WAKUU WA NCHI 6 ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA KWA KIKAO CHA DHARULA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Mwenyekiti wa Mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Rais wa Jamhuri ya Muun...







Mwenyekiti wa Mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (wa tano kutoka kushoto) akiimba wimbo wa Afrika Mashari na viongozi wenzake wa jumuiya hiyo kutoka Rwanda, Burundi, Sudani ya Kusini, Kenya, Burundi na Rwanda.

 Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakiimba wimbo wa Jumuiya hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya hiyo Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) wakati wa kikao cha Dharula cha 17 cha Jumuiya hiyo leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Kutoka (kulia) ni Rais Paul Kagame wa Rwanda, Rais Yoweri Museveni wa Uganda (wa pili kutoka kushoto) na Naibu Rais wa Kenya, William Ruto.   
Mwenyekiti wa Mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, akitoa taarifa fupi ya mkutano huo leo jijini Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa sasa wa Jumuiya ya Afrika Masharika (EAC) ambaye ni Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akiongoza kikao cha dharula cha 17 cha nchi za Jumuiya hiyo leo Ikulu jijini Dar es salaam.Kikao hicho pamoja na mambo mengine kimejadili kuhusu hali ya amani nchini Burundi na Sudani ya Kusini, ulindaji wa viwanda vya EAC, Makusanyo ya kodi ya bidhaa toka nje kupitia Mkataba wa EPA na suala la ushuru
na forodha. Kushoto ni Rais Yoweri Museveni wa Uganda.

 Mwenyekiti Jumuiya ya Afrika Masharika (EAC) ambaye ni Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli (kulia) akiteta jambo na Rais wa Mhe. Uganda Yoweri Museveni wakati wa kikao cha Dharula cha 17 cha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akitoa hotuba fupi kwa wajumbe na wageni mbalimbali waliohudhuria kikao cha dharula cha 17 cha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo Ikulu
jijini Dar es Salaam.

 Makamu wa Rais wa Kenya Mhe. William Ruto akitoa hotuba fupi kwa niaba ya Rais wa Kenya akizitaka nchi wanachama wa Jumuiya hiyo kuongeza ushirikiano wakati wa kikao cha dharula cha 17 cha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo Ikulu jijini Dar es Salaam.
 Mjumbe maalum wa Rais wa Sudani ya Kusini Mhe. Aggrey Tisa Sabuni akizungumza kwa niaba ya Rais wa Sudani ya Kusini Jenerali Salva Kiir Mayardit wakati wa kikao cha dharula cha 17 cha nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Mjumbe huyo amewashukuru viongozi wa nchi za Afrika Mashariki kwa kuiruhusu Sudani ya Kusini kujiunga na Jumuiya hiyo.
Rais wa Rwanda Paul Kagame akitoa salamu zake kwenye mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

 Naibu Katibu Mkuu Mteule wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Christopher Bizivamwo akiapishwa mbele ya Jaji wa Mahakama ya Afrika Mashariki tayari kwa kuanza kutekeleza majukumu ya Jumuiya hiyo kwa kipindi cha miaka 3 wakati wa kikao cha dharula cha 17 cha EAC kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kutoka Tanzania Balozi Augustino Mahiga
(kushoto) na Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi na Mwakilishi wa Rais wa Burundi
Mhe. Balozi Alain Aime Nyamitwe wakifuatilia kikao cha dharula cha 17 cha
Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.


Waziri wa Mambo ya Nje wa Burundi na Mwakilishi wa Rais wa Burundi katika kikao cha dharula cha 17 cha Jumuiya ya Afrika Mashariki kilichofanyika Ikulu jijini Dar es salaam leo Mhe. Balozi Alain Aime Nyamitwe akiwasilisha salam za Rais wa nchi hiyo Pierre Nkurunzinza.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein akitoa salamu zake kwenye mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt Libérat Mfumukeko akifungua Mkutano wa 17 wa Viongozi Wakuu wa Nchi
Wanachama wa Jumuiya hiyo leo jijini Dar es Salaam.


  Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na baadhi ya wabunge wa Jumuiya hiyo wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa kikao cha dharula cha 17 cha Jumuiya hiyo kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Kikao cha dharula cha 17 cha Jumuiya hiyo kikiendelea chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akiongoza kikao hicho Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wastaafu wa Tanzania na wale wa Jumuiya hiyo mara baada ya kumalizika kwa kikao cha dharula cha 17 cha Jumuiya hiyo kilichofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
 Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakijadiliana masuala mbalimbali mara baada ya kumalizika kwa Kikao cha dharula cha 17 cha Jumuiya hiyo kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye ni Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao nchini Tanzania wakifuatilia Kikao cha dharula cha 17 cha Jumuiya hiyo kilichokuwa kikiongozwa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ambaye ni Rais wa Tanzania  Dkt. John Pombe
Magufuli Ikulu jijini Dar es salaam leo. (Picha/Aron
Msigwa na Hussein Makame).

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: WAKUU WA NCHI 6 ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA KWA KIKAO CHA DHARULA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
WAKUU WA NCHI 6 ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI WAKUTANA KWA KIKAO CHA DHARULA JIJINI DAR ES SALAAM LEO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNfRJQfvO4qsziZUcY4C1alr2Mird0kUtdw4nT3bGlQeqUoqADNz94h5kZRDKulwPYPoo-NXHjrYBXK-aPLf8B3J8wGA-HBucQIcHlFu4LxjYMW_3OTJ_eOI4NNmC0QF3XkY1Wwuegm3ob/s640/IMG_6.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiNfRJQfvO4qsziZUcY4C1alr2Mird0kUtdw4nT3bGlQeqUoqADNz94h5kZRDKulwPYPoo-NXHjrYBXK-aPLf8B3J8wGA-HBucQIcHlFu4LxjYMW_3OTJ_eOI4NNmC0QF3XkY1Wwuegm3ob/s72-c/IMG_6.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/09/wakuu-wa-nchi-6-za-jumuiya-ya-afrika.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/09/wakuu-wa-nchi-6-za-jumuiya-ya-afrika.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy