Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Johnson Mfinanga, (pichani), na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni hiyo, Sadick Mu...
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa ATCL Johnson Mfinanga, (pichani), na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa kampuni hiyo, Sadick Muze wamesimamishwa kazi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni uzembe.
Akitangaza uamuzi huo mjini Mbeya, Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi, na Mawasiliano, Profesa
Makamue Mnyaa Mbarawa alisema, Mfinanga na mwenzake wamechkuliwa hatua hiyo
kufuatia uzembe walioufanya wa kuteua mmoja wa marubani kati ya watano waliotakiwa
kuwa na vigezo vinavyokubalika ilihatimaye washiriki mafunzo zaidi ya urubani
kwa ajili ya kurusha ndege mpya mbili za serikali zinazotarajiwa kununuliwa
miezi michache ijayo.
“Mmoja
wa marubani hawa hajatimiza vigezo kwa hivyo nimeamua kuwsimamisha kazi.”
Alisema Profesa Mbarawa.
COMMENTS