RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, ameapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo mbele ya zaidi ya marais 20, wakiwemo wakuu wa serikali, marafiki wa Rwanda k...
RAIS wa Rwanda, Paul Kagame, ameapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo mbele ya zaidi ya marais 20, wakiwemo wakuu wa serikali, marafiki wa Rwanda kutoka kila kona ya dunia na Wanyarwanda wenyewe, huku Tanzania ikiwakilishwa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Benjamin Mkapa.
Sherehe za kuapishwa kiongozi huyo zimefanyika Ijumaa Agosti 18, 2017 kwenye uwanja wa michezo wa Amahoro mjini Kigali.
Kuapishwa kwa Rais Kagame kunafuatia uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni ambapo alipata zaidi ya asilimia 98 ya kura zilizopigwa na hivyo kujipatia imani kubwa kutoka kwa Wanyarwanda.
Katika hotuba yake baada ya kuapishwa, Rais Kagame ambaye yuko madarakani tangu mwaka 1994 baada ya mauaji ya kimbari (halaiki), alisema, Waafrika wasikubali kuchaguliwa mfumo wa utawala wan chi za Magaharibi.Lakni pia aliwashukuru marafiki wa Rwanda kutoka kila pembe ya dunia kwa kusimama pamoja na nchi hiyo na kuiweka Rwanda mioyoni mwao na kufanya bidii katika kuitunza nchi yake ili ipate maendeleo.











Rais Kagame akiwa na mkewe Jannet na watoto wao.
COMMENTS