MAJALIWA AZINDUA KIWANDA CHA PLASTIC CHA LODHIA JIJINI ARSHA
HomeMikoani

MAJALIWA AZINDUA KIWANDA CHA PLASTIC CHA LODHIA JIJINI ARSHA

Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akimpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Ma...

WAKULIMA WILAYANI HAI WASIFU MRADI WA N2AFRICA KWA MBEGU BORA ZA MAZAO YA MAHARAGE
TUME YA TAIFA YA MIPANGO YA MATUMIZI YA ARDH I(NLUPC) YATOA TATHIMINI YA UTAFITI WALIOFANYA KORIDO YA MNGETA NA UKANDA WA UDZUNGWA-MGOMBELA-SELOUS,KILOMBERO-MOROGORO
MAZISHI YA WATOTO WATATU WALIOFARIKI KWA KULIPUKIWA NA BOMU WILAYANI MONDULI





Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akimpokea Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji, kilichopo Njiro jijini Arusha, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa wakati alipofika kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia (wa kwanza kushoto waliokaa) akiteta jambo na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akifuatiwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo na Naibu waziri wa kilimo ,Mifugo na Uvuvi Mhe. William Ole Nasha wakati walipofika kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akikata utepe tayari kwa uzinduzi wa kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha, 3 Disemba 2016.
Kutoka Kushoto (mwenye suti bluu) ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Sailesh Pandit, Mwenyekiti wa kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia wakiongozana na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akimkaribisha Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ili kuongea na hadhara iliyopo kwenye kiwanda hicho mara baada ya kuzindua kiwanda kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akiongea machache mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa akizindua jiwe la msingi katika kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha, 3 Disemba 2016.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Sailesh Pandit akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha Leo, 3 Disemba 2016.
Mwenyekiti wa kampuni ya Lodhia Group Bw. Arun Lodhia akiagana na Waziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa mara baada ya kuzindua kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha, 3 Disemba 2016.


Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Lodhia Group Bw. Sailesh Pandit akisoma risala mbele ya Mgeni rasmi ambaye niWaziri Mkuu wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa ndani ya kiwanda cha Lodhia Plastic kinachotengeneza Mabomba ya Maji ,kilichopo Njiro jijini Arusha, 3 Disemba 2016. (Picha zote Gadiola Emanuel)

Na Woinde Shizza , Arusha.

Halmashauri za majiji, manispaa na miji wametakiwa kutumia mabomba ya maji yanayozalishwa nchini badala ya kuagiza bidhaa hiyo toka nje ili kuweza kuvinufaisha viwanda vya ndani.


Hayo yamebainishwa na waziri mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa wakati akizindua kiwanda cha kutengeneza mabomba ya Plastic ya maji yenye ukubwa wa aina mbalimbali (Lodhia Plastics ) kilichopo njiro jijini hapa.

Alisema kuwa haiana haja ya halmashauri au majiji kuagiza bidhaa mbalimbali nje ya nchi wakati nchi yetu inaviwanda vya kutosha vya kutengeneza bidhaa hizo.



“Sioni sababu ya wahandisi wa Halmashauri na washauri elekezi halmashauri kushinikiza wakandarasi wa hapa Arusha kwenda kununua mabomba ya maji nje ya mkoa wakati hapa kuna kiwanda kama Lodhia ambacho kinatengeneza hizo bidhaa kwakweli hii labda iwe ni chuki tu”alisema Majaliwa ambaye ameanza ziara ya siku nane mkoani Arusha.



Alisema ni muhimu kwa halmashauri kununua mabomba hayo kwa matumizi ya miradi ya maji na kuunga mkono juhudi zinazofanywa na wawekezaji wa ndani.



“Washauri wa miradi mbalimbali acheni chuki …waache wakandarasi wanunue bidhaa bora zilizothibitishwa na Shirika la Viwango la Taifa (TBS) na Shirika la Viwango la Kimataifa (ISO),” alisema.

Aidha alitoa mfano, kwa upande wa Mkoa wa Arusha kuna mpango wa kujenga mradi mkubwa wa maji utakaogharimu dola za Marekani milioni 200, na katika utekelezaji wake ni lazima watoe kipaumbele cha kutumia mabomba yanayozalishwa na kiwanda hicho.

Mradi huo ukikamilika unatarajiwa kumaliza kero ya maji kwa wakazi wa jijini hapa.

Alisisiza haoni umuhimu wa halmashauri na wakandarasi kununua mabomba kutoka nje ya Arusha au nje ya nchi wakati kuna mabomba yanayozalishwa na wawekezaji wazawa na yanakidhi viwango.

“Serikali yetu itaendelea kuwaenzi na kuwalinda wawekezaji wote wa ndani ambao wamekuwa msaada mkubwa wa kutoa ajira ambayo ni janga kwa taifa na dunia kwa ujumla”alisema Majaliwa.

Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Lodhia Group, Arun Lodhia, alisema serikali ichukue nafasi ya kuzungumza na wenye viwanda mara kwa mara ili kujua matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi.

Alisema viwanda chini ya kampuni hiyo, vinazalisha bidhaa nyingi zenye ubora lakini makampuni yanashindwa kununua na kupenda zaidi kununua bidhaa za nje.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho, Sailesh Pandit, alisema kwamba wanashindwa kuuza mabomba ya maji na malighafi nyingine katika miradi mikubwa ya maji iliyopo mkoani Arusha.

Alisema wanashindwa kufanya hivyo licha ya bidhaa zao kuwa na TBS na ISO kutokana na hujuma wanazofanyiwa na baadhi ya wahandisi na washauri elekezi wa miradi.

“Imeshatokea mara kadhaa kwa wakandarasi wanaotekeleza miradi kuzuiwa kununua mabomba ya maji kutoka Lodhia Plastics na badala yake hulazimishwa kununua mabomba kutoka nje ya mkoa hivyo kuwasababishia gharama za ziada,” alisema.

Kuhusu ajira, alisema kiwanda hicho kimetoajiri Watanzania kati ya 1, 200 hadi 1, 300 lakini pia Watanzania zaidi ya 500 wananufaika kutokana na kushiriki katika utoaji wa huduma mbalimbali kiwandani hapo.

Alisema mtandao wa viwanda vinne vinavyomilikiwa na kampuni ya Lodhia Group wanalipa kodi wastani wa Sh. bilioni 20 kwa mwaka.

Kwa upande wao, baadhi ya makandarasi, Samuel Lugemalila wa Kampuni ya Vest Tanzania Ltd na Kastuli Mandange kutoka Fraju Group Ltd na Maxmilian Iranghay wa kampuni Wining Spirit Construction Ltd, walitoa ushuhuda kuhusu namna washauri waelekezi na watumishi wengine wanavyowakataza kununua bidhaa za Lodhia Plastics na kuwataka wanunue zinazotengenezwa nje ya mkoa.

Walisema kitendo hicho kinawashababisha kushindwa kukamilisha miradi yao kwa wakati na kuwaongezea gharama kubwa.
Aidha waliiomba serikali kuondoa urasimu kwa wahasibu kulipa malipo kwa wakati licha ya miradi kukaguliwa na kupata cheti cha uhakiki wa kazi.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAJALIWA AZINDUA KIWANDA CHA PLASTIC CHA LODHIA JIJINI ARSHA
MAJALIWA AZINDUA KIWANDA CHA PLASTIC CHA LODHIA JIJINI ARSHA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1cvxWBGrcN9-JlYYDO_Lj6JlASdAIkqe0iBdYvkJGuPld4EMSPOoTvovELG1bPRJnQZJdqWMTRBDP6yyzNk223TgJ0dCB0S7HOMwnlB9Nh8WZT5K_iDr0aoEJzIeOYbh-wAxr4QzG8rCj/s640/DSC_0242.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg1cvxWBGrcN9-JlYYDO_Lj6JlASdAIkqe0iBdYvkJGuPld4EMSPOoTvovELG1bPRJnQZJdqWMTRBDP6yyzNk223TgJ0dCB0S7HOMwnlB9Nh8WZT5K_iDr0aoEJzIeOYbh-wAxr4QzG8rCj/s72-c/DSC_0242.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/12/majaliwa-azindua-kiwanda-cha-plastic.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/12/majaliwa-azindua-kiwanda-cha-plastic.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy