Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Dk. Charles J. Tizeba (MB) amezindua Mwongozo na Wasifu wa Kilimo Kinachohimili Mabadiliko ya T...
Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Mhandisi Dk. Charles J.
Tizeba (MB) amezindua Mwongozo na Wasifu wa Kilimo Kinachohimili
Mabadiliko ya Tabianchi. Tukio hilo limefanyika katika ukumbi wa Wizara
katika makao makuu mjini Dodoma.
Uzinduzi huo umefanyika wakiwepo washiriki na wadau
mbalimbali wa maendeleo ikiongozwa na DK. Fred Kafeero, Mwakilishi Mkazi
wa FAO, Dk. Sebastian Grey, Mwakilishi wa CIAT.
Wengine waliokuwepo ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Kilimo Maji na Mazingira, Mheshimiwa Dk. Mary Nagu (MB), na
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii,
Mheshimiwa Atashasta Nditiye (MB).
Washiriki wengine walikuwa ni wadau wa kilimo hapa nchini
kama vile taasisi zisizo za kiserikali, sekta binafsi ambazo
wanashirikiana na serikali katika maendeleo ya kilimo hususan
kinachohimili mabadiliko ya tabianchi.

COMMENTS