Naibu waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani amesema daraja la Mto Momba lenye urefu wa mita 75 litakaloun...
Naibu
waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani amesema
daraja la Mto Momba lenye urefu wa mita 75 litakalounganisha Mkoa wa
Rukwa na Songwe litaanza kujengwa mapema mwaka huu.
Eng.
Ngonyani ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua barabara ya Kasansa
hadi Kilyamatundu na eneo litakapojengwa daraja la Momba na kusema kuwa
Serikali imeshampata Mkandarasi atakajenga daraja hilo.
“Serikali
imeshatoa kiasi cha sh. Bilioni tatu fedha hizo zimetusaidia kutangaza
zabuni na kumpata mkandarasi, tayari Mkandarasi wa ujenzi huu
ameshapatikana na mkataba wa makubaliano ya ujenzi umeshakamilika hivyo
mkandarasi atausaini rasmi hivi karibuni,” amesema Eng. Ngonyani.
Aidha,
Eng.Ngonyani amemtaka Meneja Wa Wakala wa barabara (TANROADS) Mkoa wa
Rukwa kuhakikisha anatoa ajira kwa wakazi waliopo kata ya Kipeta ambapo
ujenzi wa daraja hilo utafanyika.
Naye
Mbunge wa Jimbo la Kwela Mhe. Ignas Malocha ameishukuru Serikali ya
awamu ya tano ya Mhe. Dkt. John Magufuli kwa kutekeleza ahadi ya ujenzi
wa daraja hilo ambalo kukamilika kwake kutawaletea maendeleo wakazi hao
kwa vile litaufungua Mkoa wa Rukwa na kuunganisha na Songwe na Katavi.
“Kukamilika
kwa ujenzi wa daraja hili kutarahisisha usafirishaji wa mazao ya
biashara kutoka mkoa wetu kwenda mikoa mingine inayopakana na mkoa huu
na kuokoa maisha ya wananchi ambapo awali walikuwa wa wakiliwa na mamba
na wengine kusombwa na maji wakati kuvuka kwenye mto huu,” amesisitiza
Malocha.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akielekea
kukagua sehemu ambapo litajengwa Daraja la Momba litakalounganisha Mkoa
wa Rukwa na Songwe .Kulia ni Meneja wa Wakala wa barabara (TANROADS)Mkoa wa Rukwa Eng. Msuka Mkina na Wa pili kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kwela Mhe. Ignas Malocha.
Meneja wa Wakala wa barabara(TANROADS), Mkoa wa Rukwa Eng.
Msuka Mkina (aliyenyoosha kidole) akimwonesha Naibu Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Wa tatu kulia) eneo
lipakapojengwa Daraja la Momba wakati alipokagua sehemu ambapo
litajengwa Daraja hilo litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe.
Muonekano wa Sehemu ambapo daraja la Mto Momba litakapojengwa. Daraja hilo litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe.
Naibu
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia)
akitoa maelezo kwa wananchi wa kijiji cha Kilyamatundu kata ya Kipeta
Mkoani Rukwa kuhusu ujenzi wa daraja la Mto Momba litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na Songwe.
Wananchi
wa kijiji cha Kilyamatundu kata ya Kipeta Mkoani Rukwa wakifurahi mara
baada ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin
Ngonyani (hayupo picha) kutoa tamko la kupatikana kwa Mkandarasi
atakayejenga daraja la Mto Momba litakalounganisha Mkoa wa Rukwa na
Songwe.
COMMENTS