KOREA KUSINI YATOA BILIONI NNE KUJENGA KITUO CHA TAARIFA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI

Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo kwa Afrika katika B u nge la Korea Kusini wakiwasili katika uwanja mdogo wa ndege uliopo katika Hifadh...






Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo kwa Afrika katika Bunge la Korea Kusini wakiwasili katika uwanja mdogo wa ndege uliopo katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. 

Meneja Masoko wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA),Victor Ketance akipokea ugeni wa wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema akipokea ugeni wa wajumbe kutoka Bunge la Korea Kusini walipotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kutizama eneo la uwekezaji wa kituo cha kisasa cha taarifa za hifadhi hiyo.
 
Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti (SENAPA) William Mwakilema akisalimiana na wadau wa utalii,Zainabu Ansel, Mkurugenzi wa kampuni ya Utalii ya Zara (katikati) na Mkurugenzi wa Kibo Safari's Willy Chamburo (kushoto) waliokuwepo uwanjani hapo.
 
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kibo Safari's,Willy Chamburo (katikati) akizungumza jambo na kiongozi wa ugeni wa Korea Kusini Won Yul Chui (kushoto) baada ya kukutana katika uwanja mdogo wa ndege uliopo Hifadhi ya Taifa ya Serengeti .kulia ni Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti William Mwakilema. 

Wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Afrika katika Bunge la Korea Kusini wakitia saini katika kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kuangalia eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha  kisasa cha taarifa za hifadhihiyo.

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, William Mwakilema (kushoto) akizungumza na Wajumbe wa  kamati ya Maendeleoo ya Afrika ya Bunge la Korea Kusini waliofika katika Hifadhi hiyo kwa ajili ya ufuatiliaji wa maenedeleo ya kuanza kwa mradi wa ujenzi wa kituo cha kisasa cha Taarifa katika Hifadhi hiyo.

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,William Mwakilema akiongoza Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini walioko katika kamati ya Maendeleo ya Afrika kutembelea maeneo kutakapo jengwa kituo cha kisasa cha taarifa. 

Moja ya eneo lilipo sasa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo inatumika kutoa taarifa kwa njia ya picha za video za Hifadhi hiyo. 

Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakitizama picha ya Hayati Baba wa Taifa, Mwl Julius K. Nyerere akiwa na rafiki yake  Prof. Bernhard Grzimek huku wakipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti,William Mwakilema.

Ujumbe wa Wabunge wa Bunge la Korea Kusini wakipata maelezo katika michoro ya kituo cha kisasa cha taarifa katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti.

Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,William Mwakilema akitoa zawadi kwa wajumbe wa Bunge la Korea Kusini mara baada ya kutembelea eneo kutakapo jengwa kituo cha kisasa cha taarifa katika hifadhi hiyo.
Wajumbe wa Bunge la Korea Kusini wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na watumishi wa Shirika la Hifadhhi za Taifa (TANAPA ) na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

(Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog Kanda ya Kaskazini).


Hifadhi ya Taifa  ya Serengeti kwa kushirikiana na  serikali  ya
Korea  ya Kusini imeanza mchakato wa ujenzi  wa  kituo
cha  kimataifa cha kutunza tarifa za  mienendo  ya  Wanyamapori kitakachojulikana kama Serengeti Internatinal Media Centre.






Kituo hicho kinachotarajiwa kugharimu zaidi  shilingi bilioni nne kitajengwa katika Hifahi ya Taifa ya Serengeti .


Tayari serikali  ya  Korea  Kusini   imeshatuma
wajumbe  wake  kuja  nchini  tanzania  kujionea
eneo  kitakapojengwa  kituo  hicho  na  kukamilisha
taratibu  nyingine  muhimu ambapo kiongozi wa wajumbe hao Park
Joosung  amesema mradi huo ni mwendelezo  wa ushirikiano wa Korea Kusini na Tanzania katika kuimarisha uhifadhi.



Akizungumza na  ujumbe  huo  mkuu wa hifadhi ya taifa ya serengeti Wiliam Mwakilema  amesema kituo hicho kikikamilika kitaongeza chachu utalii na kitatoa fursa kwa wageni kuona aina nyingi zaidi za wanyama.

Naye mratibu wa ujenzi bw Victor Ketance  amesema ujenzi utaanza mwezi October mwaka huu na unatarajiwa kumalizika  baada ya miezi 14.





COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: KOREA KUSINI YATOA BILIONI NNE KUJENGA KITUO CHA TAARIFA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI
KOREA KUSINI YATOA BILIONI NNE KUJENGA KITUO CHA TAARIFA KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg9NgIwsb17WTCCqH46ubnhxZ__9BqjSClxFVlIpVKwWY1WnKIt2bgbDCAH5BJ2uhdSghn1BpMNS3A01jJ_86tmuhho5SqgrPHMGNFwCs21b13fjb0XJwcT6J-t21T2Tj7WmTJ0D4AsY0c/s640/IMG_7729+%25281024x683%2529.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg9NgIwsb17WTCCqH46ubnhxZ__9BqjSClxFVlIpVKwWY1WnKIt2bgbDCAH5BJ2uhdSghn1BpMNS3A01jJ_86tmuhho5SqgrPHMGNFwCs21b13fjb0XJwcT6J-t21T2Tj7WmTJ0D4AsY0c/s72-c/IMG_7729+%25281024x683%2529.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/08/korea-kusini-yatoa-bilioni-nne-kujenga.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/08/korea-kusini-yatoa-bilioni-nne-kujenga.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy