Na Agness Moshi na Bushiri Matenda –MAELEZO. Watanzania na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya nchini wameombwa kuendelea kuisaidia Taasi...
Na Agness Moshi na Bushiri Matenda –MAELEZO.
Watanzania na wadau mbalimbali wa sekta ya Afya nchini
wameombwa kuendelea kuisaidia Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
ili iendelee kufanya kazi kwa ufanisi na kutoa huduma bora.
Hayo yamesemwa na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Mwenyekiti wa Mfuko wa Tulia Trust Mhe. Dkt. Tulia Akson, wakati akikabidhi
msaada runinga nne na katoni mbili za maziwa vyenye thamani ya
shilingi 1,000,000 vilivyotolewa kwa watoto waliopo kwenye Taasisi
hiyo kwa ushirikiano na Dstv, TSN na Kampuni ya Twincity.
Dkt. Tulia amesema msaada wa Luninga unatimiza ahadi
waliohaidi kwa taasisi hiyo na unamaana kubwa sana kwa sababu utawasaidia
watoto wanaokaa hospitalini hapo kwa muda mrefu kujifunza ,na
kuwaburudisha kwa kipindi chote cha matibabu ya awali kabla ya
kufanyiwa upasuaji.
“Watoto hawa wanakaa muda mrefu hospitalini wakitibiwa hivyo
wanashindwa kujumuika na wenzao kwa michezo jambo ambalo linawafanya wahisi
upweke kwa kuwapatia runinga kutawasaidia kuondoa hali hiyo ,
kuwaburudisha na kuwapa nafasi ya kujifunza kupitia vipindi mbalimbali
vinavyorushwa na king’amuzi cha DSTV”, alisema Dkt.Tulia
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa JKCI Profesa Mohammed Janabi amesema kuwa
si watoto tu watakaofaidika kwani hata wazazi wao wataweza kujua mambo
mbalimbali yanayoendelea Nchini kwa kuangalia taarifa za Habari
zitakazokua zinaonyeshwa kupitia chaneli mbalimbali.
“ Sio watoto wote wanaokuja hapa wanatatizo la moyo peke yake
wengine wanakuja wakiwa na magonjwa mengine ambapo inabidi tuanze
kuwatibia kwanza magonjwa hayo ambapo wakati mwingine yanachukua muda mrefu
hivyo basi kwa kipindi chote hicho runinga hizi zitakua zikiwapa
burudani, elimu kwa masomo mbalimbali kama vile kiingereza, hesabu kwa
watoto wakubwa na kwa wale wadogo wataburudika kupitia katuni”,alisema Profes Janabi.
Profesa Janabi ameongeza kuwa msaada wa maziwa waliopewa utasaidia
kuimarisha afya za watoto wadogo wanaotibiwa kwani wapo wengine wamekuja wakiwa
na Afya duni, wengine wana magonjwa ya utapia mlo hivyo kupelekea kuchelewa
kupatiwa matibabu.
Aidha, Profesa Janabi amemshukuru Dkt. Tulia kupitia Mfuko wake wa Tulia
Trust kwa kuendelea kuhamasisha wadau mbalimbali kuipatia misaada Taasisi hiyo.
Kwa upande wake mtoto Mwamvita Hassani mwenye umri wa miaka 13
kutoka wilayani Kondoa kwa niaba ya watoto wanaotibiwa kwenye Taasisi hiyo
ametoa shukrani zake kwa Naibu Spika na wadau waliowapa misaada hiyo.
“Ninawashukuru sana kwakutuletea Tv na Maziwa,Tumefurahi na
tunawaombea watuletee Tv zingine”, alisema Mwamvita.
Profesa Janabi amewaomba wadau mbalimbali kujitokeza
kusaidia upatikanaji wa vitanda kwa ajili ya Taasisi hiyo kwani wanakabiliwa na
changamoto mbalimbali ikiwemo swala la upungufu wa vitanda kwa wagonjwa
kwani wanavitanda 128 tu ambavyo havikidhi mahitaji kutokana na idadi kubwa ya
wagonjwa wanaofika kwa ajili ya matibabu.
![]() | |
|
COMMENTS