WACHUUZI WANAWAKE WA SAMAKI WAELEZA ATHARI ZAKE KWA BIASHARA Na Gladness Mbisse wa Okanda Blogs WAJASIRIAMALI Wanawake wanaojishug...
WACHUUZI
WANAWAKE WA SAMAKI WAELEZA ATHARI ZAKE KWA BIASHARA
Na
Gladness Mbisse wa Okanda Blogs
WAJASIRIAMALI
Wanawake wanaojishughulisha na biashara ya ununuzi wa dagaa mchele kwenye soko
la samaki la Masasani, Dar es Salaam wamelalamikia upungufu wa bidhaa hiyo unaosababishwa
na mabadiliko ya hali ya hewa na tabia Nchi.
Sekta
hiyo kwa sasa ni moja kati ya sekta zinazoathiriwa na mabadiliko ya hali ya
hewa yanayosababisha upungufu mkubwa wa samaki hao baharini kwa ujumla hasa
katika Pwani ya Bahari ya Hindi.
Akizungumza
na Blog hii, mmoja kati ya wajasiriamali hao, Mariam Abdul aliweka wazi kuwa
kwa sasa biashara imekuwa ngumu kwa sababu za upungufu wa bidhaa hiyo ambao
umepelekea nyongeza ya gharama za uendeshwaji wa biashara hiyo.
Alisema,
tofauti na ilivyokuwa awali kwa sasa ndoo moja ya ujazo wa lita 20 ya samaki
inauzwa hadi Sh 50,000 hiyo ni mbali na fedha za kuparulia samaki hao na hivyo
fedha kwa shughuli nzima za ununuzi na uandaaji wa samaki zinakuwa juu.
Alisema,
pia kuna gharama za kununulia mafuta ya kukaangia samaki hao, mkaa bado na
ushuru wa biashara hiyo ni kabla ya kuingia sokoni na kumuuza samaki ambapo pia
kuna ushindani wa biashara.
"Sasa
ukiangalia gharama za kuandaa tu kuanzia kununua, kusafisha na kupika inakuwa
ni ngumu kwa kuwa awali bei ya kununua imeongezeka ikilinganishwa na ya sasa,
hii inamaanisha kuwa hata sisi tunatakiwa kuja kuuza kwa bei ya juu, sasa je
wanunuzi wapo?". alihoji mama huyo kwa masikitiko.
Kwa
upande wa wavuvi nao wameonesha kuguswa na upungufu wa dagaa hao ambapo mvuvi
Juma Hemedi alisema kwa sasa wavuvi hulazimika kwenda umbali mkubwa zaidi
kutafuta samaki ikiwamo aina hiyo ya samaki yaani dagaa mchele.
Alisema"Yani
kwa sasa inabidi kwenda mbali zaidi kutega nyavu ili angalau kuona kama
tunapata samaki wengi, kwa sasa tunatega nyavu usiku na mchana na tukirejea
unakuta napata ndoo mbili kubwa za dagaa mchele"
Blog
hii ilishuhudia mnada wa samaki sokoni hapo na kisha kubaini ndoo ya samaki ya
lita 20 iliyokuwa ikiuzwa kwa Sh 30,000 imepanda na kwa sasa inauzwa Sh 60,000.
Wanawake
walioathiriwa zaidi wale kutokea maeneo ya Msasani, Kinondoni, Mikocheni na
Magomeni.
Wavuvi wakiwa katika harakati za uvuvi jijini Dar es Salaam. |
Mmoja wa wachuuzi wa dagaa mchele akiwa andaa baada ya kufanya manunuzi katika eneo la Msasani jijini Dar es Salaam. |
Mmoja wa wachuuzi wa dagaa mchele akiwaandaa baada ya kuwanunua eneo la Msasani jijini Dar es Salaam. (Picha na Glads Mbise wa Okanda Blogs) |
COMMENTS