Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga (Mb.) (katikati), akipokea funguo za Magari ...
|
Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine
Mahiga (Mb.) (katikati), akipokea funguo za Magari aina ya Toyota Land
Cruiser kutoka kwa Balozi wa Omani hapa nchini, Mhe. Ali Abdullah Al
Mahruqi. Anayeshuhudia makabidhiano hayo ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Balozi Ramadhan
Mwinyi.
Makabidhiano
hayo yalifanyika kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius
Nyerere jijini Dar Es Salaam leo. Baada ya kukabidhiwa magari hayo yenye
thamani ya takriban milioni 400 za Tanzania, Waziri Mahiga alisema kuwa
msaada huo umetolewa na Serikali ya Oman kwa ajili ya kusaidia masuala
ya usafiri katika kipindi hiki cha mpito ambapo Serikali inahamia
Dodoma.
|
|
Waziri Mahiga akitoa neno la shukrani kwa niaba ya Serikali na Wizara yake kwa ujumla mara baada ya kupokea msaada huo.
|
|
Waziri akiendelea kuongea huku Watumishi wa Wizara yake wakimsikiliza kwa makini.
|
|
Balozi
Al Mahruqi naye akizungumza na kuishukuru Tanzania kwa ushirikiano
anaoumpata kwenye utendaji kazi wake hapa nchini. Alisema Serikali yake
itaendelea kuisaidia Tanzania katika masuala mbalimbali ikiwemo huduma
za kijamii.
|
COMMENTS