AJALI ZA BARABARANI ZINAWEZA KUPUNGUA KWA MADEREVA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI-KAMANDA MUSLIM
HomeJamii

AJALI ZA BARABARANI ZINAWEZA KUPUNGUA KWA MADEREVA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI-KAMANDA MUSLIM

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii. Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani kimesema kuwa ajali za barabarani zinaweza kupungua kwa maderev...

SERIKALI: MAAFISA HABARI NA MAWASILIANO TUMIENI TOVUTI KUTANGAZA MAENDELEO YA WANANCHI
AMOS CHEREHANI ENDORSES LIBE KUWA RAIS WA JUMUIYA DMV
MAKAMU WA RAIS AKUTANA NA MKURUGENZI MTENDAJI WA BILL MELINDA GATES FOUNDATION


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.


Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani kimesema kuwa ajali za barabarani zinaweza kupungua kwa madereva kufuata sheria za usalama barabarani.


Hayo ameyasema Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim wakati akizindua uwekaji wa namba maalum za simu katika mabasi yaendayo mikoani na nchi jirani leo katika kituo cha Ubungo jijini Dar es Salaam.


Amesema kuwa namba za simu katika mabasi hayo zitatumika kwa abiria kutoa taarifa ya dereva anaendesha bila kufuata sheria za usalama barabarani ikiwemo mwendo kasi.Kamanda Muslim amesema kuwa namba hizo ni bure na kwa abiria, dereva au kondakta atakaeng’oa namba hizo atachukuliwa hatua ikiwemo kunyanganywa leseni.


Amesema uwekaji wa namba maalumu kwenye mabasi unafanyika nchi nzima ikiwa yote nikulinda maisha ya abiria katika kuwa na uhakika wa safari zao.


Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo amesema kuwa watasimamia maagizo ya Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro ambapo yamekaziwa na Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim.


Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Ubungo Ibrahim Samwix amesema kuwa kila siku wanafanya ukaguzi na gari ambayo ina kasoro haiwezi kufanya safari zake.Amesema watahakikisha kuwa kila basi linalondoka katika kituo cha ubungo linakuwa na namba maalum za simu katika kila basi..

Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim akizungumza na waandishi habari katika uzinduzi wa uwekaji wa namba maalum za simu katika mabasi yaendayo Mikoani na Nchi jirani katika kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam. Picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kinondoni, Solomon Mwangamilo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mkazo na maagizo ya Ukaguzi wa magari katika kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Usalama Barabarani Kituo cha Ubungo Ibrahim Samwix (katikati) akizungumza na waandishi habari kuhusu ukaguzi magari yanayotoka kituo Kikuu Cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.



Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la polisi(SACP) Fortunatus Musilim akiweka namba maalmu za simu katika basi itakayotumika kupiga kwa abiria kwa dereva atakaye kiuka sheria za usalama barabani .




Askari wa Usalama barabani wakiwa katika ukaguzi mbalimbali wa mabasi katika kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo.


Muonekano wa Mabasi yakiwa katika kituo Kikuu cha Ubungo leo asubuhi.




Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: AJALI ZA BARABARANI ZINAWEZA KUPUNGUA KWA MADEREVA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI-KAMANDA MUSLIM
AJALI ZA BARABARANI ZINAWEZA KUPUNGUA KWA MADEREVA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI-KAMANDA MUSLIM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhy_lnVI4DBel0RkCCWqB3YI81JtBYao_2fW6OqQraEcsloMNtIZ6Xj40UJS1gWyNu-NjFb-aBjfE2hwhI2r2xjZ_gdg4EQcQmQRBrVbbrurwL3SwfXnjE6IiTcZ5qrRXkmRSkft8HOy9o8/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhy_lnVI4DBel0RkCCWqB3YI81JtBYao_2fW6OqQraEcsloMNtIZ6Xj40UJS1gWyNu-NjFb-aBjfE2hwhI2r2xjZ_gdg4EQcQmQRBrVbbrurwL3SwfXnjE6IiTcZ5qrRXkmRSkft8HOy9o8/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/08/ajali-za-barabarani-zinaweza-kupungua.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/08/ajali-za-barabarani-zinaweza-kupungua.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy