AJIB AKABIDHIWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA

Mshindi wa mwezi wa Disemba, 2015 ni Ibrahim Ajib ambapo amepata kura nyingi zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na sok...






Mshindi wa mwezi wa Disemba, 2015 ni Ibrahim Ajib ambapo amepata kura nyingi zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.

Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015.
Akikabidhiwa tunzo pamoja na pesa taslim Tsh 500,000/= na  Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Richard Mvula,  Ibrahim Ajib alisema “kila siku nimekuwa nikiendelea kujitahidi kufanya vizuri zaidi ili nami ifike siku niweze kukabidhiwa tunzo hii, kwakweli ni heshima kubwa sana kwangu, napenda kuchukua fursa hii kuupongeza uongozi mzima wa Simba kwa kuanzisha utaratibu huu, pia napenda kuwashukuru mahsbiki wangu ambao wamenipigia kura, wachezaji wenzangu kwenye kikosi cha Simba ambao kila siku tumekuwa tukishirikiana katika kazi yetu hii ya mpira, napenda kushukuru kwa sapoti kubwa ninayoipaa kutoka kwa familia yangu na mwisho napenda kumshukuru Allah kwa kuendelea kunibariki na neema zake kila siku”

Akimakabidhi tunzo hiyo Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group Richard Mvula alisema “kama mtakumbuka utaratibu huu ulianzishwa kwa ajili ya kuwapa motisha wachezaji wetu na sasa umekuwa ni utamaduni wetu katika kuwapongeza na kuonesha kuthamini jitihada zinazofanywa na wachezaji wetu katika kuutafuta ushindi wa msimu huu”

Napenda kuwakumbusha wanachama na wapenzi wa Simba kuendelea kuwapa sapoti wachezaji wetu kwani kwa sapoti yao ndio mafanikio ya timu yetu yanapopatikana, aliongeza Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group Richard Mvula

Akizungumza jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi Mkuu wa EAG Group, Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenzi wa Simba na wapenda michezo ndio watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460, Ni wale tu ambao wamejiunga na Simba News kupitia mtandao wa Voda na Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa Simba”.

Tukumbuke kuwa unaweza kumchagua mchezaji bora wa mwezi ukiwa umejiunganisha na huduma ya Simba News kwa kutuma jina la mchezaji kwenda namba 15460. Zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi wa Januari, 2016 litaanza  February 29  2016. Piga kura mara nyingi zaidi kuweza kumpata mchezaji wako bora wa Mwezi Januari, 2016.

Simba News ni huduma iliyoanzishwa na Simba ili kuwapa wapenzi wa Simba habari mbalimbali za Simba popote pale walipo ikiwemo matokeo, majina ya wachezaji wanaocheza mechi, usajili na habari nyingine za klabu ya Simba. Kujiunga na Simba News tuma neno Simba kwenda namba 15460 ni maalum kwa Tigo na Vodacom.

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: AJIB AKABIDHIWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA
AJIB AKABIDHIWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVoZz3-9gDNDrRcmrR2P3NtvM0d7nm9y4KW1h3Sxr6g2H4X-l8sL-Q5CDcUuesuUExIODm3N-BeGrHljzJuh4jRVDQaQNCx-VvpEjygxDe6T1z_N8zxsHwuFgcjRDefpfpyuy9dcnl-Yeg/s640/Ajib.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgVoZz3-9gDNDrRcmrR2P3NtvM0d7nm9y4KW1h3Sxr6g2H4X-l8sL-Q5CDcUuesuUExIODm3N-BeGrHljzJuh4jRVDQaQNCx-VvpEjygxDe6T1z_N8zxsHwuFgcjRDefpfpyuy9dcnl-Yeg/s72-c/Ajib.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2016/02/ajib-akabidhiwa-tunzo-ya-mchezaji-bora.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2016/02/ajib-akabidhiwa-tunzo-ya-mchezaji-bora.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy