Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlagosi akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni Kaimu Mkurugenz...
MAMLAKA ya Udhibiti wa huduma za Nishati na Maji, (EWURA), imetangaza ongezeko la bei
ya umeme kwa asilimia 8.5%.
ya umeme kwa asilimia 8.5%.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Felix Ngamlamgosi, ongezeko hilo la bei ni
kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), ambalo liliwasilisha maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari
mwaka 2017.
kufuatia maombi ya Shirika la Umeme Nchini, (TANESCO), ambalo liliwasilisha maombi EWURA ya kutaka ongezeko la bei kwa asilimia 18.19, ifikapo Januari
mwaka 2017.
Akitangaza bei hizo mpya jijini Dar es Salaam, leo Mkurugenzi Mkuu huyo wa EWURA amesema, baada ya kufanya uchambuzi wa kina, Mamlaka yake imefikia uamuzi wa kuongeza asilimia 8.5 itakayoanza kutumika Januari Mosi, 2017 kutokana na kuongezeka kwa gharama za uzalishaji wake.
Shirika la umeme Zanzibar (ZECO) ambalo linanunua umeme wa jumla kupeleka Zanzibar limeongezewa kwa asilimia 5.7% ya bei ya umeme.
Hata hivyo ongezeko hilo halitaathiri wateja wa majumbani ambao matumizi yao hayazidi uniti 75 kwa mwezi.
Kundi la TIB linalohusisha viwanda vidogo, mabango na minara ya mawasiliano litakua na tozo ya mwezi ya shilingi 5,520.
Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), linaendelea kufanya maboresho ya miundombinu ya umeme na kutekeleza miradi mipya ya kuunganisha wateja ili kuboresha huduma za umeme nchini.
COMMENTS