Na Mwandishi Wetu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ameizindu...
Na Mwandishi Wetu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Ajira na
Watu wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama ameizindua rasmi Bodi ya
Wadhamini wa Hifadhi ya Jamii wa NSSF Julai 5, 2016 Dar es Salaam.
Bodi hiyo
imezinduliwa rasmi na kujadili mambo muhimu ikiwa ni kufikia malengo ya mfuko
huo kwa kuzingatia masuala ya Utawala bora na ushirikiano ili kuchangia kukua
kwa uchumi wa wananchi na kusaidia mahitaji ya wanachama wa mfuko huo.
Mhe. Mhagama
aliahidi kutoa ushirikiano wake kwa Bodi hii mpya ili kusaidia majukumu yote na
kuhakikisha mafanikio yaliyopo yanakuwa ni chachu ya kuongeza kasi ya kufanya
vizuri zaidi ili kuifikisha mahali pazuri zaidi.
“Ninawaahidi
kuwapa ushirikiano wa hali na mali na kuamini kuwa Prof. Wangwe ameaminiwa na
kupewa dhamana ya kutufikisha mahali fulani kwa kuisaidia bodi hii
iliyozinduliwa rasmi leo.”Alisisitiza Mhe.Mhagama.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Prof.Samwel Chacha Wangwe alieleza kuwa, watajikita kwa
kusaidia maeneo muhimu yenye changamoto kwa kuhakikisha wanaboresha na kuongeza
wanachama wa Mfuko huo.
“eneo la Utawala
bora utakuwa msingi wa kusaidia mfuko uwe imara kwa kuzingatia kuwapa
kipaumbele wanachama ili kuendana na kasi ya kukuza uchumi kwa kuzingatia
kaulimbiu ya hapa kazi tu” Alisema Prof.Wangwe.
Mhe.Mhagama
alimalizia kwa kuwashukuru wajumbe wote kwa kufika na kushiriki katika uzinduzi
huo, “nitoe shukrani zangu za dhati kwa wajumbe wote na kuwaomba tuwe kitu
kimoja ili kuhakikisha shirika linatumia rasilimali zake ipasavyo ili kuwa na
mapato ya kutosha.” Alisisitiza Mhe. Mhagama.
COMMENTS