MKUU wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Miraji J. Mtaturu awafuturisha waislamu wa Wilaya hiyo huku akiwasihi kuendeleza tabia njem...
MKUU
wa Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida Miraji J. Mtaturu awafuturisha
waislamu wa Wilaya hiyo huku akiwasihi kuendeleza tabia njema kwa
kufuata misingi iliyohifadhiwa na Allah katika kitabu chake cha (Quran)
hata baada ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan kumalizika.
Akizungumza
na Waislamu hao baada ya kupata futuru Wilayani humo Mhe Mtaturu
alisema kuwa katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan watu wametenda mema
yanayopaswa kuendelezwa hata baada ya mwezi huo.
"Wakati
tupo kwenye mfungo huu tupo kwenye darasa la tabia njema hivyo
nawashauri hata baada ya mfungo huu tuyaendeleze," alisema Mtaturu.
Alisema
kuwa serikali inafarijika pale inapoona wananchi wake wakifuata imani
za dini zao na hivyo kuwa raia wema na nchi kuendelea kuwa na amani.
"Tunamaliza
kukamilisha moja ya nguzo tano za uislamu panapo majaaliwa ya Mwenyezi
Mungu, hivyo nawaombeni Ndugu zangu Waislamu hapa Wilayani Ikungi na
Duniani kwa ujumla isiwe mwisho wa kufanya mema bali iwe ni mwendelezo
wa kutenda haki, kudumisha amani na mshikamano katika siku zetu zote za
maisha yetu," alisisitiza Mtaturu.
Mhe Mtaturu
aliwatakia maandalizi mema ya sikukuu ya Eid El Fitri huku akiwaasa
kusherehekea kwa amani, utulivu na upendo na kukumbuka kutoa Zaka kwa
watu wasio na uwezo.
Alitumia nafasi hiyo kuwaomba
wananchi kumuombea Rais Dokta John Magufuli kutokana na kazi kubwa
anayoifanya katika kuendeleza dhamira yake ya kulinda rasilimali za
nchi ili ziwanufaishe watanzania wote hasa wale wanyonge na wasiojiweza.
Kwa
upande wake Sheikh wa Wilaya hiyo Abdi Seleman akitoa neno la shukrani
alimshukuru mkuu wa wilaya hiyo kwa kuwafuturisha na kusema kuwa hiyo ni
mara ya kwanza toka wilaya hiyo ianzishwe kwa mkuu wa wilaya kuwaalika
futari hivyo Mkuu huyo ameonyesha kuwajali watu anawaongoza.
"Kwa
sadaka yako hii kwetu tunamuomba Mwenyezi Mungu akulipe kila la
kheri,na inshallah huu usiwe mwisho bali uwe mwanzo wa kufanya hivi,"
alisema Sheikh Seleman.
Nae Kadhi wa mkoa wa Singida
Ramadhan Kaoja alimshukuru mkuu wa wilaya hiyo na kusema hiyo ni dalili
za kiongozi bora kwa kuwa karibu na jamii lakini pia ni sehemu ya
kukamilisha imani yake ambapo kwa mwezi huu wa Ramadhan kwa kufuturisha
anapata thawabu nyingi sana.
Imetolewa Na;
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya IkungiMkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akihutubia mamia ya
wakazi wa Wilaya hiyo waliojitokeza wakati wa futari katika Ukumbi was
Shule ya Sekondari Ikungi.
Kadhi
wa mkoa wa Singida Ramadhan Shekh Kaoja akitoa neno la Shukrani kwa
niaba ya waumini wote waliojitokeza kwenye ibada ya futari iliyoandaliwa
na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. Mtaturu
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akihutubia mamia ya
wakazi wa Wilaya hiyo waliojitokeza wakati wa futari katika Ukumbi was
Shule ya Sekondari Ikungi
Mkuu
wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Kushoto) Akimshukuru
mwenyekiti wa CCM wilaya Ndg Hassan Tati kwa kuhudhuria hafla ya futari
katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu (Kushoto) Akimshukuru Kadhi wa mkoa wa Singida Shekh Ramadhan Kaoja kwa kuhudhuria hafla ya futari katika Ukumbi wa Shule ya Sekondari Ikungi
Waumini
wakimpa mkono Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. Mtaturu mara baada
ya hafla ya futari aliyowaandalia katika ukumbi wa shule ya Sekondari
Ikungi kukamilika.
Waumini
wakimsikiliza kwa making Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji J. Mtaturu
mara baada ya hafla ya futari aliyowaandalia katika ukumbi wa shule ya
Sekondari Ikungi kukamilika.

Sekondari Ikungi kukamilika

Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya IkungiMkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe Miraji Jumanne Mtaturu akihutubia mamia ya wakazi wa Wilaya hiyo waliojitokeza wakati wa futari katika Ukumbi was Shule ya Sekondari Ikungi.

COMMENTS