WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameyataka mashirika na taasisi za umma yaangalie utendaji wa Serikali ya awamu ya tano katika kipindi cha mwaka mmoja na yatoe ushauri wa namna bora ya kuboresha maendeleo nchini.
Ametoa kauli hiyo leo asubuhi (Jumanne, Februari 28, 2017) wakati akifungua Mkutano wa kujadili Nafasi ya Mashirika ya Umma katika Utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano Ikulu jijini Dar es Salaam.
Akifungua mkutano huo wa siku moja kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri Mkuu amesema ana imani kuwa washiriki wa mkutano huo wataangalia uzoefu ambao Serikali imeupata katika mwaka mmoja tangu iingie madarakani na kushauri namna bora ya kukabiliana ba vikwazo ambavyo vimejitokeza.
“Ninaamini mtaangalia uzoefu tulioupata kwa mwaka mmoja uliopita ambao Serikali hii imekuwa madarakani, mtaangalia ni mpango upi tuliopanga na upi umefanikiwa ama upi umekwama na nini kilisababisha vikwazo hivyo vitokee,” amesema.
Alisema matarajio ya Serikali kutokana na mkutano huo ni kwamba washiriki wa wataainisha namna mashirika ya umma yatakavyoweza kuchangia katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Maendeleo hususan katika kujenga uchumi wa viwanda.
“Ninaamini mtaweka wazi hatua za haraka za kisheria na za kimuundo zinazotakiwa kuchukuliwa na Serikali ili ushiriki wa mashirika yetu usikumbane na mikingamo ya kisheria na vikwazo vya mazoea ya watumishi na watendaji,” amesema.
Amesema anatarajia kuwa washiriki wa mkutano huo watapendekeza namna mashirika yanavyoweza kuunganisha nguvu katika kutekeleza aina fulani ya mradi na ushirika huo ukawa na tija.
“Kutokana na majadiliano yenu, naamini mtaainisha vihatarishi (risks) vilivyopo kwa mashirika ya Serikali kushiriki moja kwa moja kwenye utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo na kupendekeza mbinu za kukabiliana na vihatarishi hivyo; na pia mtashauri namna bora ya kutekeleza mapendekezo yenu bila kuathiri majukumu mahsusi ya uanzishwaji wa mashirika,” amesema.
Amesema yaya binafsi anasubiri kwa shauku kubwa, muhtasari wa mkutano huo ambao anataraji utakuwa na mapendekezo yanayotekelezeka ya namna gani mashirika yaliyopo nchini kwa umoja wake au moja moja yanavyoweza kushiriki kikamilifu kwenye ajenda hiyo ya maendeleo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, FEBRUARI 28, 2017.
 |
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa akihutubia wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma ulioandaliwa kwa ushirikiano
baina ya Taasisi ya Uongozi na Msajili wa Hazina leo Jijini Dar es Salaam.
Lengo la mkutano huo ni kujadili nafasi ya Mashirika ya Umma katika utekelezaji
wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 -2020/21.
Kutoka kulia ni Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja na
Kaimu Msajili wa Hazina, Elias Mwakibinga.
|
 |
Waziri wa Fedha na Mipango
Dkt. Philip
Mpango akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma
ulioandaliwa kwa ushirikiano baina ya Taasisi ya Uongozi na Msajili wa Hazina
leo Jijini Dar es Salaam. Lengo la mkutano huo ni kujadili nafasi ya Mashirika
ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka
Mitano 2016/17 -2020/21. Kutoka kulia ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Kassim Majaliwa, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph
Semboja na Kaimu Msajili wa Hazina, Elias Mwakibinga.
|
 |
Mtendaji
Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja akielezea jambo wakati wa
ufunguzi wa Mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma ulioandaliwa kwa ushirikiano
baina ya Taasisi ya Uongozi na Msajili wa Hazina leo Jijini Dar es Salaam.
Lengo la mkutano huo ni kujadili nafasi ya Mashirika ya Umma katika utekelezaji
wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 -2020/21. Kutoka kulia ni Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Maduka Kessy, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa na Kaimu Msajili wa Hazina,
Elias Mwakibinga.
|
 |
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (katikati) pamoja na Waziri wa Fedha na
Mipango Dkt. Philip Mpango (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja wakifuatilia matukio katika mkutano huo. |
 |
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN)
inayozalisha magazeti ya na DailyNews HabariLeo, SundayNews na SpotLeo. Dkt. Jim
Yonaz akiteta jambo na Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Ubunifu wa kampuni hiyo
Ichikael Maro waliposhiriki katika mkutano huo, ulioandaliwa kwa ushirikiano
baina ya Taasisi ya Uongozi na Msajili wa Hazina leo Jijini Dar es Salaam.
|
 |
Baadhi ya washiriki wa
Mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma ulioandaliwa kwa ushirikiano baina ya
Taasisi ya Uongozi na Msajili wa Hazina wakifuatilia mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam. Lengo la mkutano
huo ni kujadili nafasi ya Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa
Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 -2020/21. |
 |
Waziri Mkuu wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa
akiagana na Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uongozi Profesa Joseph Semboja
mara baada ya kufungua Mkutano wa Wakuu wa Mashirika ya Umma ulioandaliwa kwa
ushirikiano baina ya Taasisi ya Uongozi na Msajili wa Hazina wakifuatilia
mkutano huo leo Jijini Dar es Salaam.
Lengo la mkutano huo ni kujadili nafasi ya Mashirika ya Umma katika utekelezaji
wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano 2016/17 -2020/21. |
 |
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa Mkutano wa Wakuu
wa Mashirika ya Umma ulioandaliwa kwa ushirikiano baina ya Taasisi ya Uongozi
na Msajili wa Hazina wakifuatilia mkutano huo
leo Jijini Dar es Salaam. Lengo la mkutano huo ni kujadili nafasi ya
Mashirika ya Umma katika utekelezaji wa Mpango wa Pili wa Taifa wa Maendeleo wa
Miaka Mitano 2016/17 -2020/21. (Picha na Frank Shija – MAELEZO).
|

COMMENTS