MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NI JESHI LA MAENDELEO YA WATU: NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI NZUNDA
Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Tickson Nzunda akizungumza na Maafisa Maendeleo ya Jamii katika mkutano wa mwaka wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii na kuwaasa kuleta mabadiliko katika maeneo yao kwani wao ni wanajeshi wa maendeleo. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW )
HomeJamii

MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NI JESHI LA MAENDELEO YA WATU: NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI NZUNDA

Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW  Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wana jukumu la kuhamasisha wananchi kubadili fikra zao ili wawe na...

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NCHINI TUCTA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM
WATANZANIA WATAKIWA KUENDELEA KUIAMINI SERIKALI-MAJALIWA
MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA AMUAGIZA KAMISHNA MKUU WA TRA KUKUTANA NA WAFANYABIASHARA MARA KWA MARA



Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW 

Wataalam wa Maendeleo ya Jamii wana jukumu la kuhamasisha wananchi kubadili fikra zao ili wawe na mtazamo chanya unaowapa hamasa ya kushiriki kazi za kujitolea ili kujiletea maendeleo yao wenyewe na Taifa lao. 

Hayo yamezungumzwa Mjini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu kutoka OR TAMISEMI Bw. Tickson Nzunda wakati wa Mkutano wa Mwaka kwa Wataalam wa Sekta ya Maendeleo ya Jamii na kuwataka washiriki kufanya kazi zao kwa umahiri, kujenga uelewa kwa viongozi wa Halmashauri, kuchochea mabadiliko sehemu za mitaani na vijijini, kuelimisha jamii kubadili mitazamo na fikra, na hivyo kukuza ari ya wananchi kushiriki maendeleo ili kufikia uchumi wa kati na wa viwanda. 
Pamoja na mambo mengine, Naibu Katibu Mkuu amewataka Wataalam wa Maendeleo ya Jamii kuratibu shughuli za Mashirika yasiyo ya Kiserikali kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na taratibu ili kuhakikisha kuwa mashirika hayo yanakuwa na mchango unaokusudiwa katika kufanikisha mipango ya Halmashauri, Mikoa na Taifa ili kuboresha ustawi na maendeleo ya watu.

“Tunatarajia kuwa Mashirika yasiyo ya Kiserikali yangehakikisha kuwa yanasaidia kutoa mchango wa kuwekeza kwenye uwekezaji wa vipaumbele vya kitaifa vilivyoainishwa ikiwemo kuboresha miundo mbinu ya elimu mashuleni ili kuwa na mazingira wezeshi ya kufundishia na kujifunzia, jambo ambalo halifanyiki ipasavyo” alisema Bw. Nzunda.

Naye Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Sihaba Nkinga amefafanua kuwa watumishi wa maendeleo ya jamii ndiyo washawishi na waragibishi wakuu katika kuamsha ari ya wananchi kushiriki mipango ya maendeleo kwa ajili ya mabadiliko ya watu wenyewe.

“Tutambue dhamana tuliyonayo lakini pia umahiri wenu utumike kusaidia watu masikini, wananchi wa vijijini na makundi maalumu katika kuwaongoza kupata haki na fursa sawa” alisema Bibi Sihaba. 

Akizungumza katika mkutano huo Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Nyasa, Protas Sule amesema kuwa wataalamu wa maendeleo ya jamii wanajukumu la kuhimiza wananchi, Mashirika Yasiyo ya Kiserikali kwa kusaidiana na Serikali na jamii kutatua matatizo haya bila kusubiri Serikali kutekeleza kila kitu.

 “Afisa Maendeleo ya Jamii akifanikiwa kubuni mradi utatoa majawabu ya kero za vikundi vya vijana na wanawake atakuwa amefanya kazi kubwa ya kuaminisha jamii kwa Serikali na kuamsha ari yao kufanya kazi za maendeleo” alisema Bw. Sule

Maafisa Maendeleo ya Jamii wanatakiwa kuonesha utumishi uliotukuka katika kuhamashisha na kuamsha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo yao bila kutegemea Serikali kuwafanyia kazi.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NI JESHI LA MAENDELEO YA WATU: NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI NZUNDA
MAAFISA MAENDELEO YA JAMII NI JESHI LA MAENDELEO YA WATU: NAIBU KATIBU MKUU TAMISEMI NZUNDA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiqVSZhPvgRxQCEkoSObzUIPnMatE6LZntHJEubmiahq2kU5XslK_lMhQrZp2RYdm_IB_7UFJhhK_fz1fb_Je7znQjdQa1qkVFW68tphi9b3XV8-68UVDQIjxgInrBHgh2-j-eisoG_dZ8/s640/Picha.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiqVSZhPvgRxQCEkoSObzUIPnMatE6LZntHJEubmiahq2kU5XslK_lMhQrZp2RYdm_IB_7UFJhhK_fz1fb_Je7znQjdQa1qkVFW68tphi9b3XV8-68UVDQIjxgInrBHgh2-j-eisoG_dZ8/s72-c/Picha.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/11/maafisa-maendeleo-ya-jamii-ni-jeshi-la.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/11/maafisa-maendeleo-ya-jamii-ni-jeshi-la.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy