Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalan...
Mbunge
wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa
mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa
mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji
wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa
na mbunge wa jimbo la kilolo.
Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo
Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya wanawake wa kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo
Mbunge wa jimbo la kilolo Vennance Mwamoto akikabidhi vifaa vya mchezo wa mpira wa miguu kwa wanamichezo wa kijiji cha Bomalang'ombe wakati wa mkutano wa hadhara ulifanyika katika kijiji hicho na kulia ni wachezaji wa timu ya kijiji cha Bomalang'ombe wakipokea jezi na mpira walizopewa na mbunge wa jimbo la kilolo.
Mbunge wa Jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto amegawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na timu za Jimbo hilo kwa lengo la kukuza vipaji vya wanamichezo na kuwandeleza ili wawe wachezaji bora hapo baadae.
Mwamoto
ametekeleza ahadi hiyo katika Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo
hilo la Kilolo katika ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi
wake kwa kuweza kumchagua kwa kura nyingi na kwenda kuwaakilisha
Bungeni.
Akielezea wakati wa kutoa vifaa hivyo vya Michezo, Mwamoto amebainisha kuwa, vifaa hivyo anavitoa ni kutokana na ahadi yake yeye kama Mbunge aliiahidi kwa Vijana hao kuwapatia vifaa hivyo huku baadhi yao pamoja na timu zilimuomba vifaa hivyo ambapo sasa anafanya kutekeleza.
“Niliahidi
kuleta vifaa vya Michezo kwa kila Kata.Lakini pia mimi mwenyewe
niliwaahdi kuwaletea vifaa nan leo hii natimiza ahadi yangu kwenu.”
Alieleza Mwamoto.
Mwamoto
ameongeza kwa kusema ameamua kutoa vifaa hivyo Kwa lengo la kusaidia
Serikali katika juhudi za kuinua michezo lakini pia nisehemu ya Kazi
zake kama Mbunge.
“Mimi
nimecheza mpira kwa mafanikio ndio maana hadi saizi,kwa hilo mimi najua
kuwa michezo ni ajira rasmi hivyo mtu kama unakipaji kitumie kipaji
chako vizuri”. Mwamoto
Amesema
kuwa michezo licha ya kujenga utimamu wa mwili lakini pia ni ajira huku
akitoa mfano Kwa Mbwana Samatta anavyofanikiwa na leo anakipiga Ulaya.
Vifaa hivyo vya michezo ikiwemo seti nzima za Jezi na
mipira ya kuchezea ni hatua ya kuinua na kuendeleza vipaji kwa Vijana
wa Jimbo hilo ambao wamekuwa na shahuku kubwa ya kuibua vipaji vyao vya
mpira wa miguu.
“Leo
nimetoa mipira na jezi hizi kwa timu za Bomalang’ombe na vijiji vya
jirani kwa timu zote za wanaume na wanawake kwa lengo la kuendeleza
vipaji vyenu”alisema Mwamoto
Aidha,
amewataka Vijana hao kuwa na tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara
kwani yatawasaidia kufanya vizuri katika mpira wa miguu na pia mazoezi
ni afya huku kipaji cha mpira wa miguu kikiwa ni ajira kwao pia endapo
michezo itaendelezwa zaidi hasa kwa vijana walio pembezoni.
COMMENTS