MAKAMU WA RAIS DK BILAL AZINDUA RASMI BENKI YA MAENDELEO PLC, JIJINI DAR LEO Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal, ak...
MAKAMU WA RAIS DK BILAL AZINDUA RASMI BENKI YA MAENDELEO PLC, JIJINI DAR LEO
Makamu
wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi cheti, Msaidizi wa Askofu wa Dayosis ya Mashariki na Pwani ya KKKT Mchungaji George Fupe, ambaye ni mmoja kati ya
waanzilishi wa benki hiyo na wahamasishaji kwa watu kununua hisa katika
benki hiyo. Kulia ni Askofu Mkuu wa
Kanisa la KKKT, Dk Alex Malasusa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki.
Makamu
wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi cheti, Afisa Utawala wa Benki ya Maendeleo, Rose Mushi,
ambaye ni mmoja kati ya waanzilishi wa benki hiyo na wahamasishaji kwa
watu kununua hisa katika benki hiyo, ambapo walifanikiwa kupata jumla
ya shilingi Bilioni 4.5. Makamu alikabidhi vyeti hivyo wakati wa hafla ya
uzinduzi rasmi wa benki hiyo iliyopo jijini Dar es Salaa. Wa pili (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha, Janet Mbene, Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT, Dk Alex Malasusa (kulia).
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal,
akifunua kitambaa kuashiria kuweka Jiwe la Msingi katika benki ya
Maendeleo PLC, wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo,
iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la
KKKT, Dk Alex Malasusa (kushoto) ni Naibu Waziri wa Fedha, Janet
Mbene.
Makamu
wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal,
akikata utepe kuashiria kufungua benki ya Maendeleo PLC, wakati wa
hafla ya uzinduzi rasmi wa benki hiyo, iliyofanyika leo jijini Dar es
Salaam. Kulia ni Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Alex Malasusa, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck Sadiki (kushoto) Naibu
Waziri wa Fedha, Janet Mbene (mwenye miwani).
Makamu
wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal,
akimkabidhi mfano wa kadi ya ATM, mteja wa kwanza kufungua Account
katika benki hiyo, Elianasa Marco Njiu, mkazi wa jijini Dar es Salaam,
wakati wa hafla ya ufunguzi wa Benki hiyo iliyofanyika jijini Dar es
Salaam, Novemba 12, 2013. Wa pili (kulia) ni Mteja wa kwanza kupata
mkopo katika benki hiyo, Margareth Chiwata.
Makamu
wa Rais wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal,
akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa bemki hiyo, leo.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa benki hiyo.
Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria hafla hiyo ya ufunguzi wa benki hiyo.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo na
wachungaji wa Kanisa la KKKT, baada ya ufunguzi rasmi wa benki hiyo.
Watazamaji 300 tu wataruhusiwa kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 5,000.
Taifa
Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager imeingia kambini leo
(Novemba 12 mwaka huu). Miongoni mwa wachezaji wanaotarajia kuripoti ni
kipa Ivo Mapunda wa Gor Mahia.
BODI YA LIGI KUU YAFUNGIA VIWANJA SABA
Bodi
ya Ligi Kuu Tanzania (TPL Board) imefungia viwanja saba vilivyokuwa
vikitumiwa na timu za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) na Ligi Daraja la Kwanza
(FDL) hadi vitakapofanyiwa marekebisho ili kukidhi mahitaji ya mechi za
mpira wa miguu.
Uamuzi
huo umefikiwa na TPL Board katika kikao chake cha kwanza kilichofanyika
juzi (Novemba 10 mwaka huu) jijini Dar es Salaam ambapo pamoja na mambo
mengine kilipitia ripoti za mechi za VPL na FDL katika mzunguko wa
kwanza.
Viwanja
vilivyofungiwa na marekebisho yanayotakiwa kufanyika kwanza ili
viruhusiwe kutumika tena ni Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba (majukwaa
yake yamechakaa, hivyo kuhatarisha usalama wa watazamaji), na Uwanja wa
CCM Mkwakwani jijini Tanga (vyumba vya wachezaji kubadilishia nguo
(dressing rooms) havina hadhi).
Uwanja
wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya (sehemu ya kuchezea- pitch ni
mbovu), Uwanja wa Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha
(pitch ni mbovu), Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi (vyumba vya kubadilishia
kutumika kwa ajili ya shule ya awali), Uwanja wa Majimaji mjini Songea
(pitch ni mbovu) na Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro (pitch ni mbovu).
Klabu
ambazo timu zake zinatumia viwanja hivyo zimeshaarifiwa rasmi juu ya
uamuzi huo ambapo ama vinatakiwa kuwasiliana na wamiliki wa viwanja
hivyo ili wafanye marekebisho au kutafuta viwanja vingine vya kuchezea
mechi zao.
Kwa
upande wa ripoti za mechi za VPL; Mbeya City imepigwa faini ya sh.
500,000 na kupewa onyo kali kwa timu yake ya U20 kutocheza mechi ya
utangulizi walipocheza na Yanga. Pia wanatakiwa kulipa gharama za
uharibifu baada ya washabiki wao kuvunja kioo cha basi la Yanga baada ya
gharama hizo kuthibitishwa na Bodi ya Ligi.
Pia
Mbeya City imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa washabiki wake kushambulia
basi la wachezaji wa Tanzania Prisons baada ya mechi dhidi yao, na
kulipa gharama za uharibifu baada ya kuthibitisha na Bodi ya Ligi.
Coastal
Union imepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki
wake ilipocheza na Azam kwenye Uwanja wa Mkwakwani ambapo mwamuzi
msaidizi Hassan Zani alishambuliwa kwa mawe na kujeruhiwa mkononi na
kichwa, tukio lililosababisha mchezo kusimama kwa dakika tatu.
Beki
wa Coastal Union, Hamad Khamis wa Coastal Union amepigwa faini ya sh.
500,000 kwa kumpiga kichwa kwa makusudi Kipre Tchetche wa Azam. Kitendo
hicho kilisababisha refa amtoe nje kwa kadi nyekundu, hivyo atakosa
mechi tatu zinazofuata za timu yake.
Mchezaji
Cosmas Lewis wa Ruvu Shooting alifanya kitendo cha utovu wa nidhamu kwa
kupiga kelele wakati mgeni rasmi akisalimia timu na kukataa kupeana
mkono na kamishna kwenye mechi dhidi ya Rhino Rangers, hivyo amefungiwa
mechi tatu na kupigwa faini ya sh. 500,000.
Mtunza
vifaa (Kit Man) wa JKT Ruvu, Selemani Oga aliondolewa kwenye benchi la
ufundi wakati wa mechi yao dhidi ya Mbeya City kwa kosa la kutoa lugha
chafu kwa refa, hivyo suala lake litapelekwa katika Kamati ya Maadili.
Kocha
Msaidizi wa Oljoro JKT, Fikiri Elias amepigwa faini ya sh. 500,000 na
kufungiwa mechi tatu kwa kumshambulia kwa matusi refa wakati wa mechi
yao dhidi ya Ashanti United. Naye mtunza vifaa wa timu hiyo Elas Justin
amepelekwa Kamati ya Maadili kwa kumshambulia refa kwa matusi ya nguoni.
Simba wamepigwa faini ya sh. 500,000 kutokana na vurugu za washabiki wake wakati wa mechi dhidi ya Kagera Sugar.
Katika
FDL, mchezaji Ally Mtoni wa Villa Squad amepigwa faini y ash. 200,000
na kufungiwa mechi tano. Kosa lake ni kujisaidia haja ndogo golini wakti
wa mechi dhidi ya Ndanda FC iliyochezwa mjini Mtwara.
Kamishna
Paul Opiyo wa mechi ya FDL kati ya Villa Squad na Transit Camp kwa
kutokuwa makini. Katika ripoti yake ameeleza kuwa Transit Camp
ilichelewa kufika uwanjani, lakini hakusema ilichelewa kwa muda gani.
Kocha
wa Polisi Dar es Salaam, Ngelo Nyanjabha na Meneja wa timu hiyo Mrimi
Masi wamepigwa faini ya sh. 200,000 na kufungiwa mechi tatu kila mmoja
kwa kuongoza kundi la washabiki kumvamia refa wa mechi yao dhidi ya
Villa Squad iliyochezwa Dar es Salaam.
Pia
Bodi ya Ligi imeagiza Polisi waandikiwe barua ya onyo kwa vile wakati
waamuzi wanapigwa walikuwepo lakini hawakutoa msaada kwa wakati.
Kocha
wa Friends Rangers, Kheri Mzozo amepigwa faini ya sh. 200,000 na
kufungiwa mechi sita kwa kosa la kumtukana refa na kutishia kuhamamisha
washabiki waingie uwanjani kufanya fujo kwenye mechi dhidi ya Villa
Squad.
Naye
Kocha msaidizi wa timu ya Transit Camp, Haji Amiri amepigwa faini ya
sh. 200,000 na kufungiwa mechi sita kwa kutoa lugha ya matusi kwa
mwamuzi wa akida wakati wa mechi dhidi ya Friends Rangers.
Adhabu
zote zimetolewa kwa mujibu wa kanuni. Pia Bodi ya Ligi imeahirisha
kufanya uamuzi wa mechi kati ya Stand United na Kanembwa JKT iliyochezwa
Uwanja wa Kambarage ili kukusanya taarifa zaidi. Mechi hiyo
haikumalizika. Bodi ya Ligi itakutana tena Jumapili (Novemba 17 mwaka
huu).
COMMENTS