VIJANA WAKUMBUSHWA WAJIBU WA KUTAMBUA NAFASI ZA UONGOZI KATIKA JAMII

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM 16.12.2017 VIJANA nchini wametakiwa kutambua wajibu wao katika Taifa kwa kutumia fursa zinazojit...



Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM
16.12.2017

VIJANA nchini wametakiwa kutambua wajibu wao katika Taifa kwa kutumia fursa zinazojitokeza kuwania nafasi  mbalimbali za Uongozi katika jamii ili kutetea maslahi na agenda mbalimbali zinazogusa  maendeleo yao.

Hayo yamesemwa leo Jumamosi (Desemba 17, 2017) Jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Ushawisihi na Utetezi wa Taasisi ya Vijana ya TYVA, Yusuf Bwango wakati wa mdhahalo wa vijana uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao.
Kwa mujibu wa Bwango alisema tafii mbalimbali zimebaini kuwa Vijana wengi wamekuwa na mtazamo hasi kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za Uongozi hususani Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na kubaki nyuma katika nafasi hizo huwaniwa na kushindaniwa na Wazee pekee.
“Tumefanya mdahalo huu kwa malengo ya kuwajengea uwezo vijana kutambua kuwa wao ndio Viongozi wa baadae na hili litaanzia katika chaguzi mbalimbali zinazofanyika katika ngazi za kijamii ikiwemo chaguzi za Serikali za Mitaa” alisema Bwango.
Bwango alisema umefika wakati kwa Vijana wa Kitanzania kuweza kutumia majukwaa mbalimbali ili kuweza kubadili fikra na mitazamo yao kuhusu mifumo ya kiutawala na kutumia majukwaa hayo kuunda vyombo imara vitakavyoweza kuwasilisha na kupaza sauti zao.
Aliongeza kuwa mdahalo huo pia umekusudia kuwawezesha vijana kupata taarifa mbalimbali kuhusu nafasi ya vijana kitaifa na kimataifa pamoja na juhudi mbalimbali zilizochuliwa na Serikali kuwasaidia vijana kuweka kupaza sauti zao ikiwemo uanzishaji wa vyombo maalum vya utetezi wa Vijana ikiwemo Mabaraza ya Vijana.
Akifafanua zaidi Bwango alisema kupitia mitandao hiyo Vijana wataweza pia kuwasiliana na kuunganisha nguvu ya pamoja itakayowezesha kujadili changamoto na mikakati mbalimbali itakayowawezesha kuwaletea maendeleo yao kupitia Nyanja za kisiasa, kijamii na kiuchumi.
Alisema tangu Mwezi Julai hadi Novemba, mwaka huu TYVA imeweza kutoa elimu ya uraia kwa vijana wa Mikoa mbalimbali nchini ikiwemo Dodoma, Dar es Salaam, Morogoro, Tanga, Pwani, Zanzibar na kuwawezesha vijana kutambua wajibu, nafasi na haki za kikatiba waliyonayo katika Taifa.
Bwango alisema katika midahalo hiyo iliyoendeshwa na TYVA kwa kushirikana na Mamlaka mbalimbali za Serikali, vijana wengi waliweza kupatiwa elimu ya uraia pamoja na fursa mbalimbali zinazoweza kuwakwamua kiuchumi ikiwemo elimu kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Kwa upande wake, Bi. Sumaiya Mahmoud kutoka Taasisi ya Mwanamke na Uongozi alisema mapambano ya harakati za ukombozi katika jamii hususani kwa wanawake zitafanikiwa kwa kujenga mkakati wa pamoja wa ushawishi utakaoweza kuondoa vikwazo mbalimbali vilivvyopo kaika mfumo ya kiutawala.
“Ili kujikwamua na kufikia na juu katika ngazi za maamuzi ni wajibu wa wanawake wote kuunda mkakati wa pamoja na kuacha kusubiri na tufute dhana ya mwanamke ni kiumbe dhaifu” alisema Sumaiya.  

   Sumaiya Mahmoud kutoka Taasisi ya Mwanamke na Uongozi akichangia hoja wakati wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.




Baadhi ya Vijana kutoka sehemu mbalimbali za Jijini wakifuatilia mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.



 Oscar Munga akichangia hoja wakati wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.



Anna Winstone akichangia hoja wakati wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam.



Mmoja wa washiriki wa mdahalo wa vijana ulioandaliwa na Taasisi ya Vijana ya TYVA uliolenga kuwajengea uwezo wa kutumia mitandao ya kijamii katika kutetea maslahi yao. Mdahalo huo ulifanyika leo Jumamosi Desemba 16, 2017 katika hoteli ya Regency Park Jijini Dar es Salaam. (PICHA NA MPIGAPICHA WETU)



COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: VIJANA WAKUMBUSHWA WAJIBU WA KUTAMBUA NAFASI ZA UONGOZI KATIKA JAMII
VIJANA WAKUMBUSHWA WAJIBU WA KUTAMBUA NAFASI ZA UONGOZI KATIKA JAMII
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjq4sRze-jIEBWIWNYgCosku3W5DzlfNC2qjZZdoESlM-cpDLs5uJdUXglCxzyKSor0nuic4wZTsoBnqb-JgDLyuMTa4QqCXI5J337w_dE8ch3TFRjG21oS6QQeNofZRx7OEHEE9rFwqUk/s640/1..JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjq4sRze-jIEBWIWNYgCosku3W5DzlfNC2qjZZdoESlM-cpDLs5uJdUXglCxzyKSor0nuic4wZTsoBnqb-JgDLyuMTa4QqCXI5J337w_dE8ch3TFRjG21oS6QQeNofZRx7OEHEE9rFwqUk/s72-c/1..JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/vijana-wakumbushwa-wajibu-wa-kutambua.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/vijana-wakumbushwa-wajibu-wa-kutambua.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy