SAKATA LA MATIBABU YA WAGONJWA WA SICKLE CELL (SELIMUNDU), MUHIMBILI, SERIKALI WATOA MSIMAMO

Bi. Yasmin Razak, akiwa amembeba mtoto anayeugua maradhi ya Selimundu (Sickle cell), wakati wa mkutano wa waandishi wa habar...













Bi.Yasmin Razak, akiwa amembeba mtoto anayeugua maradhi ya Selimundu (Sickle cell), wakati wa mkutano wa waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mama huyu ambaye mwanaye pia anaugua ugonjwa huo, lakini
matibabu yake anapatanchini Uingereza, ameamua kusimama kidete kutetea wagonjwa wa selimundu kuendelea kuhudumiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na kumuomba
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, kuingilia kati mpango wa kuwaondoa wagonjwa 6,000 hospitalini hapo na kuwapeleka kwenye hospitali wanakotoka.








NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said, MNH
HOSPITALI ya Taifa Muhimbili, MNH, na
Serikali kupitia Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, wametoa msimamo kuhusu sintofahamu iliyowakumba wagonjwa wa sickle cell (Selimundu), waliokuwa wakipatiwa matibabu kwenye hospitali hiyo kubwa kabisa hapa nchini.

Kauli ya MNH kuhusu tiba ya Selimundu
Tunapenda umma uelewe kuwa huduma hii haijasitishwa na wala
Hospitali haitasitisha utoaji wa huduma hiyo.” Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitali hiyo, Profesa
Lawrence M. Museru, amewaambia waandishi
wa habari leo Aprili 25, 2016.

Hofu ya wagonjwa
Awali baadhi ya wazazi wa watoto wenye kuugua maradhi ya Selimundu, wakiongozwa na Bi.Yasmin Razak, wameonyesha hofu ya maisha ya watoto wao kufuatia taarifa kuwa jumla ya wagonjwa 6,000 waliokuwa wakipatiwa matibabu ya Selimundu hospitalini
hapo chini ya mradi wa utafiti wa ugonjwa huo, “Welcome Trust.” Watarudishwa kwenye utaratibu wa matibabu chini ya muongozo wa Wizara ya Afya kwenye hospitali walikotoka, kwa vile mradi huo wa utafiti umemaliza kazi yake Machi 31, 2016.

Gharama za matibabu ya Selimundu
Ni kweli kwamba takribani miaka kumi kulikuwa na mradi uliokuwa ukifadhili matibabu pamoja na utafiti wa wagonjwa wa selimundu,  Mradi huu kwa sababu ya utafiti ulihitaji wagonjwa wote wa selimundu kuja Muhimbili kwa
ajili ya utafiti na tiba. Hivyo basi hali hii ilisababisha wagonjwa wengi wanaohitaji huduma ya selimundu kuja Hospitalini hapa licha ya kwamba mahitaji yao hayakuhitaji utalaamu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Amesema Profesa Mseru.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Dkt. Doroth Gwajima, amewaondoa hofu wagonjwa kuhusu gharama za matibabu hayo ambapo alisema, muongozo wa serikali uko wazi, wazee na watoto watapatiwa matibabubure na wengine
wanachangia kupitia bima ya afya na fedha taslim, hata hivyokwa wale ambao hawatakuwa na uwezo utaratibu wa kuwapatia matibabu upo.
Hofu ya wagonjwa
Kutokana na mazoea ya muda mrefu ya kupatiwa matibabu bure ya ugonjwa huo wa selimundu, na hasa ikizingatiwa hakuna tiba ya kuuponya kabisa ugonjwa huo, wagonjwa wamehoji watawezaje kumudu kulipia gharama hizo?

Wazazi wa watoto wanaougua ugonjwa huo, wametmuomba Rais John Magufuli, kuingilia kati suala hilo ili kuokoa maisha ya wagonjwa hao ambao kwa asili ya ugonjwa wenyewe, mgonjwa hupata maumivumakali mwilini, mabadilikoya viungo, na
wakati mwingine kupungukiwa damu mara kwa mara.

Kauli ya Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam
“Hospitali zote za Manispaa ya jiji la Dar es Salaam, na hata zile zilizopo mikoani na wilayani, zina uwezo wa kutoa huduma za ugonjwa wa Selimundu, na hata ikionekana kuwa mgonjwa anahitaji matibabu zaidi, rufaa huandaliwa na mgonjwa
hupelekwa kwenye hospitali kubwa zaidi ili kupatiwa matibabu yanayofaa.” Dkt.Grace Magembe, Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam.




 Bi.Getrude Thadeo kutoka Tabora, akiwa na mtoto wake wa miaka 13, Angela Romwadi, ambaye anaugua Selimundu
 Bi.Mkami Titus wa Temeke jijini Dar es Salaam akiwa na mtoto wake Shedrack Yahaya(4), anayeugua selimundu
 Bi.Walivyo Mohamed kutoka Rufiji mkoani Pwani, akiwa na mtoto wake wa miaka 4, Siraji Majid

 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Hospitaliya Taifa Muhimbili (MNH), Profesa Lawrence Museru, akiwa na Mkuu wa Idara ya Magonjwa na Afya ya Watoto ya MNH, Dkt. Mary B. Charles, akizungumza na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa yake mapema leo Aprili 25, 2016
 Profesa Museru
 Dkt. Doroth Gwajima, Mkurugenzi wa Huduma za Tiba Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.
 Profesa Museru na timu yake wakati akiongea na waandishi wa habari.
 Dkt.Grace Magembe, Mganga Mkuu wa jiji la Dar es Salaam.
 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Elineema Meda. Dkt. Meda ni mmoja wa walioshiriki kwenye utafiti wa ugonjwa huo wa Selimundu chini ya mradi wa Welcome Trust.
 Bi. Yasmin wakati wa mkutanona waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Baadhiya akina mama wakiwa na watoto wao wanaosumbuliwa na maradhi ya Selimundu. Hapa wakihudhuria mkutano na waandishi wa habari ulioitishwa na Bi. Yasmin ambaye ameamua kuwasimamia na kuwasemea wagonjwa wa Selimundu.


Bi. Yasmin (katikati), akiwa na Bi.Walivyo Mohammed na mtoto wake Siraji (kushoto) na Bi. Getrude Thadeona mtoto wake Angela.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: SAKATA LA MATIBABU YA WAGONJWA WA SICKLE CELL (SELIMUNDU), MUHIMBILI, SERIKALI WATOA MSIMAMO
SAKATA LA MATIBABU YA WAGONJWA WA SICKLE CELL (SELIMUNDU), MUHIMBILI, SERIKALI WATOA MSIMAMO
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiBCtayQGe1jIQA5c8JKZ2Hyo3pNQk5I-EOw6uOOfBKj9NNc-o7Ti50gMp-5VgH9sol5YiIl-cA3Dr1dGkWCYiBOGgHukhrlI2J8UmQZvZgJYCBDqmJCQ0Rd4nyaUx5BIxqRt4GP4BQCLLp/s640/b1.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiBCtayQGe1jIQA5c8JKZ2Hyo3pNQk5I-EOw6uOOfBKj9NNc-o7Ti50gMp-5VgH9sol5YiIl-cA3Dr1dGkWCYiBOGgHukhrlI2J8UmQZvZgJYCBDqmJCQ0Rd4nyaUx5BIxqRt4GP4BQCLLp/s72-c/b1.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/04/sakata-la-matibabu-ya-wagonjwa-wa.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/04/sakata-la-matibabu-ya-wagonjwa-wa.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy