MAKAMU WA RAIS ASAFIRI NA BOMBADIER Q400 NEXTGEN KUTOKA DAR MPAKA MWANZA
HomeJamii

MAKAMU WA RAIS ASAFIRI NA BOMBADIER Q400 NEXTGEN KUTOKA DAR MPAKA MWANZA

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea tiketi ya kusafiria muda mfupi kabla ya kusafir...






 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea tiketi ya kusafiria muda mfupi kabla ya kusafiri kuelekea Mwanza na abiria wa kawaida kwa ndege mpya ya Bombardier Q400 NextGen kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbalawa(kushoto) na Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania Mhandisi Ladisaus Matindi.



  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akizungumza na waandishi  wa habari muda mfupi kabla ya kupanda ndege mpya za Bombardier Q400 NextGen kuelekea mkoani Mwanza kwenye ziara ya kikazi.


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanya kazi wa
ndege mpya za Bombardier Q400 NextGen kuelekea mkoani Mwanza kwenye
ziara ya kikazi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwasalimu abiria waliosafiri nae kwenye ndege mpya ya Bombadier
Q400 ya shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) akitokea Dar es Salaam
kuelekea jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi.


                                           ........................................................



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Mwanza ambapo kwa mara ya kwanza umetumia usafiri ya ndege ya Shirika la Ndege
la Tanzania (ATCL) aina ya bombardier Q400 kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi wa habari katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam kabla ya kusafiri na
baada ya kuwasili mkoani Mwanza amewahimiza wananchi kutumia usafiri wa ndege
za ATCL kwa sababu ni wa bei nafuu na usafiri wake ni wa uhakika.

Amesema kwa kutumia ndege ya ACTL imemsaidia kupunguza gharama kubwa ya usafiri kwa kutumia ndege za binafsi za kukodi kwa ajili ya safari za kikazi za ndani ya nchi.
“Ni ndege zetu ni fahari yetu zipo Tanzania ni lazima sisi Watanzania tuzitumie ipasavyo kusafiria ndio maana na mimi leo nimeamua kutumia usafiri wa ATCL kwa sababu ni mzuri na wa uhakika

Makamu wa Rais amesema amefurahi kusafiri kwa mara ya kwanza na ndege hiyo kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza na amehimiza viongozi na wananchi kwa ujumla kutumia usafiri wa ndege za ATCL ili kulipa nguvu shirika hilo katika ufanyaji wake wa kazi kwa
viwango bora zaidi.

Mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Mwanza, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali na wa vyama vya siasa ambao waliongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.


Akiwa mkoani Mwanza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya kikazi siku NNE mkoani humo katika  wilaya za Ukerewe,Ilemela,Nyamagana,
Misungwi,Kwimba na Magu mkoani Mwanza.
Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MAKAMU WA RAIS ASAFIRI NA BOMBADIER Q400 NEXTGEN KUTOKA DAR MPAKA MWANZA
MAKAMU WA RAIS ASAFIRI NA BOMBADIER Q400 NEXTGEN KUTOKA DAR MPAKA MWANZA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiGWimYfHEyLQXUAPyl7Jo4Cqv77tYVC1OB-vF2h3dDazkK5Uqz7NPYTL-3ZlBPKjagoxwJLSLlCqjFulrc_ecPdFDtoYmHn9kxGqwQpHRIjxpD_0TtMXnRJUl6rBfemyS7qy_B2d-oek/s640/7.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiiGWimYfHEyLQXUAPyl7Jo4Cqv77tYVC1OB-vF2h3dDazkK5Uqz7NPYTL-3ZlBPKjagoxwJLSLlCqjFulrc_ecPdFDtoYmHn9kxGqwQpHRIjxpD_0TtMXnRJUl6rBfemyS7qy_B2d-oek/s72-c/7.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/11/makamu-wa-rais-asafiri-na-bombadier.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/11/makamu-wa-rais-asafiri-na-bombadier.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy