Na Daudi Manongi, MAELEZO, DODOMA. Serikali kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imesema kuwa itaendelea kuelimisha jamii na wadau mbalimba...
Na Daudi Manongi,
MAELEZO, DODOMA.
Serikali
kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu imesema
kuwa itaendelea kuelimisha jamii na wadau mbalimbali kuhusu mifumo,maudhui na
taratibu za uridhiaji wa mikataba ili kufanya maandalizi stahiki kabla ya
uridhiaji wa mikataba hiyo.
Hayo yamesemwa
leo Bungeni Mjini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na
Ajira Mhe. Anthony Mavunde wakati akijibu Swali la Mhe.Ussi Pondeza Mbunge wa
Chambani.
“Nchi yetu
inazo sheria mbalimbali zinazotambua na kusimamia maslahi ya wafanyakazi nchini
wakiwemo wafanyakazi wa majumbani,wafanyakazi wa mahotelini na vyama vyao”,Aliongeza
Mhe. Mavunde.
Aidha Waziri
Mavunde amewataka wafanyakazi nchini kutambua juhudi za Serikali za kulinda na
kutetea haki na maslahi ya wafanyakazi
kupitia sheria,kanuni na taratibu zilizopo nchini.
Amesema Serikali
inaendelea kupitia kwa makini azimio lililofikiwa na Shirika la kazi la Umoja
wa Mataifa mwaka 2011 linaotaka kila nchi mwanachama wa ILO kuwa na Sheria ya
kuwalinda wafanyakazi wa Mahotelini na Majumbani.
“Ni kweli kuwa
Mwaka 2011, Nchi wanachama wa Shirika la Kazi Duniani ikiwemo Tanzania
zilipitisha mkataba wa kimataifa kuhusu kazi za Staha kwa wafanyakazi wa
Majumbani,ambapo hadi sasa nchi zilizoridhia ni 23 kati ya nchi 189 na kwa
upande wa Afrika zimelizia nchi mbili tu kwa iyo bado tunaendelea kuupitia ili
kufanya maandalizi ya kuridhia”,Aliongeza Mhe.Mavunde.
Pamoja na hayo
Waziri Mavunde amesisitiza kuwa Tanzania Bara ina sheria zake za kazi ambazo
zinawahusu wafanyakazi wote ikiwemo
wafanyakazi wa mahotelini na majumbani ambazo zinalinda haki zao.
COMMENTS