RC MAKONDA:TUNAITENGENEZA DAR ES SALAAM MPYA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda  na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wakikata utepe leo wakati wa makabidhiano ya  mradi wa Maboresho ya Mtaa wa Samora.
HomeJamii

RC MAKONDA:TUNAITENGENEZA DAR ES SALAAM MPYA

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda  na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema wakikata utepe leo wakati wa makabidhiano...

RAIS DKT MAGUFULI AWAANDALIA FUTARI WANANCHI WA MKOA WA PWANI
JPM -AKEMEA URASIMU NA RUSHWA KWENYE KUTOA VIBALI KWA WAWEKEZAJI
KATIBU MKUU OFISI YA MAKAMU WA RAS AKUTANA NA WATUMISHI WA KITUO CHA DAR ES SALAAM



KOM01
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo akizungumza leo wakati alipokabidhiwa mradi wa Maboresho ya Mtaa wa Samora jijini Dar es salaam  na Shirika la Maendeleo la Serikali ya Japan (JICA)
KOM3
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjemna Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita na Meya wa Ilala, Charles Kwiyeko  wakiongozana wakati wa makabidhiano ya  mradi wa Maboresho ya Mtaa Samora.
………………………………………………………………….
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda leo amekabidhiwa mradi wa Maboresho ya Mtaa Samora jijini Dar es salaam uliogharimu zaidi ya Shilingi Milioni 840 zilizofadhidhiliwa na  Serikali ya Japan kupitia Shirika la Kimataifa la maendeleo Japan (JICA) na Manispaa ya Ilaa uliokamilika kwa 100%.
Mradi huo umehusisha ujenzi wa sehemu za Maegesho, mapumziko ya watu,upandaji wa miti na Maua,maboresho ya mazingira,uwekaji wa alama za barabarani pamoja na maboresho ya mitaa kuanzia Makutano ya Barabara ya Samora na Morogoro ikienda sambamba na kupunguza msongamano.
Akizungumza kwenye makabidhiano hayo Makonda amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema kuhakikisha majengo yote ya Ghorofa eneo la Posta yanafungwa Taa na Luninga za Matangazo ili kupendezesha Mji na kuongeza mwanga nyakati za usiku.
Amesema katika nchi zilizoendelea ikiwemo Marekani majengo marefu yamekuwa sehemu ya matangazo hususani nyakati za usiku na kufanya miji kupendeza hivyo hata Dar es Salaam tunaweza kufanya hivyo ili kufikia azma ya Rais Magufuli kutaka Dar es salaam kuwa mji wa Biashara.
Aidha amesema mradi huo utakuwa wa awamu ili kuhakikisha mitaa na maeneo ya wazi yanaboreshwa ilikuwafanya wananchi kuwa na maeneo mengi ya kupumzika na kubadilishana mawazo ikiwa ni maono yake ya Dar es salaam Mpya.
Awali eneo hilo lililofahamika kama Kaburi Moja lilikuwa likitumika kama Choo, Maegesho holela na wakati mwingine likitumiwa kwa uhalifu na uchafu wa mazingira.
Amewataka wananchi kutunza vizuri eneo hilo ili liweze kuwanufaisha wengi huku akipiga marufuku wamachinga kutofanya biashara kwenye eneo hilo.
Aidha Makonda amesema anataka kuona vituo vyote vya Daladala mkoa wa Dar es Salaam vinaboreshwe kuwa vya kisasa na kuwa sehemu ya matangazo ili kupendezesha mji na kuchangia ongezeko la mapato.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: RC MAKONDA:TUNAITENGENEZA DAR ES SALAAM MPYA
RC MAKONDA:TUNAITENGENEZA DAR ES SALAAM MPYA
http://fullshangweblog.com/home/wp-content/uploads/2017/08/KOM1-2.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/rc-makondatunaitengeneza-dar-es-salaam.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/rc-makondatunaitengeneza-dar-es-salaam.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy