Aliyekuwa meneja wa wema Martin Kadinda akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu pamoja na wanasheria Na Humphrey Shao, Globu ya...
Aliyekuwa meneja wa wema Martin Kadinda akiwa katika mahakama ya hakimu mkazi kisutu pamoja na wanasheria
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Mwanamitindo maarufiu nchini, Martin Kadinda amesema kuwa yeye sio meneja wa Wema Sepetu kwa sasa, bali amefika mahakamani hapo kama rafiki wa karibu wa msanii huyo.
Kadinda amesema hayo katika maongezi maalum na mwandishi wa globu ya jamii juu ya uhusiano wake na Wema Sepetu kwa sasa. hasa mara baada ya kuhusishwa na tuhuma za matumizi na uuzwaji wa dawa za kulevya.
“kwa sasa mie sio meneja wa wema,mimi ni rafiki yake tu wa karibu hivyo nimeamua kuja hapa kwa ajili ya kujua rafiki yangu amefikia wapi katika kipindi hiki ambacho anapitia magumu” amesema Kadinda
Ametaja kuwa yeye kwa sasa anaendelea na biashara yake ya kushona suti tu ili aweze kujipatia ugali wake wa kila siku na sio kujihusisha na makundi ambayo sio sahiii.Hata hivyo kadinda ameonekana akisubiri kwa hamu kubwa kuona rafiki yake anafikishwa mahakamani hapo,lakini haikuwa hivyo Wema hakufikishwa tena mahakamani hapo.
COMMENTS