Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni pamoja na waratibu wa Mradi wa DMDP wakikagua b...
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kinondoni pamoja na waratibu wa Mradi wa DMDP wakikagua baadhi ya barabara zinazojengwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo amefurahishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji la Dar as salaam (DMDP) unaotekelezwa katika Manispaa ya Kinondoni, Ilala, na Temeke.
Waziri Jafo ameonyesha kulidhishwa na maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo alipotembelea Manispaa ya Kinondoni leo na kukuta jengo la Ofisi na maabara lipo katika hatua ya mwisho kukamilika huku baadhi ya barabara zimeshakamilika na barabara zingine zipo katika hatua mbalimbali ya ujenzi.
Katika ziara hiyo, Waziri Jafo amefanikiwa kutembelea barabara za Makumbusho, Mwenge viwandani, na Nzasa, pamoja na Ofisi mpya zilizojengwa eneo la Magomeni.
Akizungumza mara baada ya kukagua, Jafo amewataka wasimamizi wa mradi huo kuendelea kusimamia ubora wa miundombinu inayojengwa ili iweze kidumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wake, Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Ally Hapi amemuhakikishia Waziri Jafo kwamba amejipanga vyema na timu yake wilayani kinondoni ili mfano kwa wilaya zingine katika kutekeleza mradi huo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI Selemani Jafo akikagua tabaka la lami na mifereji inayojengwa kupitia mradi wa DMDP.

Baadhi ya barabara zinazoendelea kujengwa wilayani Kinondoni kupitia mradi wa DMDP.
COMMENTS