MAKONDA AZIDI KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI KWA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM.
HomeJamii

MAKONDA AZIDI KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI KWA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kupokea Pikipiki za kisasa 10 kwa ajili ya...




Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari katika hafla ya kupokea Pikipiki za kisasa 10 kwa ajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa pikipiki ya TONGBA ya China.


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Paul Makonda akikagua kwa kujaribu kuziendesha Pikipiki hizo za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa pikipiki ya TONGBA ya China.


Muonekano wa pikipiki hizo. (
Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii)


MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amepokea Pikipiki za kisasa 10 kwaajili ya Askari wa Usalama Barabarani zenye thamani ya Shilingi Million 400 kutoka kampuni ya utengenezaji wa Pikipiki ya TONGBA ya China.


Hatua hiyo inakuja baada ya RC Makonda kutafuta kampuni hiyo na kuwasilisha ombi la kupatiwa Pikipiki za kisasa kwaajili ya kuongoza Misafara ya Viongozi, Misiba na kuwahisha Wagonjwa waliozidiwa Hospitalini ambapo kampuni hiyo ilipokea kwa mikono miwili ombi hilo kwa kutoa Pikipiki hizo.


Makonda amesema lengo lake ni kuboresha Mazingira ya utendaji kazi wa Jeshi la Polisi kwa kuhakikisha Askari wanakuwa na vifaa vya kutosha ambapo hadi sasa amefanikiwa kupata Baiskeli 500, Pikipiki za kawaida 200 Computer 100 , Pikipiki za Trafic 10 na kufanya maboresho ya Magari ya Jeshi hilo yaliyokuwa yameharibika.


Aidha Makonda amemuagiza aliekuwa Kaimu Kamanda wa Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam kuwa kamata Askari wote waliobainika kushirikiana na wauzaji wa Dawa za kulevya na wale wanaobambikizia Wananchi kesi kukamatwa ndani ya saa tano.


Agizo hilo limekuja baada ya hivi juzi msamaria mwema kutoa taarifa za uwepo wa muhusika wa dawa za kulevya na Askari walipofika kwenye Hotel wakamkamata na kupewa Rushwa baada ya muda mtuhumiwa akaachiliwa na kurudi kwenye Hotel na kufanya fujo kumtafuta alietoa taarifa na baada ya Makonda kufika na kuangalia Camera za CCTV wakawabaini Askari hao.


Pamoja na hayo amesema wapo Askari waliomkamata Mwananchi akiwa Mpenzi wake kwenye Gari kisha kuwapiga Picha za Utupu na kuwalazimisha watoe kiasi cha Million Tano iliwasisambaze picha hizo kitendo ambacho ni kinyume Sheria ambapo Makonda awezi kuruhusu vitendo hivyo votendeke kwenye Mkoa wake na kueleza kuwa anataka Sheria na Haki vitendeke.


Makonda kubaini uwepo wa Askari wa Uwanja wa Ndege wanaoshirikiana na Raia wa China kusafirisha Kobe na Wanyamapori na Askari wanawabambikia kesi wananchi ikiwemo wale wanaowakamata watu kwenye sehemu za mapumziko.


Amesema hatokubali kuona Askari wachache wanaotumia Magwanda kuwanyanyasa Wananchi na kuchafua taswira ya Jeshi la Polisi na kufanya Wananchi kushindwa kutoa ushirikiano.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKONDA AZIDI KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI KWA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM.
MAKONDA AZIDI KUBORESHA MAZINGIRA YA KAZI KWA JESHI LA POLISI DAR ES SALAAM.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhX9U1MHzw9LVdfAVLRvLMNkq8A3J-uM9lggnTbZoIvxSVvQfK7h_UaGP1pPWC1NXwaEJbF-n1L5Zy4fPYdyIRgB2ZdYQbu-LGxEKj2HV48ZPAbQTDHIMxwn66CORgB2zFUwrVM7FxBbJIQ/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhX9U1MHzw9LVdfAVLRvLMNkq8A3J-uM9lggnTbZoIvxSVvQfK7h_UaGP1pPWC1NXwaEJbF-n1L5Zy4fPYdyIRgB2ZdYQbu-LGxEKj2HV48ZPAbQTDHIMxwn66CORgB2zFUwrVM7FxBbJIQ/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/makonda-azidi-kuboresha-mazingira-ya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/makonda-azidi-kuboresha-mazingira-ya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy