MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU, BGML WAKABIDHI MIRADI YA THAMANI YA SHILINGI BILIONI MOJA WILAYA YA MSALALA

 MOJA kati ya majengo ya shule ya Msingi Busindi, yaliyomaliziwa kujengwa na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalal...





 MOJA kati ya majengo ya shule ya Msingi Busindi, yaliyomaliziwa kujengwa na mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala mkoani Shinyanga. Mgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya Acacia, umekabidhi miradi minne ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi bilioni 1 ikiwa ni sera ya kampuni kujenga mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi.

NA
K-VIS MEDIA
MGODI wa dhahabu wa Bulyanhulu, BGML, Jumatatu Agosti 31, 2015, umekabidhi miradi, yenye thamani ya shilingi Bilioni Moja kwa Mamlaka ya Halmashauri ya Wilaya yaMsalala mkoani Shinyanga. Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi miradi hiyo, Meneja Mkuu wa Mgodi huo unaomilikiwa na Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia, Michell Ash, alisema, “Sisi BGML tulitoa ufadhili wa kugharimia miradi ya kijamii kwa wenyeji wetu na leo tunakabidhi miradi hiyo minne baada ya kukamilika kwake ikiwa ni ishara ya muendelezo wa utekelezaji wa ahadi zetu za kampuni kuwajibika kusaidia jamii.” Alisema
“Ninayo furaha kuu kutangaza kuwa BGML ilifadhili miradi minne kwa thamani ya shilingi Bilioni 1,100,546,766 na tunatarajia kutoa fedha zaidi mwaka huu kusaidia sekta
za Afya na Elimu.”Alifafanua
Akitoa mchanganuo wa miradi iliyogharimiwa na mgodi huo ulioko wilayani Msalala, Ash alisema, BGML ilikamilisha ujenzi wa nyumba sita za walimu wa shule ya msingi
Bugarama kwa thamani ya shilingi milioni 403,437,000, kukamilisha ujenzi wa madarasa sita na na ujenzi wa tenki la maji kwenye shule ya msingi Busindi kwa
thamani ya shilingi 129,333,860 na ukamilishaji wa ujenzi wa nyumba mbili za walimu na ofisi ya walimu shule ya msingi Busindi kwa gharama ya shilingi 137,229,200.
Miradi mingine ni Ujenzi wa visima sita vya maji huko Kakola(1) na Kakola (9), Buyange, Bushing’we, shule ya sekondari Bugarama, Mwasabuka yote ikiwa na
gharama ya shilingi 174,392,000.
Hali kadhalika BGML ilikamilisha ujenzi wa maabara ya Biolojia, Kemia na Fizikia kwenye shule ya msingi Nyikoboko ikitumia kiasi cha shilingi 256,154,706.
Akitoa shukrani za wilaya baada ya kupokea miradi hiyo, Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya alisema, ni faraja ilioje kuona wawekezaji wanaonyesha moyo wankuisaidia jamii inayozunguka
mgodi huo. “Nataka niseme, mafanikio haya tunayoyaona leo hii ni matokeo ya ushirikiano mzuri kati ya wananchi na wawekezaji, ambapo wameamua kusaidia pale wananchi wanapokwama.”
Alisema na kutoa wito kwa uongozi wa shule na maeneo yaliyokabidhiwa miradi hiyo kuitunza.
Kukabidhiwa kwa miradi hiyo ni utekelezaji wa Sera ya kampuni ya Acacia inayomiliki mgodi huo ya mahusiano mema na jamii inayozunguka migodi yake.

 Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoaniShinyanga, Benson Mpesya, Meneja Mkuu Mgodi wa Dhahabu Bulyanhulu, BGML,
Michelle Ash, (katikati) na Mkurugenzi wa Maendeleo Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, wakipapu maji wakati wa uzinduzi rasmi wa kisima kirefu cha maji kilichojengwa kwa ufadhili wa kampuni hiyo huko Bugarama. BGML, inayomilikiwa
na Kampuni ya Acacia, imekabidhi miradi mine ya elimu na maji kwa Halmashauri hiyo yote ikiwa na thamani ya shilingi Bilioni 1.
Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Msalala, ambaye pia ni
Mkuu wa Wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga, Benson Mpesya, (kushoto), akiongozana na Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu ulioko wilaya ya Msalala Mkoani Shinyanga, Michelle Ash, (katikati), na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Busindi, Joseph Misungwi, baada ya kuzindua moja kati ya nyumba kadhaa za
walimu, zilizojengwa kwa msaada wa mgodi huo. Mhgodi huo unaomilikiwa na kampuni ya uchimbaji na utafutaji madini, Acacia, umekabidhi halmashauri ya wilaya hiyo, miradi ya elimu na maji yenye thamani ya shilingi Bilioni 1, kwenye hafla hiyo iliyofanyika Agosti 31, 2015.


















Khalfan Said Photojournalist K-VIS MEDIA P.Box 77807 Mobile; +255 646-453/+255-653-813-033 Blog:http//khalfansaid.blogspot.com Dar es Salaam, Tanzania

COMMENTS

Name

analogia,2,Biashara,618,dijital,235,Jamii,3473,Magazeti,385,Michezo,334,Mikoani,1262,Moto,334,Sanaa,247,Siasa,369,Slide,10,tv,4,Uchumi,276,
ltr
item
Okandablogs: MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU, BGML WAKABIDHI MIRADI YA THAMANI YA SHILINGI BILIONI MOJA WILAYA YA MSALALA
MGODI WA DHAHABU WA BULYANHULU, BGML WAKABIDHI MIRADI YA THAMANI YA SHILINGI BILIONI MOJA WILAYA YA MSALALA
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiTF09Mi1Py6szrBxeOEmOERfpn9zYSZrv0u6HNw7_6C7STYspER2ppAw_3A3HkeGB41iXYuawRaE22dBQLhtieOmodWltYiUOmW54MTkhy2MajUJ5VqMOwn9NPNNbFMooHWn2y27Gh8DQ/s640/b9.jpg
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiTF09Mi1Py6szrBxeOEmOERfpn9zYSZrv0u6HNw7_6C7STYspER2ppAw_3A3HkeGB41iXYuawRaE22dBQLhtieOmodWltYiUOmW54MTkhy2MajUJ5VqMOwn9NPNNbFMooHWn2y27Gh8DQ/s72-c/b9.jpg
Okandablogs
https://robertokanda.blogspot.com/2015/09/mgodi-wa-dhahabu-wa-bulyanhulu-bgml.html
https://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/
http://robertokanda.blogspot.com/2015/09/mgodi-wa-dhahabu-wa-bulyanhulu-bgml.html
true
7708052459372695991
UTF-8
Loaded All Posts Not found any posts VIEW ALL Readmore Reply Cancel reply Delete By Home PAGES POSTS View All RECOMMENDED FOR YOU LABEL ARCHIVE SEARCH ALL POSTS Not found any post match with your request Back Home Sunday Monday Tuesday Wednesday Thursday Friday Saturday Sun Mon Tue Wed Thu Fri Sat January February March April May June July August September October November December Jan Feb Mar Apr May Jun Jul Aug Sep Oct Nov Dec just now 1 minute ago $$1$$ minutes ago 1 hour ago $$1$$ hours ago Yesterday $$1$$ days ago $$1$$ weeks ago more than 5 weeks ago Followers Follow THIS CONTENT IS PREMIUM Please share to unlock Copy All Code Select All Code All codes were copied to your clipboard Can not copy the codes / texts, please press [CTRL]+[C] (or CMD+C with Mac) to copy