ASKOFU MOKIWA AWAONGOZA WAUMINI WAKE KUTOA MSAADA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAM
HomeJamii

ASKOFU MOKIWA AWAONGOZA WAUMINI WAKE KUTOA MSAADA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAM

 Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk.Valentino Mokiwa (katikati), akiwaongoza waumini wa kanisa hilo Archidikonari ya Kin...

BALOZI DK. PINDI CHANA NA MWENYEKITI WA BODI YA WADHAMINI WA LAPF WATEMBELEA BANDA LA LAPF MAONYESHO YA SABASABA
WAZIRI WA USALAMA WA KENYA JENERALI MSTAAFU JOSEPH NKAISSERY AFARIKI DUNIA
BEI YA DAWA ZA SERIKALI YASHUKA NCHINI





 Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Dk.Valentino Mokiwa (katikati), akiwaongoza waumini wa kanisa hilo Archidikonari ya Kinondoni kufanya usafi katika viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala Dar es Salaam leo asubuhi wakati kanisa hilo lilipotoa msaada wa vitanda na magodoro katika hospitali hiyo vyote vikiwa na thamani ya sh.milioni 12.

 Waumini wa kanisa hilo wakiendelea na kufanya usafi.
 Takataka zikipelekwa eneo maalumu.
 Takataka zikipelekwa kutupwa.
 Waumini wa kanisa hilo wakipiga picha mbalimbali za tukio hilo.


Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Tanzania, Dk.Valentino Mokiwa (kulia), akipanda mti nje ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, wakati alipowaongoza waumini wa kanisa hilo  kutoa msaada wa magodoro na vitanda vya wagonjwa pamoja na kufanya usafi wa mazingira Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto anayemsaidia kupanda mti ni Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk.Daniel Nkungu na wengine ni waumini wa kanisa hilo.  


 Kiongozi wa  kanisa hilo wilaya ya Kinondoni Achidikin Con Mathew Maigwa (kulia), akipanda mti.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Daniel Nkungu (kulia), akipanda mti.
 Ofisa  Afya wa Hospitali hiyo, Amina Pole (kushoto), 
akipanda mti.
 Waumini wa kanisa hilo na viongozi wao wakiwa kwenye 
tukio hilo.
 Askofu Dk. Valentino Mokiwa akimkabidhi moja ya kitanda kati ya 15,  Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daniel Nkungu.
Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo, Daniel Nkungu akitoa neno la shukurani kwa niaba ya Serikali baada ya kupokea msaada huo.

Na Dotto Mwaibale

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Angilikana Tanzania, Dk Valentino
Mokiwa amesema migogoro ya kisiasa inayoibuka hivi sasa inaweza kuhatarisha hali ya amani nchini.

Dk. Mokiwa ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam leo wakati
akiwaongoza waumini wa  kanisa hilo 
Archidikonari ya Kinondoni kutoa misaada ya vifaa tiba na kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala.

"Migogoro ya kisiasa ambayo imeanza kuzuka hivi sasa
inaweza kuhatarisha amani ya nchi ni vizuri viongozi wanaovutana wakutana na
kuweka mambo sawa" alisema Mokiwa.

Alisema migogoro ya kisiasa inayoendelea inaweza kusababisha
kutoweka kwa amani hivyo ni jukumu la viongozi husika kuliangalia jambo hilo
kwa karibu na kulitafutia ufumbuzi.

Alisema nchi yetu inahitaji amani na utulivu na kuondokana
na matukio ya kuogopesha akitolea mfano miili ya watu saba iliyokutwa ndani ya viroba vilivyotupwa mto Ruvu Bagamoyo mkoani Pwani.

Alisema matukio kama hayo yanaweza kuwafanya wananchi
kukimbia nchi yao kwa hofu hivyo inatakiwa kila mmoja wetu kuwa na hofu ya Mungu.

Akizungumzia msaada uliotolewa na kanisa hilo katika
hospitali hiyo 
 ambao ni  vitanda 15, magodoro 20, mashuka 40 na viatu vya tahadhri jozi 30 vyenye thamani ya Sh milioni 12 alisema kanisa hilo kwa muda mrefu limekuwa likifanya maombi ya
kuwaombea viongozi wa nchi na kutoa misaada ya kijamii hususan katika sekta ya afya, elimu na maeneo mengine.

Mokiwa alisema wananchi wanapokuwa katika afya bora ndipo
wanapoweza kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo hivyo kuinua uchumi wao na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa  kanisa hilo wilaya ya Kinondoni Achidikin Con Mathew Maigwa alitoa mwito kwa wadau wa maendeleo kote nchini kuwa na moyo wa kusaidia watu wenye uhitaji kama
wanavyotoa michango ya harusi na sherehe nyingine.

Alisema ni jukumu la kima mmoja wetu wa kusaidia jamii na si
kuiachia serikali pekee na ndio maana kanisa hilo limekuwa likifanya hivyo kama
neno la mungu linavyoelekeza kuwa tupendane kwani unapokwenda kumfariji mgonjwa
inasaidia kumpa hali ya unafuu.



Akizungumza kwa niaba ya serikali na Mganga Mkuu wa
Hospitali hiyo Mwakilishi wa Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk. Daniel Nkungu alilishukuru
kanisa hilo kwa msaada huo na kusema inazidisha ari ya kazi kwa wafanyakazi na
kuwafariji wagonjwa ikiwa na kuwafanya wapate nafuu na kupona  haraka.

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: ASKOFU MOKIWA AWAONGOZA WAUMINI WAKE KUTOA MSAADA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAM
ASKOFU MOKIWA AWAONGOZA WAUMINI WAKE KUTOA MSAADA NA KUFANYA USAFI HOSPITALI YA MWANANYAMALA JIJINI DAR ES SALAAM
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgvWhPyP1RbOvFZeFnj8jBQCQDnYvHTibidWgWYxhyphenhyphenKaKAlLXHhtFdhx9_snHRShJSStDazdiMR1KApMpL3-WXgOYw8p9a1bAM9giH0mFxRkxQ6iyT7Sz0NA7ELc2epra99mNXdfd0WOcMJ/s640/IMG_8871.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgvWhPyP1RbOvFZeFnj8jBQCQDnYvHTibidWgWYxhyphenhyphenKaKAlLXHhtFdhx9_snHRShJSStDazdiMR1KApMpL3-WXgOYw8p9a1bAM9giH0mFxRkxQ6iyT7Sz0NA7ELc2epra99mNXdfd0WOcMJ/s72-c/IMG_8871.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2017/01/askofu-mokiwa-awaongoza-waumini-wake.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2017/01/askofu-mokiwa-awaongoza-waumini-wake.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy