Mshauri wa Taasisi ya Mama’s & Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR) Balozi Patrick Chokala akizun...
Mshauri
wa Taasisi ya Mama’s & Papa’s For Community Reform Rehabilitation
Center (MPFCR) Balozi Patrick Chokala akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu utoaji wa TUZO kwa baadhi ya watu wenyemkachango katika jamii
leo Jijini Dar es Salaam. Tuzo hizo zitatolewa tarehe 12 mwezi huu.
Watakaopewa tuzo hizo ni Dkt. Reginald Mengi, Mchungaji Dkt. Getrude
Rwakatale, Mhe. Agustino Lyatonga Mrema, Mustafa Sabodo, na Mohamed
Gulam Dewji. Kulia ni Mjumbe wa Taasisi hiyo Omary Kombe.
Msanii
wa muziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni Balozi wa Taasisi ya Mama’s
& Papa’s For Community Reform Rehabilitation Center (MPFCR), Nurdin
Bilal maarufu kama Shetta (baba Kaira) akielezea jambo mbele ya
waandishi wa habari kuhusu yeye kuwa Balozi wa Taasisi hiyo kwa lengo la
kuunga mkono jitihada za kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya leo
Jijini Dar es Salaam.Taasisi hiyo pia imetoa Tuzo za heshima kwa baadhi
ya watu wenye mchango katika jamii. Kutoka kulia ni Mshauri wa Taasisi
hiyo Balozi Patrick Chokala na Mkurugenzi wa Taasisi hiyo Bibi. Emmi
Ally Ghahae.

Baadhi
ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wao na wawakilishi wa
Taasisi ya Mama’s & Papa’s For Community Reform Rehabilitation
Center (MPFCR) leo jijini Dar es Salaam. Taasisi hiyo inatarajia kutoa
Tuzo za heshima kwa baadhi ya wadau wanajali na kuthamini
jamii.Watakaopewa tuzo hizo ni Dkt. Reginald Mengi, Mchungaji Dkt.
Getrude Rwakatale, Mhe. Agustino Lyatonga Mrema, Mustafa Sabodo, na
Mohamed Gulam Dewji.
COMMENTS