TaGLA YAWEZESHA MAFUNZO YA KUTOA HUDUMA KWA MAJERUHI WA AJALI KWA NJIA YA VIDEO
HomeJamii

TaGLA YAWEZESHA MAFUNZO YA KUTOA HUDUMA KWA MAJERUHI WA AJALI KWA NJIA YA VIDEO

Mratibu wa Mafunzo ya Mabingwa wa Tiba ya Mifupa nchini ( SICOT , Société Internationale de Chirurgie Orthopédique et de Traumatolo...

ZAIDI YA WATU KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO BIASHARA CHA PAPAI SALAMA
PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100: UHAMIAJI
SERIKALI YAANZA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA KUPANUA WIGO WA VIVUTIO VYA UTALII NCHINI



Mratibu wa Mafunzo ya Mabingwa wa Tiba ya Mifupa nchini (SICOT , Société Internationale de Chirurgie Orthopédique et de Traumatologie) Dk. Robert Mhina (kulia) kutoka Taasisi ya Mifupa Tanzania (MOI) , akishiriki mafunzo ya utoaji huduma kwa majeruhiwa wa ajali kwa njia ya video yaliyoratibiwa na kufanyika kwa njia ya video kwenye kumbi za
Wakala ya Mafunzoa kwa Njia ya Mtandao, yakijumuisha nchi. Kushoto ni Dk.Lukwinyo na Dk. Mbaruku Mlinga.




 Madaktari mbalimbali wakifuatilia mafunzo hayo kwa makini.

Madaktari wa Tiba ya Mifupa wakishiriki mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Dk.Hamid Masoud, Dk.Valentine Restus na Dk. Joseph Msemwa.


Na Dotto Mwaibale

UMOJA wa Madaktari Bingwa wa Mifupa Duniani (SICOT) ikishirikiana na Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA), umetoa elimu ya  kutoa huduma kwa majeruhi wa ajali kwa njia ya mtandao wa mafunzo kwa njia ya video.

Umoja huo ulitoa elimu hiyo kwa kushirikiana na Madaktari Bingwa na wataalamu wa Mifupa kutoka nchi za Tanzania, Marekani, Pakistani na Brazil.

Akizungumza mara baada ya mafunzo hayo akiwa TaGLA, Dar es Salaam, Mratibu wa Umoja huo hapa nchini, Dk. Robert Mhina alisema kupitia mafunzo haya wameweza kujadili mambo mbalimbali yahusuyo ajali za barabarani.

“Huwa tunajadili mada mbalimbali kama ajali za barabarani kwa kubadilishana uzoefu na Madaktari wa nchi nyingine kwa kutumia mtandao wa mafunzo kwa njia ya video, na wakati wote huwa tunazungumza na nchi kutoka mabara mengine ili kubadilishana uzoefu,”alisema.

Alisema madaktari hao huwa wanakubaliana katika kujadili mada na kujadili kuhusu mambo muhimu yanayohusu tiba ya mifupa huku wakipeana majukumu.

“Kupitia vikao hivi hutusaidia sana hata kwa wale wanafunzi wanaojifunza Ubingwa kuona kitu gani kinaendelea duniani, bila gharama za kusafiri nje ya nchi” alisema Dk Mhina.

Alisema tayari Umoja huu inaangalia uwezekano wa kutoa nafasi kwa wanafunzi kutembela vituo kingine katika nchi hizo ili kuona na kuongeza uzoefu zaidi.

“Mwaka huu kuna vikao kama sita hivi, kikao hiki ni mwazo tu,”alisema na kuongeza kuwa kupitia mkutano huo itawasaidia wananchi kwa kuboreshewa ufanyaji wa tiba sahihi za mifupa hivyo kupata huduma za matibabu zilizoboreshwa kutokana na ajali za barabarani.

Watoa mada katika mkutano huo uliofanyika kwa njia ya video walikuwa ni pamoja na Dk. Syed M. Avais wa King Edward Medical University, Dk. Robert D. Zura wa Louisiana State University Health Science Center na Dk. Robert I. Mhina, wa  Taasisi ya Mifupa Tanzania (MOI) kutoka nchini Tanzania.

(Imeandaliwa na mtandao wa www.habari za jamii.com-simu namba 0712-727062)

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TaGLA YAWEZESHA MAFUNZO YA KUTOA HUDUMA KWA MAJERUHI WA AJALI KWA NJIA YA VIDEO
TaGLA YAWEZESHA MAFUNZO YA KUTOA HUDUMA KWA MAJERUHI WA AJALI KWA NJIA YA VIDEO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizyh3OGsoLSGmoTwB9pcrE4ukqpqfv_2pYrJ8mScdwuJG1xgzMEEm3a65pU3Tg07eSFxPgXC8pEnW2o0JVOcLbWi7_jiyAB40aBKQkM3m20XA8Fi7xhE6gDvaKp81A8_X4NnOrbxnz4v7e/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEizyh3OGsoLSGmoTwB9pcrE4ukqpqfv_2pYrJ8mScdwuJG1xgzMEEm3a65pU3Tg07eSFxPgXC8pEnW2o0JVOcLbWi7_jiyAB40aBKQkM3m20XA8Fi7xhE6gDvaKp81A8_X4NnOrbxnz4v7e/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/02/tagla-yawezesha-mafunzo-ya-kutoa-huduma.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/02/tagla-yawezesha-mafunzo-ya-kutoa-huduma.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy