Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umefikia tamati leo Ikulu Jijini Dar es Salaa. Mkatano huu ul...
Mkutano
wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
umefikia tamati leo Ikulu Jijini Dar es Salaa. Mkatano huu ulikuwa na
ujumbe na uwakilishi kutoka nchi zote sita zinazounda Jumuiya ya Afrika
Mashariki. .
Rais
Mhe. Dkt. Magufuli akizungumza katika Mkutano huu wakati wa kukabidhi
kiti cha Uwenyekiti amesema katika kipindi cha miaka miwili ya
Uwenyekiti wa Tanzania, Jumuiya ya Afrika Mashariki imepata mafanikio
makubwa na kuifanya istawi zaidi katika maeneo mbalimbali ikiwemo
biashara kutokana na kupunguzwa kwa vikwazo vya biashara visivyokuwa vya
kiforodha, kuboreka kwa mfumo wa elimu ya Juu ndani ya Jumuiya na
kuongezeka kwa Sudan Kusini katika Jumuiya.
Aidha
mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Mhe. Museveni
akiongea mara baada ya kukabidhiwa nafasi hiyo amesema kunakila sababu
ya kulinda na kudumisha Mtangamano kwa kuwa unaharakisha kasi ya
maendeleo ya nchi wanachama na watu wake, unaimarisha ulinzi na usalama
wa nchi wanachama, na kudumisha undugu wa kihistoria uliodumu kwa muda
mrefu miongoni mwa nchi wanachama.
Pia
Mkutano huu wa 18 wa Wakuu wa nchi umeshuhudia viapo vya viongozi wapya
wawili katika ngazi ya Jumuiya ambao ni Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki kutoka Sudan Kusini, Jaji Charles Oyo Nyawezo na Naibu
Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Jumuiya ya Afrika Mashariki Eng. Steven
Mrote kutoka Tanzania. Katika Kutano huu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekabidhi rasmi uwenyekiti kwa
Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Museveni.
Rais
wa Jumhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akihutubia hadhira iliyohudhuria Mkutano wa 18 wa Kawaida wa Wakuu wa
Nchi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika Ikulu Jijini Dar es
Salaa.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akisaini moja ya nyaraka ya makabidhiano ya uwenyekiti wakati wa Mkutano
wa 18 wa Kaiwa wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Afrika Mshariki.

Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt.
Augustine Mahiga (wakwanza kulia) akifuatilia Mkutano. Wengine ni Waziri
wa Fedha na Mipango Mhe.Dkt. Philip Mpango (katika) na Waziri wa Elimu,
Sayansi,Teknolojia na Ufundi Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (kushoto).
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Aziz P. Mlima (kulia) akifuatilia Mkutano
Rais
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Jaji Charles Oyo Nyawezo
kutoka Sudan Kusini kwa kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Jumuiya ya
Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo. 

Rais
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Eng.Steven Mrote kutoka
Tanzania kwa kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Sekretariat ya Jumuiya
ya Afrika Mashariki mara baada ya kula kiapo.
Rais
Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza mwanafunzi wa kitado cha nne
aliyejishindia nafasi ya nne katika mashindano ya uandishi wa insha ya
Jumuiya ya Afrika Mashariki kutoka Shule ya Sekondari Kibaha, Tanzania
Bw.Joseph Mbogo
Waziri Mhe. Mahiga akifuatilia Mkutano
Picha ya pamoja
COMMENTS