NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AMWAGIZA CHICO KUJENGA KIWANJA CHA NDEGE SHINYANGA.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Elius Kwandikwa, amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya kichina ya CHICO a...


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mheshimiwa Elius Kwandikwa, amemtaka Mkandarasi wa kampuni ya ujenzi ya kichina ya CHICO aliyepewa zabuni ya ujenzi wa kiwanja cha ndege cha Shinyanga kufika eneo la mradi na kuanza ujenzi wa kiwanja hicho haraka iwezekanavyo.
Akizungumza mara baada ya kukagua maendeleo ya kiwanja hicho katika eneo la Ibadakuli leo, mkoani Shinyanga, Naibu Waziri Kwandikwa, amesema kuwa haoni sababu ya mkandarasi huyo kuchelewa kuleta vifaa vyake katika eneo la mradi hadi sasa wakati tayari mkataba wa kuanza kazi hiyo umeshasainiwa.
"Mkandarasi hana sababu ya kuchelewa kuanza kazi wakati fedha zipo na zimeshatengwa kwa ajili ya mradi huu na mkataba umeshasainiwa,  sasa namwagiza mkandarasi huyu kuleta vifaa vyake na kuanza kazi mara moja", amesema Naibu Waziri Kwandikwa.

Aidha, Naibu Waziri huyo amemtaka Meneja wa kiwanja hicho kuhakikisha anatoa ushirikiano na kumsimamia mkandarasi huyo ili kuhakikisha kiwanja hicho kinakamilika mapema nakwa viwango vinavyotakiwa.
"Naamini tukimsimamia vizuri mkandarasi huyu tutapata kiwanja kizuri na imara hapa Shinyanga na tutafungua fursa mbalimbali za kiuchumi katika mkoa huu", amesisitiza Naibu Waziri Kwandikwa.
Kwa upande wake, Meneja wa kiwanja cha ndege cha Shinyanga, Julius Misollow, amemhakikishia Naibu Waziri huyo kutoa ushirikiano kwa mkandarasi huyo atakapowasili eneo la mradi.
Amefafanua kuwa mradi huo unatarajiwa kuhusisha ujenzi wa barabara ya kuruka na kutua ndege, jengo la abiria, maeneo ya maegesho ya ndege na mnara wa kuongozea ndege.

Ameongeza kuwa ujenzi wa kiwanja hicho kwa kiwango cha lami chenye urefu wa kilomita mbili unatarajiwa kugharimu zaidi ya shilingi Bilioni 49.
Katika hatua nyingine Naibu Waziri Kwandikwa, amekagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Mwigumbi - Maswa (KM 50.3), mkoani Simiyu na kumsisitiza mkandarasi anayejenga barabara hiyo kuikamilisha kwa wakati na kwa viwango.

Amesisitiza kuwa kukamilika kwa barabara hiyo ambayo ni kiungo kwa wananchi wa Maswa, Bariadi, Lamadi na Mwanza, kutarahisisha huduma za usafirishaji wa abiria na mizigo katika maeneo hayo.

Naye, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani Simiyu, Mhandisi Albert Kent, amesema kuwa mradi upo katika hatua nzuri na unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili kutoka sasa.
Naibu Waziri Kwandikwa amefanya ziara ya kikazi katika mkoa wa Shinyanga na Simiyu ambapo amekagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na Wizara yake.

(Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elius Kwandikwa, akifafanua jambo kwa Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Josephine Matiro (Wa tatu kushoto), alipofika mkoani humo kukagua  maendeleo ya kiwanja cha ndege cha Shinyanga kilichopo eneo la Ibadakuli.

Muonekano wa Barabara ya Mwigumbi – Maswa (KM 50.3), inayojengwa kwa kiwango cha lami  na mkandarasi CHICO kutoka nchini China. Barabara hii inaunganisha mkoa wa Shinyanga na Simiyu.

Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoani Simiyu, Mhandisi Albert Kent, akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhe. Elius Kwandikwa, kazi za ujenzi zinazoendelea katika barabara ya Mwigumbi – Maswa (KM 50.3).




COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AMWAGIZA CHICO KUJENGA KIWANJA CHA NDEGE SHINYANGA.
NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AMWAGIZA CHICO KUJENGA KIWANJA CHA NDEGE SHINYANGA.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjbQguFiKqkG9md5mXeV9dcJPtCq55tKsuABXY6hrBkbeJb4LMgErfN5s0c5JnxtxAgs2bQYJ7nTRP3QjWnq1cFeWLjRO_BG6nUyJ4j4xBn9OQu8ctz4ygxhbnpKwTzdOwASwNsL9Jcecc/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjbQguFiKqkG9md5mXeV9dcJPtCq55tKsuABXY6hrBkbeJb4LMgErfN5s0c5JnxtxAgs2bQYJ7nTRP3QjWnq1cFeWLjRO_BG6nUyJ4j4xBn9OQu8ctz4ygxhbnpKwTzdOwASwNsL9Jcecc/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/10/naibu-waziri-kwandikwa-amwagiza-chico.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/10/naibu-waziri-kwandikwa-amwagiza-chico.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy