UZINDUZI NA MAKABIDHIANO YA VIFAA VYA USAFI KWA MACHINGA JIJINI MWANZA WAGUBIKWA NA DOSARI YA UBADHIRIFU.

Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Machinga mkoani Mwanza-SHIUMA, Matondo Masanja, akizungumza hii leo katika hafla ya kukabidhi v...









Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Machinga mkoani Mwanza-SHIUMA, Matondo Masanja, akizungumza hii leo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) vyenye thamani ya Shilingi Laki Sita, kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi. Hafla hiyo imeambatana na Kauli Mbiu isemayo "Machinga Kukaa Katika Mazingira Safi Inawezekana, Tusonge Mbele Kwa Usafi".
Na BMG




Shughuli ya uzinduzi na makabidhiano ya vifaa vya usafi ambavyo ni diaba za kukusanyia uchafu pamoja na fagio kwa machinga wa Makoroboi Jijini Mwanza, imeingia dosari baada Mwenyekiti wa Shirika la Machinga mkoani Mwanza SHIUMA, kutofautiana kauli na Katibu wake, juu ya matumizi ya fedha za mkopo zilizotolewa na halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Hayo yamejili baada kusomwa kwa risala ya machinga katika shghuli hiyo iliyofanyika hii leo katika eneo la Makoroboi, bila kuainisha kwamba SHIUMA pia ni miongoni mwa vikundi vilivyonufaika na mikopo midogo midogo kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza.

Hali hiyo ilisababisha diwani wa Kata ya Nyamagana na Naibu Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha, kuhoji ni kwa nini SHIUMA haikuweka bayana kupokea mkopo wa Shilingi Milioni Moja kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza, hali iliyosababisha machinga kupiga makelele kwa madai kwamba uongozi wa SHIUMA unatumia ndivyo sivyo pesa bila kuwanufaisha wanachama.

Alipotakiwa kutolea ufafanuzi suala hilo, Katibu wa SHIUMA,Venatus Anatory, alikiri uongozi kupokea mkopo wa shilingi Milioni Moja kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kwamba Shilingi Laki Sita kati ya fedha hizo, zilitumika kununua vifaa hivyo vya usafi huku Mwenyekiti wa Shiuma,Matondo Masanja, akisema fedha za mkopo bado zipo na kwamba baadhi ya wanachama watanufaika na fedha hizo kwa njia ya mkopo.

Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mabula, ambae alikuwa mgeni rasmi katika shughuli hiyo, amewahimiza viongozi wa Shiuma katika kikao cha utendaji kitakachoketi ijumaa ya wiki hii, kuhakikisha fedha za mkopo zinakopeshwa kwa wanachama na si kufanya manunuzi ya vifaa vya usafi kama Katibu alivyoeleza na kwamba viongozi hao wahakikishe wanakuwa wawazi katika mapato na matumizi ya fedha za wanachama.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula, akizungumza hii leo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kulia), akizungumza hii leo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Shirika la Umoja wa Machinga mkoani Mwanza, Matondo Masanja.
Diwani wa Kata ya Nyamagana na Kaimu Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha (kushoto), akizungumza hii leo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Katibu wa SHIUMA, Venatus Anatory, akizungumza hii leo katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Ombeni Mbise (katikati) akisoma risala ya machinga Jijini Mwanza kwa niaba ya Katibu wa SHIUMA, katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM Taifa, Mkoa wa Mwanza, akitoa salamu zake katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Francis Sisamo ambae ni Katibu wa CCM Kata ya Nyamagana Jijini Mwanza, akitoa salamu zake katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Nasoro Hemed ambae ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyamagana Magharibi Jijini Mwanza, akitoa salamu zake katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Mkuu wa Kituo cha Polisi Makoroboi Jijini Mwanza, akitoa salamu zake katika hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Edmund Kaiza ambae ni Meneja wa Kituo cha Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi mkoani Mwanza, akifafanua namna kituo hicho kilivyojipanga kuwasaidia Machinga Jijini Mwanza kujikomboa kiuchumi ikiwemo utayari wake wa kujenga Soko Kubwa kwa ajili ya Machinga (Machinga Complex) katika eneo la Makoroboi Jijini Mwanza ikiwa mamlaka husika zitakubaliana na wazo hilo ambalo limeidhinishwa na Machinga.

Baadhi ya Machinga Jijini Mwanza wakifuatilia kwa ukaribu hafla ya kukabidhi vifaa vya usafi (diaba na fagio) kwa wafanyabiashara ndogondogo Jijini Mwanza (Machinga) ili kusaidia kuweka mazingira yao katika hali ya usafi.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kushoto), akimkabidhi Mwenyekiti wa SHIUMA, Matondo Masanya, diaba kama ishara ya Uzinduzi wa Vifaa vya Usafi kwa ajili ya Machinga Jijini Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kushoto), akimkabidhi Mwenyekiti wa SHIUMA, Matondo Masanya, diaba kama ishara ya Uzinduzi wa Vifaa vya Usafi kwa ajili ya Machinga Jijini Mwanza.
Mbunge wa Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza, Stanslaus Mabula (kushoto), Diwani wa Kata ya Nyamagana na Kaimu Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Bhiku Kotecha (katikati), wakimkabidhi Mwenyekiti wa SHIUMA, Matondo Masanya (kulia), fagio kama ishara ya Uzinduzi wa Vifaa vya Usafi kwa ajili ya Machinga Jijini Mwanza.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: UZINDUZI NA MAKABIDHIANO YA VIFAA VYA USAFI KWA MACHINGA JIJINI MWANZA WAGUBIKWA NA DOSARI YA UBADHIRIFU.
UZINDUZI NA MAKABIDHIANO YA VIFAA VYA USAFI KWA MACHINGA JIJINI MWANZA WAGUBIKWA NA DOSARI YA UBADHIRIFU.
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg_hyhlrKrxSmdGmmPFVyfL9H_uox5g1yfdwdyZkLgQqnMoYBRi2W65LHs-QpGW-ySXD1Je4TMIbp5lC3RS4EeB8JGulhhXIFVnyA9Qn7ShZxJfxxLYAuhX5pZPU9zdczJkgzNxguTeVh4/s640/1.JPG
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEg_hyhlrKrxSmdGmmPFVyfL9H_uox5g1yfdwdyZkLgQqnMoYBRi2W65LHs-QpGW-ySXD1Je4TMIbp5lC3RS4EeB8JGulhhXIFVnyA9Qn7ShZxJfxxLYAuhX5pZPU9zdczJkgzNxguTeVh4/s72-c/1.JPG
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/07/uzinduzi-na-makabidhiano-ya-vifaa-vya.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/07/uzinduzi-na-makabidhiano-ya-vifaa-vya.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy