SERIKALI YAUNDA TUME KUCHUNGUZA KUUNGUA KWA CHUMBA CHA MIZIGO UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM
HomeJamii

SERIKALI YAUNDA TUME KUCHUNGUZA KUUNGUA KWA CHUMBA CHA MIZIGO UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM

  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati), akiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Uwanja wa N...

EYAKUZE, MKURUGENZI MTENDAJI WA TWAWEZA NA MKUTANO UNAOJADILI UWEPO ZA SHERIA ZA HABARI, HAKI YA KUPATA TAARIFA MJINI PARIS
PROFESA MBARAWA ATETA NA MAKAMU WA RAIS WA JICA.
MKUTANO WA BARAZA KUU LA 24 LA SHIRIKA LA POSTA TANZANIA WAFUNGWA RASMI DAR ES SALAAM






 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati), akiwa na viongozi mbalimbali wakiwemo wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) wakati akitoka kukagua chumba namba cha kuhifadhia mizigo kilichoungua moto jana usiku.



 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (katikati), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari kuhusu hatua zilizofikiwa na serikali baada ya kutokea moto huo. Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Gabriel Migile na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Profesa Ninatubu Lema.
 Mkutano na wanahabari ukiendelea. 


 Paa la chumba kilichoungua.
 Waandishi wa habari wakiangalia chumba hicho.
 Chumba namba mbili cha kutunzia mizigo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), kikiwa kimetekea kwa moto uliotokea jana usiku katika uwanja huo.
wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imeunda tume ya watu 12 kwa ajili ya kuchunguza tukio la kuungua moto chumba namba mbili cha kuhifadhia mizigo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA).

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa alisema tume hiyo itaongozwa na Mwenyekiti wa Bodi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Joseph Nyahende.

"Tume hiyo tumeipa muda wa mwezi mmoja ili kukamilisha uchunguzi huo ambapo tutatoa taarifa kamili ya chanzo cha moto huo" alisema Mbarawa.

Akizungumzia kuhusu tukio hilo alisema moto huo ulitokea jana usiku kwenye chumba namba mbili cha kuhifadhia mizigo ya abiria katika uwanja huo hata hivyo thamani ya vitu vilivyoungua bado haijajulikana.

Katika hatua nyingine Waziri Mbarawa ameinyoonyea kidole kampuni inayofanya kazi ya kupokea mizigo katika uwanja huo ya Swissport kuwa iache kufanya njama za kuzuia kampuni ya Nas Dar Airco iliyopewa mkataba wa kazi katika uwanja kufanya kazi vinginevyo serikali itaifutia leseni.

"Tunataarifa kuwa nyinyi Swissport mnaizuia kampuni hiyo kufanya kazi nasema badilikeni vinginevyo tutawafutia leseni yenu" aliagiza Profesa Mbarawa.

Profesa Mbarawa alitoa maagizo kwa kampuni hiyo ianze kufanya kazi haraka iwezekanavyo kama walivyokubaliana katika mkataba waliopewa.

Mkurugenzi Mkuu wa Swissport Mrisho Yassin hakuweza kuzungumzia suala hilo kwa wakati huo kutokana na mazingira yaliyokuwepo baada ya mkutano huo na alipopigiwa simu baadaye muda wote simu yake ilikuwa ipo bize.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SERIKALI YAUNDA TUME KUCHUNGUZA KUUNGUA KWA CHUMBA CHA MIZIGO UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM
SERIKALI YAUNDA TUME KUCHUNGUZA KUUNGUA KWA CHUMBA CHA MIZIGO UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiyIDqxmQu8od_7YKnM-aSWiCmvTOqwOEDSJOhc8S_bWJaipFf2cYlGd8SHQul8EWg92RFxWKpFHUL1ze3nPOivcCJQYii_i7WE4QVBazJB3ilFEx_5A1zbhmI-Ntegj-rHRw-ORN433xZF/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiyIDqxmQu8od_7YKnM-aSWiCmvTOqwOEDSJOhc8S_bWJaipFf2cYlGd8SHQul8EWg92RFxWKpFHUL1ze3nPOivcCJQYii_i7WE4QVBazJB3ilFEx_5A1zbhmI-Ntegj-rHRw-ORN433xZF/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/01/serikali-yaunda-tume-kuchunguza-kuungua.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/serikali-yaunda-tume-kuchunguza-kuungua.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy