Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akizungumza na Gavana wa Lubumbashi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia y...
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa amewataka
watumishi wa Wizara hiyo Sekta ya Uchukuzi kutumia vizuri fursa ya
kuhamia Dodoma kwa kuwatumikia watanzania kwa uadilifu na weledi.
Amesema
hayo jijini Dar es Salaam wakati akiwaaga watumishi wa Sekta ya
uchukuzi wa awamu ya kwanza ambao wameondoka leo kuelekea mjini Dodoma.
“Nawapongeza
kwa kupata fursa ya kuwa katika awamu ya kwanza katika Wizara hii
kuhamia Dodoma fahamuni hii ni fursa na si changamoto kwani hatua hii
inasogeza huduma karibu na wananchi hivyo watumikieni kwa moyo”, amesema
Prof. Mbarawa.
Prof.
Mbarawa amesema kuwa nia ya Serikali ni kuhakikisha watumishi wake
wanahamia Dodoma na kuendelea na utekelezaji wa majukumu yake kwa
wananchi.
“Watumishi
wa Sekta ya Uchukuzi wanaohamia Dodoma katika awamu ya kwanza ni pamoja
na Katibu Mkuu Sekta ya Uchukuzi, Wakurugenzi na Wakurugenzi wasaidizi,
wakuu wa vitengo na maafisa waandamizi”, amesisitiza Dkt. Chamuriho.
Waziri
wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza
na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Sekta ya Uchukuzi), Dkt. Leornard
Chamuriho kabla ya kuwaaga watumishi wa Wizara hiyo wanaohamia Dodoma leo, jijini Dar es salaam. (Picha na Biseko Ibrahim).
COMMENTS