THBUB YALAANI MHE. TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI
HomeJamii

THBUB YALAANI MHE. TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI

- Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli S.L.P 2643, DAR ES SALAAM Simu: +255 22 2135747/8; 213...



-
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora
Kitalu Na. 8, Mtaa wa Luthuli
S.L.P 2643, DAR ES SALAAM
Simu: +255 22 2135747/8; 2137125; 2135222
Faksi: +255 22 2111281
Tovuti: www.chragg.go.tz

Septemba 8, 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Tamko la THBUB KUHUSU MHE. TUNDU LISSU (Mb) KUPIGWA RISASI

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) imesitushwa na kusikitishwa na kitendo cha Mhe. Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika kupigwa risasi, tukio lililotokea Septemba 7, 2017 mjini Dodoma.

Tume inalaani vikali kitendo hicho kwani ni kitendo cha uvunjifu mkubwa wa sheria na haki za binadamu.

Tukio hili ambalo limekuja siku chache tu baada ya tukio la ofisi za wanasheria wa IMMMA zilizoko jijini Dar es Salaam kulipuliwa kwa bomu siyo la kawaida, na limeleta hofu siyo kwa familia ya Mhe. Tundu Lissu pekee, bali kwa wananchi wengi nchini.

Isitoshe, matukio haya hayaleti picha nzuri kwa nchi inayoheshimu demokrasia, haki za binadamu na utawala bora.

Hivyo, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora:
  1. Inalitaka Jeshi la Polisi kuhakikisha linakamilisha haraka upelelezi wa tukio hilo na kuwapeleka wahusika katika vyombo vya sheria.

Tume inaamini kuwa iwapo wahusika wa tukio hili watachukuliwa hatua kali itasaidia kukomesha vitendo vya aina hii vinavyofanywa na makundi ya watu wanaojichukulia sheria mkononi ambayo yanaonekana kujitokeza hivi karibuni.

  1. Aidha, inapenda kukumbusha kuheshimu haki za binadamu na misingi ya utawala bora na kuepuka ukiukwaji wa Katiba na sheria za nchi.

  1. Mwisho, inamtakia Mhe. Tundu Lissu kila la kheri katika matibabu yake ili apone haraka.

Imetolewa na:
(SIGNED)
Mhe. Bahame Tom Nyanduga
Mwenyekiti

TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA

Septemba 8, 2017

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: THBUB YALAANI MHE. TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI
THBUB YALAANI MHE. TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI
https://lh4.googleusercontent.com/oimTf4Hv9wXvGknM0sqcOcbCWaDTsl3Aj_CfCwD8hDDs0TOkWMsrazeilsiDpaiDuo_xMJi-3R75qHip5olmqYz8wlaW45zuLBD-OwpJbtfXdfT6Lr8qfQuKZTQ87Y8uVmn1FAUgedkACRUoqw
https://lh4.googleusercontent.com/oimTf4Hv9wXvGknM0sqcOcbCWaDTsl3Aj_CfCwD8hDDs0TOkWMsrazeilsiDpaiDuo_xMJi-3R75qHip5olmqYz8wlaW45zuLBD-OwpJbtfXdfT6Lr8qfQuKZTQ87Y8uVmn1FAUgedkACRUoqw=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/09/thbub-yalaani-mhe-tundu-lissu-kupigwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/09/thbub-yalaani-mhe-tundu-lissu-kupigwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy