UHAMIAJI TANGA YAWAONYA VIONGOZI WA VITONGOJI NA VIJIJI VILIVYOPO MIPAKANI WANAOUZA ARDHI KWA WAGENI”
HomeJamii

UHAMIAJI TANGA YAWAONYA VIONGOZI WA VITONGOJI NA VIJIJI VILIVYOPO MIPAKANI WANAOUZA ARDHI KWA WAGENI”

VIONGOZI wa Vitongoji na Vijiji vilivyopo kwenye mipaka mkoani Tanga wameonywa kuacha tabia ya kuuza ardhi kwa wageni wanaofika kwenye...

DK. KIGWANGALLA AWATAKA WALIOVAMIA KIWANJA CHA MAMLAKA YA HIFADHI YA NGORONGORO KILICHOPO NJIRO, JIJINI ARUSHA KUJIANDAA KISAIKOLOJIA
NECTA YATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
JESHI LA ZIMAMOTO NA UKOAJI HALIFANYI BAISHARA YA KUREKEBISHA VIZIMA MOTO 'FIRE EXTINGUISHER'


VIONGOZI wa Vitongoji na Vijiji
vilivyopo kwenye mipaka mkoani Tanga wameonywa kuacha tabia ya kuuza
ardhi kwa wageni wanaofika kwenye maeneo yao badala yake hakikishe
wanatoa taarifa wanapowaona watu wasiowajua ili kuweza kukomesha vitendo
vya wahamiaji haramu.



Hayo yalisemwa na Ofisa Uhamiaji Mkoa wa Tanga Crispian Ngony’ani wakati
akizungumza na vyombo habari ambapo alisema viongozi hao wamekuwa ni
tatizo kubwa badala ya kukemea vitendo vya wahamiaji haramu lakini
wamekuwa wakiwakumbatia kwa kuwapatia ardhi jambo ambalo ni kosa
kisheria.



Alisema utafiti walioufanya mpakani mwa Kenya na Tanzania Horohoro
wamebaini idadi kubwa ya wakenywa wameuziwa ardhi katika maeneo hayo na
wanaishi nchini kinyume cha sheria huku akiwataka viongozi hao kuachana
na vitendo hivyo kabla hawajakamatwa na kupelekwa kwenye vyombo vya
dola.



“Tatizo kubwa viongozi wa vitongoji na vijiji badala ya kumemea uuzaji
wa ardhi kinyemele hivyo napenda kutoa onyo kwao kuacha tabia hiyo kwani
sisi kama idara ya uhamiaji tupo macho kuhakikisha wale wote
wanaohusika na vitendo hivyo tunawachukulia hatua “Alisema.



Alisema viongozi hao badala ya kukemea uzaji wa haramu ardhi kwa wageni
wao wamekuwa mstari wa mbele kuwakarabisha kwenye maeneo hayo bila
kutambua kufanya hivyo ni makosa kisheria hivyo kuwaonya kuacha vitendo
vya namna hiyo mara moja.



“Pindi wanapomuona mgeni au raia anauza ardhi watoe taarifa kwenye
vyombo vinavyo husika ikiwemo idara ya uhamiaji tukishirikiana kwa
mtindi huo tutaweza  kukomesha vitendo vya watu kuvamia ardhi yetu na
kuishi kinyume cha sheria tu “Alisema Ofisa Uhamiaji huyo.



Wakati huo huo,Ofisa Uhamiaji huo alisema katika kipindi cha mwaka 2017
wamekamatwa watanzania 61 kwa kuvunja sheria za uhamiaji ambapo kosa
kubwa ni kushiriki vitendo viovu vya kuwasafirisha wahamiaji hao katika
maeneo mbalimbali na kuwaingiza nchini.



Alisema hasa wahamiaji ambao ni raia kutoka nchini Ethiophia

wanaonekana wana biashara kubwa sana kwa baadhi ya watu mkoani Tanga kwa
kwenda nchini Kenya  kuwachukua kwa kufanya udalali na kuwapitisha
kwenye njia za panya hadi kwenye maeneo wanayotaka kufika.



Aidha alisema kutokana na hali hiyo idara hiyo imeweka mikakati kabambe
ya kuhakikisha wanakomesha vitendo vya namna hiyo kwa kuongeza udhibiti
wa watu wanaoingia nchini kwa kushirikiana na vyombo vya vyengine vya
dola.



Hata hivyo alisema katika kipindi hicho kesi 28 zimefunguliwa ambazo
zilikuwa zinawahusu watanzania na zilizokuwa zikiendelea ni 10, nne
zilikwisha, mbili zilifutwa na moja iko kwa wakili wa serikali na
nyengine moja ipo uhamiaji. (Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya
Tanga Raha)
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UHAMIAJI TANGA YAWAONYA VIONGOZI WA VITONGOJI NA VIJIJI VILIVYOPO MIPAKANI WANAOUZA ARDHI KWA WAGENI”
UHAMIAJI TANGA YAWAONYA VIONGOZI WA VITONGOJI NA VIJIJI VILIVYOPO MIPAKANI WANAOUZA ARDHI KWA WAGENI”
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi2OglOCI66Jdi1XKkWnXfts70pgsIKoWOyKMc0SodQr9ziKHZf8EhixwL6iMrEGH3v4htAnXfJVr4Y8qgg_D5e_8XK343GeWniruGp4XWhFIqzLb2pUO_z8CJ93D0Mnp_hFpEfKrNDic0a/s640/IMG_1796.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi2OglOCI66Jdi1XKkWnXfts70pgsIKoWOyKMc0SodQr9ziKHZf8EhixwL6iMrEGH3v4htAnXfJVr4Y8qgg_D5e_8XK343GeWniruGp4XWhFIqzLb2pUO_z8CJ93D0Mnp_hFpEfKrNDic0a/s72-c/IMG_1796.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/12/uhamiaji-tanga-yawaonya-viongozi-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/12/uhamiaji-tanga-yawaonya-viongozi-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy