural Devolopment Organization
(RDO) kwa kutoa ujuzi endelevu kwa jamii ili kuondokana na kuwa tegemezi katika
maisha na kuishi kwa kujitegemea kutokana na ujuzi unaopatikana chuoni hapo.





“Chuo
cha ufundi stadi cha RDO VTC na shirika kwa ujumla vinanuia kuinua jamii kutoka
a hali ya chini kiuchumi na kufikia hali nzuri ya kimaisha na ndio maana tupo
huku vijijini ambako ndio kuna wananchi wengi wa hali hiyo” alisema Filipatali





Lakini
Filipatali alisema kuwa chuo hicho kimelenga kuwapa ujuzi wa muda mfupi na muda
mrefu kwa lengo la kuwasaidia kuendelea kufanya shughuli nyingine za
kimaendeleo.





“Tunatoa
ujuzi kwa njia tofauti tofauti hivyo tunapoona kuwa wanafunzi wanauwezo wa
kujitegemea na wapo tayari kwenda kujitegemea huwa tunawaruhusu ili kupisha
nafasi kwa wanafunzi wengine kupata ujuzi wa kiufundi” alisema Filipatali





Filipatali
alisema kuwa wanafunzi wawapo chuoni hapo wanajifunza ufundi
bomba,kuchomelea,ufugaji wa ng’ombe,upishi,ushonaji,kilimo,elimu ya kompyuta useremala,ufundi
chuma ufundi uashi na ufundi umeme.





“Sasa
wanafunzi yeyote Yule akitoka hapa katika chuo chetu anaweza kujitegemea kwa
kuwa atakuwa ameshapata ujuzi kwa vitendo anaweza kufanyia kazi mahali popote
pale atakapo amua kuweka makzi yake” alisema Filipatali





Aidha
Filipatali alisema kuwa vijana wanatakiwa kujituma kwa kufanya kazi na kuacha
kuwa tegemezi katika jamii.





Naye
katibu wa mbunge wa jimbo la mufindi kaskazini Baptist Mdende amewataka
wananchi kuwapeleka watoto kupata elimu ya ufundi katika chuo hicho ambacho
kinatoa elimu kwa gharama nafuu.





“Haiwezekani kuwa chuo hiki kipo hapa jimboni kwetu lakini wanafunzi wanaosoma hapa wanatoka mbali na kuja kuchukua ujuzi huu wakati sisi wazawa tunawaficha watoto wetu tabia kama hii haikubariki hata kidogo hivyo nawaomba wananchi na viongozi kuhakikisha vijana wetu wanapata elimu ya ufundi katika chuo hiki” alisema Mdende.


Mdende alisema kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha hivyo aliwashukuru shirika lisilo la kiserikali la Rural Development Organization (RDO) Tanzania kupitia chuo cha ufundi VTC Mdabulo kwa kutoa elimu bure kwa wanafunzi yatima na wanaishi katika mazingira magumu.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: CHUO CHA VTC MDABULO KIMEKUWA MKOMBOZI KWA WANAFUNZI YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MKOANI IRINGA.
CHUO CHA VTC MDABULO KIMEKUWA MKOMBOZI KWA WANAFUNZI YATIMA NA WANAOISHI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU MKOANI IRINGA.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEihcKgoI3XTSO1A0OmuSKvjKfK9m5N6LlCN0CRvtA2vIJNTUnQ07HOctI1_dFrJT8RZ20k305Q_tnGk9YPAX9YeoHJJpIwQIZ2hseZzPOqkzbjO9kLTTdkprPoloZUyeOeIK34DJwEh0ZwP/s640/IMG_0535.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEihcKgoI3XTSO1A0OmuSKvjKfK9m5N6LlCN0CRvtA2vIJNTUnQ07HOctI1_dFrJT8RZ20k305Q_tnGk9YPAX9YeoHJJpIwQIZ2hseZzPOqkzbjO9kLTTdkprPoloZUyeOeIK34DJwEh0ZwP/s72-c/IMG_0535.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2018/03/chuo-cha-vtc-mdabulo-kimekuwa-mkombozi.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2018/03/chuo-cha-vtc-mdabulo-kimekuwa-mkombozi.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy