TRA YAMZUNGUMZIA MSANII DIAMOND KUHUSU KODI: NI WAKATI WA SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI DAR
HomeJamii

TRA YAMZUNGUMZIA MSANII DIAMOND KUHUSU KODI: NI WAKATI WA SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI DAR

 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo (katikati), akitoa hotuba ya...

JARIDA LA WIZARA YA NISHATI NA MADINI TOLEO LA 168
IDARA YA HABARI YAFANYA MAHOJIANO NA MAKAMU WA RAIS
RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NCHINI TUCTA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

 Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo (katikati), akitoa hotuba ya ufunguzi wa  semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam leo Mei 13, 2017. Kulia ni Mwenyekiti wa semina hiyo, Bi. Angella Msangi na kushoto ni Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Mwangosi
 Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi





NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MKURUGENZI wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Bw. Richard Kayombo, ameendelea kukanusha kwamba, Mamlaka hiyo haijamkadiria msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnamuz kulipa kodi ya shilingi Milioni 400.
Hayo ameyasema leo Mei 13, 2017 wakati akifafanua hoja mbalimbali kwa waandishi wa habari wanaoshiriki semina ya siku moja iliyoandaliwa na TRA ili kutoa elimu ya ulipajin kodi kwa waaandishi na kufanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), jijini Dar es Salaam.
“Tuko kwenye hatua za awali za mazungumzo bado hatujakadiria kodi amnayopaswa kulipa Diamond, na kwa bahatio nzuri tumekaa naye na bado tuko kwenye mazungumzo na sio kweli kwamba tumemkadiria shilingi Milioni 400,” Alisema na kuongeza
“Tunajaribu kujua vyanzo vyake vya mapato, lakini hata kama imetokea mtu umekadiriwa kulipa kodi kwa kiasi Fulani na hujaridhika unayo nafasi ya kukata rufaa kwa Kamishna Mkuu wa TRA, na ndapo hujaridhika na rufaa hiyo ipo Mamlaka nhyingine ambayo iko nje ya TRA, Tax Tribunal, na bodi ya Rufaa za kodi.” Alifafanua Bw.Kayombo.
“Hivyo mtu asiwe mnyonge anayo nafasi ya kukata rufaa, tatu ndani ya TRA, na mbili nje ya TRA ikiwa ni pamoja na Mahakamani, kwa hivyo watu wasiogope. Alisema. Awali akifungua semina hiyo.
Bw. Kayombo aliwaasa waandishi wa habari kujenga uzalendo kwa kuunga mkono juhudi za Mamlaka ya Mapato Tanania TRA, katika kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi.
Hayo yamesemwa leo Mei 13, 2017 na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi kutoka TRA, Bw. Richard Kayombo(pichani juu), wakati wa ufunguziwa semina ya siku moja ya ujasiriamali na elimu ya kulipa kodi kwa waandishi wa habari kwenye ukumbin wa Benki Kuu ya Tanzania jijini Dar es Salaam.
“Najua kihistoria linapokuja swala la kulipa kodi huwa kuna changamoto nyingi watu kuelewa swala hili, lakini napenda niwaeleze ndugu zangu, ili kuiwezesha serikali kutoa huduma stahiki kwa wananchi ni lazima watu walipe kodi, hivyo waandishi wa habari mnao wajibu mkubwa kutumia taaluma yenu kuelimisha umma umuhimu wa kulipa kodi, Alisema Bw. Kayombo.
Bwana Kayombo amesema, TRA kwa niaba ya serikali ya ndiyo chom,bo chenye mamlaka ya kukusanya kodi za serikali katika kutoka kwa watu binafsi, makampuni na taasisi za umma.
“Huduma za usafiri, elimu, afya na miundombinu itakuwa bora tu endapo wananchi watatimiza wajibu wao wa kulipa kodi.” Alisema na kuongeza katika semina hii waandishi wa habari watapata fursa ya kujifunza mambo mbalimbali yahusuyo kodi ikiwemo kodi ya majengo kutoka kwa watalamu wa kodi wa TRA.


  Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi
  Waandishi wa habari wakifuatilia hotuba ya ufunguzi


 Waandishi wa habari wakifuatilia
 Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TRA, Bi. Rachael Mkundai, (kulia), akiwakaribisha waandioshi wa habatri kwenye semina. Kushoto ni Mwenyekiti wa semina, Bi. Angella Msangi


Bw. Sydney Mkamba, Afisa Kodi Mkuu
Afisa Kodi Mkuu wa TRA, Bw.

 Bw. Emmanuel Herman, kutoka Mwananchi
 Mwenyekiti wa semina akifuatilia
 Bw. Obeid Mwangasa
 Othman Michuzi (kushoto) wa Mtaa kwa Mtaa Blog na Mushi wa The Habari.com
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TRA YAMZUNGUMZIA MSANII DIAMOND KUHUSU KODI: NI WAKATI WA SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI DAR
TRA YAMZUNGUMZIA MSANII DIAMOND KUHUSU KODI: NI WAKATI WA SEMINA YA WAANDISHI WA HABARI DAR
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjZvnmXKzXJzezW3y3MCtQUmTQyiclX9lUdl-necQryBF9sZ57fZiWWXsuuBw82AMCFVdaSSaF-Jwb_5IavnKC5dXX9f1R5yN-qpxGY5EIKNOuLEBFp1qeT1GMduTBtPrYHg5czeZlKwYw/s640/Richard+Kayombo.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjZvnmXKzXJzezW3y3MCtQUmTQyiclX9lUdl-necQryBF9sZ57fZiWWXsuuBw82AMCFVdaSSaF-Jwb_5IavnKC5dXX9f1R5yN-qpxGY5EIKNOuLEBFp1qeT1GMduTBtPrYHg5czeZlKwYw/s72-c/Richard+Kayombo.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/05/tra-yamzungumzia-msanii-diamond-kuhusu.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/05/tra-yamzungumzia-msanii-diamond-kuhusu.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy