Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akifungua Kikao Kazi cha siku mbili cha kujadili masuala ya Utawala na Rasilimali ...
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akifungua Kikao Kazi cha siku mbili cha kujadili masuala ya Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara , Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora kinachofanyika Mjini Dodoma, akisisitiza umuhimu wa Maafisa Utumishi kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuongeza tija katika kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwa hiyo ndiyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akifungua Kikao Kazi cha siku mbili cha kujadili masuala ya Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara , Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora kinachofanyika Mjini Dodoma, akisisitiza umuhimu wa Maafisa Utumishi kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuongeza tija katika kutoa huduma kwa wananchi kwa kuwa hiyo ndiyo dhamira ya Serikali ya Awamu ya Tano.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Musa Iyombe akizungumza wakati wa ufunguzi wa Kikao Kazi cha siku mbili cha kujadili masuala ya Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara , Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaakilichoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora kinachofanyika Mjini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wa Kikao Kazi cha siku mbili cha kujadili masuala ya Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara , Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora kinachofanyika Mjini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa Kikao Kazi cha siku mbili cha kujadili masuala ya Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara , Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora kinachofanyika Mjini Dodoma.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Bw. Mathias Kabunduguru akizungumza wakati wa ufunguzi Kikao Kazi cha siku mbili cha kujadili masuala ya Utawala na Rasilimali Watu katika Wizara ,Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoandaliwa na TAMISEMI kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa umma na Utawala Bora kinachofanyika Mjini Dodoma.
....................................................................................
Maafisa Utumishi Waaswa Kuzingatia Weledi Katika Kutekeleza Majukumu Yao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amewataka Maafisa
Utumishi wa Mikoa na Halmashauri zote nchini kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili
kuongeza ari ya watumishi wa umma katika kutoa huduma zenye ubora kwa wananchi.
Akizungumza wakati akifungua Kikao Kazi cha Siku mbili kilichowahusisha
Wakurugenzi wa Rasilimali watu wa Wizara zote, Idara zinazojitegemea na Maafisa
Utumishi wa Halmashauri zote hapa nchini mapema leo mjini Dodoma Waziri Jafo
amesema kuwa ni dhamira ya Serikali kuona changamoto za Watumishi wa Umma
zinatatuliwa kwa wakati.
“Maafisa Utumishi mnalo jukumu kubwa lakuwasaidia watumishi katika maeneo yao
kwa kufanya kazi zenu kwa kuzingatia weledi, kuepuka rushwa, vitendo vya upendeleo
na mambo yote yanayoweza kuchafua taswira ya Serikali kupitia huduma mnazotoa”
Alisisitiza Mhe. Jafo
Akifafanua zaidi Waziri Mhe. Jafo amesema kuwa wajibu wa Maafisa Utumishi ni kuwa
Kiungo kati ya Wakurugenzi na watendaji wa Taasisi hali itakayosaidia kupunguza au
kuondoa malalamiko yanayofikishwa Ofisi ya Rais TAMISEMI.
Aliongeza kuwa Maafisa Utumishi wanajukumu kubwa katika kuhakikisha watumishi
wanapandishwa madaraja kwa wakati, wanathibitishwa kazini kwa wakati ili
kuwaongezea morali kwa watumishi hali itakayoongeza ubora wa huduma zinazotolewa
kwa wananchi.
Pia aliwaasa Maafisa Utumishi kuhakikisha kuwa Wanatunza taarifa zote za
Watumishi kwa kuzingatia sheria , Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma ili kulinda
maslahi mapana ya nchi.
Kwa upande Wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Musa Iyombe
amewataka Maafisa Utumishi wote kufanya kazi kwa kuzingatia kuwa Serikali ya
Awamu ya Tano inalenga kuleta mabadiliko kwa wananchi kwa kuwapa huduma bora.
Aidha, Mhandisi Iyombe aliwaasa kuacha kufanya kazi kwa mazoea hali inayopelekea
kuwepo kwa malalamiko mengi kutoka kwa watumishi na hivyo kuzorotesha kasi
yakuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande wake Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Bw.
Mathias Kabunduguru akizungumza katika Kikao Kazi hicho amesema kuwa baadhi ya
masuala yanayoleta kero kwa watumishi wa Umma ni pamoja na Mamlaka za Ajira
kukataa kuidhinisha au kupitisha barua za watumishi kuhama, hivyo aliwaasa Maafisa
hao kutozuia maombi ya watumishi wanaoomba kuhama.
“Mamlaka husika inaweza kuweka maoni yakuomba mbadala wa Mtumishi
anayeondoka na sikuzuia barua yake yakuomba uhamisho kwa kuwa uhamisho wa
watumishi unajengwa kwa Misingi ifuatayo, kwanza mtumishi anayohaki ya kufanya
kazi popote,Uhamisho hujenga Afya ya Utumishi kwa ujumla na pia swala hilo husaidia
Kujenga umoja wa Kitaifa.
Aliongeza kuwa Kikao Kazi hicho kitakuwa chachu ya kuimarisha
Uadilifu,Uwajibikaji,Uwazi, na misingi mingine ya Utawala Bora.
’’Pamoja na Kukamilika kwa zoezi la uhakiki wa Vyeti vya Kidato cha nne, Sita, Ualimu
na Vyuo Vikuu bado wapo waajiri aidha kwa makusudi au kwa bahati mbaya
wameendelea kuwafumbia macho watu wenye vyeti bandia ambapo wiki iliyopita
tulilazimika kuchukua hatua kali dhidi ya Maafisa Utumishi wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kwimba kutokana na kuficha watu wenye vyeti Bandia” Alisisitiza Bw. Kabunduguru.
Akizungumzia swala la kutambua mchango wa watumishi wanaofanya kazi kwa bidii
Bw. Kabunduguru amesema linaongeza ari yao katika kutekeleza majukumu yao hivyo
ni vyema utaratibu wa kuwatambua hata kwa kuwaandikia barua za kutambua mchango
wao na pia kuwaadhibu watumishi wazembe wasiotekeleza majukumu yao.
Kikao Kazi hicho cha siku Siku mbili kilichowahusisha Wakurugenzi wa Rasilimali watu
wa Wizara zote, Idara zinazojitegemea na Maafisa Utumishi wa Mikoa, Halmashauri
zote hapa nchini kinafanyika mjini Dodoma kimeandaliwa kwa ushirikiano wa Ofisi ya
Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma na Utawala bora na Ofisi ya Rais TAMISEMI
kikiwa ni sehemu ya mkakati wa Serikali kuimarisha utendaji na huduma zinazotolewa
kwa wananchi.
COMMENTS