NCHI HAIJAKUMBWA NA BAA LA NJAA-MAJALIWA
HomeJamii

NCHI HAIJAKUMBWA NA BAA LA NJAA-MAJALIWA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nchi haijakumbwa na baa la njaa na amewataka Watanzania utosikiliza kampeni za upotoshwaji z...


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema nchi haijakumbwa na baa la njaa na amewataka Watanzania utosikiliza kampeni za upotoshwaji zinazofanywa na baadhi ya wafanyabiasha kuhusu hali ya chakula kwani si za kweli bali ni za uzushi zenye lengo la  kupandisha bei za vyakula.
Amesema Serikali ndio yenye jukumu la kutoa taarifa za kuwepo kwa njaa ama kutokuwepo na kwamba taarifa zinazosambazwa za kuwepo kwa baa la njaa nchini hazina ukweli wowote na Serikali inawahakikishia wananchi kuwepo kwa usalama wa chakula.

Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo
(Jumatatu, Januari 16, 2017) wakati akizungumza na waandishi wa habari mkoani hapa mara baada ya kuzindua safari za ndege za Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kutoka Dar es Salaam kwenda Dodoma, ambapo amesisitiza kwamba hali ya upatikanaji chakula nchini ni tofauti na inavyoelezwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo baada ya kutolewa kwa taarifa katika vyombo mbalimbali vya habari kuhusu kuwepo kwa baa la njaa nchini jambo ambalo si la kweli. Amewataka wananchi kuwa watulivu na jambo hilo likitokea Serikali itatoa taarifa.
“Mwaka jana nchi ilikuwa na akiba ya chakula cha zaidi ya tani milioni tatu hali iliyopelekea baadhi ya Wabunge na wafanyabiashara kuomba kibali cha kuuza nafaka nje ya nchi, ambapo Serikali ilitoa kibali hicho baada ya kujiridhisha kuwepo kwa akiba ya kutosha ya chakula,” amesema.
Amesema baada ya kutolewa kwa kibali hicho tani milioni 1.5 ziliuzwa nje ya nchi na
Kiasi cha tani milioni 1.5 zilizobaki zilihifadhiwa kama akiba ambapo tayari wameruhusu ziuzwe hapa nchini ili kupunguza kupanda kwa bei za vyakula nchini.

“Naomba wananchi msiwe na wasiwasi juu ya hali ya chakula nchini. Msisikilize kelele zinazopigwa na watu mbalimbali pamoja kwenye baadhi ya vyombo vya habari yakiwemo magazeti kwani taarifa hizo si za kweli. Chakula kipo cha kutosha licha ya mvua kusuasua katika baadhi ya maeneo nchini,” amesema.
Hata hivyo Waziri Mkuu amesema kuwa kwa sasa mvua zimeanza kunyesha katika maeneo mbalimbali nchini, hivyo amewaomba wananchi kuzitumia kwa kulima mazao ya muda mfupi yanayostahimili ukame.
Waziri Mkuu amesema kwamba endapo kutatokea uhaba wa chakula nchini, Serikali itatoa utaratibu wa namna ya upatikanaji wa chakula kwa wananchi wake. Kuhusu kupanda wa bei ya vyakula katika baadhi ya masoko amesema inatokana na kuwepo kwa uhaba wa chakula katika nchi jirani.

Aidha, Waziri Mkuu amesema kwamba Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, itatoa taarifa kuhusiana na hali halisi ya chakula nchini kwa sasa na pia itatoa taarifa kuhusu hali ya mvua ili Watanzania waweze kupata ukweli wa hali ilivyo.

 IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.     
JUMATATU, JANUARI 16, 2017.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: NCHI HAIJAKUMBWA NA BAA LA NJAA-MAJALIWA
NCHI HAIJAKUMBWA NA BAA LA NJAA-MAJALIWA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgMbQRm92iMG2c6NlmLFPKVXOTx4PHL5seEMBKRGfuon_aWsSD4-BdNrSacQcVKxnojnn7gKKrzdnTZn1TfN0-94ZcyMlPQXlIqBR6pInA28Gx-pPg7xr_btdL5FeKjC0CAGc4JSUZF1AM/s320/download.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgMbQRm92iMG2c6NlmLFPKVXOTx4PHL5seEMBKRGfuon_aWsSD4-BdNrSacQcVKxnojnn7gKKrzdnTZn1TfN0-94ZcyMlPQXlIqBR6pInA28Gx-pPg7xr_btdL5FeKjC0CAGc4JSUZF1AM/s72-c/download.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/01/nchi-haijakumbwa-na-baa-la-njaa-majaliwa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/nchi-haijakumbwa-na-baa-la-njaa-majaliwa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy