MKUTANO MKUU WA WANABLOGU TANZANIA 2016 UMEFUNGUA MILANGO YA MAFANIKIO.
HomeJamii

MKUTANO MKUU WA WANABLOGU TANZANIA 2016 UMEFUNGUA MILANGO YA MAFANIKIO.

Disemba 05 na 06 mwaka huu 2016 ulifanyika Mkutano Mkuu wa Waendeshaji/ Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii nchini kupitia umoja wao w...








Disemba 05 na 06 mwaka huu 2016 ulifanyika Mkutano Mkuu wa Waendeshaji/ Wamiliki wa Mitandao ya Kijamii nchini kupitia umoja wao wa Tanzania Bloggers Network TBN, uliofanyika ukumbi wa PSPF Jijini Dar es salaam.

Siku ya kwanza ilikuwa mahususi kwa ajili ya semina kwa wanablogu hao juu ya namna ya kuendesha mitandao yao kwa ajili ya manufaa ya kijamii na yao pia. Siku ya pili ilikuwa mahususi kwa ajili ya mkutano Mkuu ambapo wajumbe wa mkutano huo waliwachagua viongozi wao ambapo Mwenyekiti wa TBN Joachim Mushi (aliyesimama juu) na wasaidizi wake walisalia katika nafasi zao.
#BMGHabari

Mkutano huo ulifunguliwa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas, ambapo alitamka rasmi kwamba serikali inatambua mchango wa wanablogu nchini katika kuipasha jamii habari hivyo itaendelea kushirikiana nao akionya watendaji wa serikali hususani maafisa habari wa mikoni wasiotoa ushirikiano kwa wanablogu hao kuacha mara moja tabia hiyo.

Katika kilele cha mkutano huo, mgeni rasmi alikuwa Waziri wa habari, utamaduni, sanaa na michezo, Nape Nnauye, ambaye alikiri umuhimu wa wanablogu nchini akisema kwamba, watatambuliwa rasmi kupitia kanuni za sheria mpya ya vyombo vya habari nchini ya mwaka 2016 na kwamba watapewa kadi za wanahabari (Press Card) ili kuwasaidia katika utendaji wao wa kazi.

Kauli iliyowafurahisha wengi ni ile ya Waziri Nnauye aliyowakaribisha wadau mbalimbali ili kufanikisha utoaji wa tuzo kwa wanablogu kwa mwaka ujao 2017 akisema wanafanya kazi kubwa hivyo ni vyema kutambua mchango wao kupitia tuzo.

BMG inawapongeza wote waliofanikisha mkutano huo, ikiwemo Bank ya NMB kwa ufadhiri wake, NHIF, PSPF, Kampuni ya bia Serengeti, Cocacola na TANAPA. Kwa pamoja tuienzi kaulimbiu ya mkutano huo, "Mitandao ya Kijamii ni Ajira, Itumike kwa Manufaa".
Kutoka (kushoto) ni Katibu wa TBN, Khadija Kalili, Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dk. Hassan Abbas na Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili na mjumbe wa kamati tendaji TBN, Klantz Mwantepele.
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas (kulia), akizungumza kwenye mkutano huo. Katikati ni Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi na kushoto ni Katibu wa TBN, Khadija Kalili.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa TBN, Joachim Mushi, Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo na Msemaji wa Serikali Dk. Hassan Abbas na Meneja Mwandamizi wa Amana Huduma za Bima na Ziada wa Benki ya NMB, Stephen Adili.
Mwanablogu akitoa neno la shukurani kwa niaba ya wenzake.
Mwanahabari na Blogger  Frederick Katulanda 
Wanablogu wakiendelea kutoa mawazo yao katika kuijenga TBN
Wanablogu wanachama wa TBN
Wanablogu wanachama wa TBN
Tazama HAPA na HAPA ujionee.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MKUTANO MKUU WA WANABLOGU TANZANIA 2016 UMEFUNGUA MILANGO YA MAFANIKIO.
MKUTANO MKUU WA WANABLOGU TANZANIA 2016 UMEFUNGUA MILANGO YA MAFANIKIO.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhGWR79sTSkqI77oE_bpEbLjU0smdHIutVEXS8gWlMyA7oaTzVRg9eyda5FKD81vvjwtNDCqMOZBJ-NNj3HwkoGFPBejcKxhiJatqebGHuhob9I-B54aov8p_gGGwRuOsWticlgZsrI8Lc/s640/4.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhGWR79sTSkqI77oE_bpEbLjU0smdHIutVEXS8gWlMyA7oaTzVRg9eyda5FKD81vvjwtNDCqMOZBJ-NNj3HwkoGFPBejcKxhiJatqebGHuhob9I-B54aov8p_gGGwRuOsWticlgZsrI8Lc/s72-c/4.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/mkutano-mkuu-wa-wanablogu-tanzania-2016.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/mkutano-mkuu-wa-wanablogu-tanzania-2016.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy