TAARIFA; YA KIFO CHA MEJA JENERALI MSTAAFU

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA Simu ya Upepo   : “ N G O M E ”         Makao Makuu ya Jeshi, Simu ya Mdomo : DSM  2215...





K:\logo[3].png

JESHI LA ULINZI LA WANANCHI WA TANZANIA

Simu ya Upepo   : “N G O M E        Makao Makuu ya Jeshi,
Simu ya Mdomo : DSM  22150463    Sanduku la Posta 9203,
Telex            : 41051            DAR ES SALAAM,  22 Machi, 2016.
Tele Fax        : 2153426
Barua pepe    : ulinzimagazine@yahoo.co.uk
Tovuti        : www.tpdf.mil.tz
       
Taarifa ya kifo kwa Vyombo vya Habari
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) lina sikitika kutangaza kifo cha Meja Jenerali January Claudio Kisanko (mstaafu) kilichotokea tarehe 21Machi 2016,  
Meja Jenerali January Kisanko (mstaafu) alizaliwa mwaka 1945 katika kijiji cha Mkima, Tarafa ya Lyangalile, Wilaya ya Sumbawanga. Alipata Elimu ya Msingi Mkoani Rukwa na baadaye elimu ya Sekondari katika Shule ya Sekondari ya wavulana Agakhan ambayo kwa sasa ni shule ya Sekondari Tambaza, hadi alipohitimu kidato cha Sita mwaka 1966.
Marehemu Meja Jenerali January Claudio Kisanko (Mstaafu) alijiunga na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania tarehe 31 Mei, 1967 na kutunukiwa Kamisheni tarehe 24 Julai, 1969.Marehemu alilitumikia Jeshi kwa muda wa miaka 35 na mwezi 1 hadi alipostaafu utumishi Jeshini tarehe 30 Juni 2002.
Katika utumishi wake marehemu alishika Madaraka mbalimbali Ikiwemo Kamanda wa patuni Nachingwea 1969 hadi 1970, Kamishina wa Mipango na Sera katika Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa 2001, madaraka ambayo alikuwa nayo hadi alipostaafu tarehe 30 Juni 2002.
Meja Jenerali January Kisanko enzi za uhai wake.

Marehemu Meja Jenerali January Kisanko (Mstaafu) alifariki dunia tarehe 21 Machi, 2016 katika Hospitali ya TMJ Dar es Salaam. Ameacha Mke na Watoto. Mwili wa marehemu unatarajiwa kuagwa rasmi tarehe 28 Machi, 2016 kuanzia saa 3:00 asubuhi katika Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo na mazishi yatafanyika katika makaburi ya Kinondoni Jijini Dar es Salaam, saa 10:00 jioni.


MUNGU AILAZE MAHALI PEMA PEPONI ROHO YA MAREHEMU
MEJA JENERALI JANUARY KISANKO (MSTAAFU)
AMINA


Imetolewa na Kurugenzi ya Habari na Mahusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.
Kwa Mawasiliano zaidi: 0784-477638


COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: TAARIFA; YA KIFO CHA MEJA JENERALI MSTAAFU
TAARIFA; YA KIFO CHA MEJA JENERALI MSTAAFU
https://lh6.googleusercontent.com/XQ3pwlJxvPHJmVjYW6_zSoMEStOmxeWFz7jvCBP8Kreply8xRdvQxhKvcv0-t8jzpBiX8g12LmzZ_McnG8PHsV2X5hrIOpIZWcuAiw_e8k26yG9h8ondwPQLNb4155SM4zhGtaNtuCcgzG-fAQ
https://lh6.googleusercontent.com/XQ3pwlJxvPHJmVjYW6_zSoMEStOmxeWFz7jvCBP8Kreply8xRdvQxhKvcv0-t8jzpBiX8g12LmzZ_McnG8PHsV2X5hrIOpIZWcuAiw_e8k26yG9h8ondwPQLNb4155SM4zhGtaNtuCcgzG-fAQ=s72-c
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/03/taarifa-ya-kifo-cha-meja-jenerali.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/03/taarifa-ya-kifo-cha-meja-jenerali.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy