NA K-VIS BLOG ALIYEKUWA Mgombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu mstaafu, Bw. Edward L...
NA K-VIS BLOG
ALIYEKUWA
Mgombea kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Waziri Mkuu mstaafu,
Bw. Edward Lowassa, amekamatwa na polisi mkoani Geita akiwa njiani kuelekea
kwenye mkutano wa kampeni za udiwani kata ya Nkome mkoani hum oleo Januari 16,
2017.
Taarifa
kutoka Geita zinasema, pamoja na Bw. Lowassa, Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa
Geita, Bi. Upendo Furaha Peneza, naye pia amekamatwa. Bi Peneza alikuwa kwenye
msafara wa Bw. Lowassa.
Taarifa zaidi
zinasema, Bw. Lowassa alikumbana na “mkono wa dola” baada ya kusimamishwa na
wananchi waliokuwa wamejipanga pembezoni mwa barabara na hapo msafara wake
ulisimama na kuanza kuwasalimia, kitendo ambacho wapasha habari wanasema
kiliwafanya polisi kumtia mbaroni na kuamuru msafara wake uelekee kituo cha
polisi.
“Msafara wa
Bw. Lowassa ulikuwa ukitokea moani Kagera na ulipofika stendi ya zamani Geita
wananchi wakamsimamisha, aliposhuka kwenye gari kuwasalimu wanageita, polisi
wakamkamata na kumpeleka kituo cha Polisi Geita.” Mmoja wa mashuhuda alisema.
Taarifa zilizopatikana baadaye zinasema, Bw. Lowassa ameachiwa huru baada ya kuhojiwa na polisi na msafara wake sasa umeelekea mkoani Mwanza.
Taarifa zilizopatikana baadaye zinasema, Bw. Lowassa ameachiwa huru baada ya kuhojiwa na polisi na msafara wake sasa umeelekea mkoani Mwanza.
COMMENTS