Katibu Mkuu wa CUF, na Makamu wa Kwanza wa Rais wa zamani wa Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad leo Mei 6, 2017, amemtembelea W...
Katibu
Mkuu wa CUF, na Makamu wa Kwanza wa Rais
wa zamani wa Zanzibar, Maalim Seif
Sharrif Hamad leo Mei 6, 2017, amemtembelea Waziri Mkuu wa zamani, na mjumbe wa
Kamati Kuu ya CHADEMA, Mhe. Edward Lowassa akiwa ofisini kwake, (oval), Mikocheni
jijini Dar es Salaam ambako wamejadiliana masuala mbali ya siasa na zaidi
mgogoro ndani ya CUF. Kwa mujibu wa taaifa za asaidizi wa Mhe. Lowassa,
mazungumzo hayo yalijikitazaidi katika kuimarisha umoja na mshikamano miongoni
mwa vyama vya upinzani, vinavyounda vuguvugu la Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA). Maalim Seifyuko jijini Dar es Salaam kwa ziara ambayo sio rasmi lakini
inalengo la kuwatembelea wanachama wa CUF, pamoja na viongozi mbalimbali wa
kisiasa.
COMMENTS