Mohamed Saif, Zambia Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameongoza Ujumbe wa Tanzania kuelekea nchini Zambia il...
Mohamed Saif, Zambia
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameongoza Ujumbe wa Tanzania kuelekea nchini Zambia ili kuanza ziara ya kukagua njia nzima linapopita Bomba la Kusafirisha Mafuta ghafi kutoka Tanzania hadi Zambia (TAZAMA) na Vituo vinavyotumika kusukuma mafuta hayo.
Ziara hiyo ya kutembelea Mkuza wa Bomba imeanza rasmi tarehe 27 Januari huko Ndola nchini Zambia na kumalizika tarehe 31 Januari, 2017ambapo itafanywa kwa ushirikiano wa Mawaziri wa Nishati kutoka Tanzania na Zambia wakiambatana na Makatibu wakuu, pamoja na viongozi waandamizi kutoka nchi zote mbili sambamba na uongozi wa TAZAMA.
Kufanyika kwa ziara hiyo kumetokana na makubaliano ya Marais wa nchi husika, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli na Mhe. Edgar Lungu ya Tarehe 28 Novemba, 2016 kuhusu kuboresha zaidi Bomba hilo la TAZAMA kwa manufaa ya nchi zote mbili.
Imeelezwa kuwa Ziara hiyo inafanyika kwa kufuata njia ya Mkuza kwa kupitia vituo vyote vinavyosukuma mafuta na baadaye kikao cha pamoja cha viongozi hao kitakachofanyika jijini Dar es Salaam.
Ziara hii imechagizwa pia na ziara ya Rais Lungu kwenye kituo cha TAZAMA jijini Dar es Salaam ambapo ilielezwa kuwa ufanisi wa bomba hilo umeshuka ikilinganishwa na hapo hapo awali kwani lilikuwa na uwezo wa kusafirisha tani milioni 1.1 za mafuta kwa mwaka lakini kwa sasa linasafirisha tani 600,000 tu.
Hivyo ili kuboresha miundombinu ya TAZAMA, nchi hizo zimekubaliana kushughulikia chanzo cha kuzorota kwa utendaji kazi wa TAZAMA ili Bomba hilo liweze kuendeshwa kwa faida kwa kunufaisha pande zote mbili.
Ziara hiyo pia imelenga kufanya tathmini kwa kukagua Mkuza wa Bomba na maeneo yanayopendekezwa kujengwa bomba la kusafirisha Mafuta Safi (Finished Product) na Gesi Asilia kutoka Tanzania hadi Zambia kupitia njia ya Mkuza huo (way-leave) wa bomba la TAZAMA.
Bomba la kusafirisha mafuta ghafi la TAZAMA linaloanzia nchini Tanzania hadi mji wa Ndola nchini Zambia lina urefu wa kilomita 1,710 na kipenyo cha inchi 8 hadi 12 na lilianza kazi Mwaka 1968.
Rais wa Zambia, Mhe.
Edgar Lungu (kushoto) akifurahia jambo na Waziri wa Nishati na Madini wa
Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kumalizika kwa mkutano
uliofanyikia Ikulu ya Zambia.
|
Rais wa Zambia, Mhe.
Edgar Lungu (wa tatu kushoto mstari wa nyuma) katika picha ya pamoja na Ujumbe
kutoka Tanzania na Baadhi ya Mawaziri wa nchini Zambia.
|
Rais wa Zambia, Mhe.
Edgar Lungu (kushoto) akifurahia jambo na Waziri wa Nishati na Madini wa
Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo mara baada ya kumalizika kwa mkutano
uliofanyikia Ikulu ya Zambia.
|
COMMENTS